angalia kifo cha mwanafunzi akwilina kilisababishwa na ujeuri wa wanasiasa...hatimaye mtu asiye na hatia akafa, je kama mwenyekiti asinge hamasisha maandamano ha lazima....kifo kinge tokea? hapana.
Hivyo mambo mengi wanasiasaa wanayafanya kwa kuwatoa muhanga wasio na hatia.....tunataka wawatangulize watoto zao mbele ya maandamano kama kweli wana uchungu wa kukomboa wananchi.
Watoto wao Kivipi wakati nimeshakuambia kuwa dunia hii kuna watu wameumbwa ili watetee maisha ya wengine.
Hivi nyie CCM madaraka ndio mnatoaga watoto wenu kwenda kupambana na majambazi au Magaidi?
Hivi vurugu zinatokana na Watu kupiga kura na kamapeni au zinatokana na dhuluma zinazofanywa na Wasimamizi ambao kiukweli wanapaswa kusimamia Haki.?
Hivi ni wapi ambapo hua hapatokei fujo haki inapokosekana.
Ni mpumbavu tu atakuunga mkono kwa sababu hujui gharama za watu wanaojitolea kwa ajili ya wengine ilivyokubwa.
Hata CCM wanawatangulia polisi ambao ni watoto wa maskini kwenda kuua watu na kupata maadaui huku wao wakinywa bia na kujilimbikizia mali . Haoa hao polisi akipewa rushwa ya buku mbili wanamfukuza kazi kama mbwa na kumtungia sheria ya kikokotoo. Hiyo ndiyo haki! Watu walioingia madarakani kwa rushwa na dhulma watawezaje kwenda kuongoza watu na kupinga rushwa ?
Nyie ndio mnaojiwaza tu matumbo yenu ndio maana hamjali hata ujai wa watu wengine alimradi mnapata kwa kupitia ujambaza kuuza madawa na mikataba mibovu . Nchi imejaa mikataba mibovu kwa sababu hamjali kuisoma kwa makini ili muifanyie marekebisho ,mnachoangalia ni 10% . Wabunge wa CCM hawataki uhuru wa Bunge na Bunge Live ili watete wengine. Wako pale kuangalia nafsi zao ili Mwenyekiti asije akawafukuza au kukata majina yao. Hiyo ndiyo dunia unayoitaka . Dunia ya watu wanaofanana na wanyama. Dunia ya watu ambao hata akipita na kuona Unaporwa au Kupigwa watu wakae kimya mana hayawahusu na hawawezi kuingilia kumsaidia mtu mana wanaweza wakaumizwa kwa kumtetea mwingine.
Mnataka dunia ambayo Polisi wakipigiwa siku kuwa kuna uhalifu waogope kwa sababu nao ni binadamu wanajali maisha yao na familia zao , na anayeibiwa ni mtu mwingine.
Kila unachokifurahia leo kuna watu waliumia kwa sababu hiyo.
Leo wakina Gwajima Kakobe na Wengine unaowaona wakiunga mkono fahari za Dunia na kukataa Haki na usawa kwa wanadamu huku wakihakasisha kuwa wengine ni wasaliti na hawapaswi kuishi ,wakesahau kuwa kuna waliopigania Haki ya kuabudu na uhuru wa kuabudu. Marehemu Moses kolola aliteswa sana alipoanza kuhubiri Ulokole Tanzania wakati wa Awamu ya kwanza na kuitwa mchochezi kwa sababu tu aliyakosoa makanisa makongwe na hayo ndiyo yaliyokuwa na matajiri wengi na watawala walisali huko. moses Kolola alijitoa kutetea kila anachokiamini mpaka alipokuja Mwinyi ambaye ni muislam lakini mwenye Utu na aliyeguswa na shida za wengine akaamua kuwa Kolola asibughudhiwe kwani ana uhuru wa kuamini anachoona kinafaa ,akasema Ruksa. Mwinyi akapigwa vita na wagandamizaji na waroho wa damu za watu wanaopenda kuona binadamu wenzao wakiteseka kwa umaskini na kukosa uhuru huku wao wakiwa na maisha safi.
Suala la Akwilina lilipaswa liwaguse wahusika wote.
Aliyepiga risasi binadamu mwenzake kwa sababu ya ukereketwa alipaswa awajibishwe.
Mkurugenzi aliyeacha kutimiza wajibu wake kwa haki alipaswa awajibishwe.
Mbowe aliyehamasisha maandamano bila kibali alipaswa naye awajibishwe. Hiyo ndiyo haki !! Damu ya Akwiline ,Damu ya Karume,Damu ya Dr.Sengondo Mvungi,Damu ya Alfonsi mawazo, Damu ya Wazanzibari wapatao 27 2001 , Damu ya Sokoine, Damu ya Horace Kolimba, Damu ya Azori Gwanda, Damu ya Ben Saanane iliyomwagwa kwa sababu tu ya misimamo yao na mawazo yao Hakika Mungu na asili ya Viumbe itajibu kwa vizazi vya wahusika.