CHATO: Rais Magufuli asema Serikali haitafunga mipaka wala kuwazuia watu kutoka ndani ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona

CHATO: Rais Magufuli asema Serikali haitafunga mipaka wala kuwazuia watu kutoka ndani ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona

Madhara ya kujifungia ndani na kufunga mipaka na biadhara ni makubwa kuliko madhara ya Corona yenyewe, Tuchape kazi na kuongeza tahadhari, Naungana na kulubaliana na Maamuzi sahihi ya Rais. Big up JPM, Rais Shupavu na Jasiri uhitajika kwaajili ya Maamuzi magumu katika kipindi kigumu ili kulinusuru Taifa.
Chibudee,
 
technically,
Kwa hili la kufunga nakuunga mkono kwa asilimia 100 japo tumechelewa lakini athari zinaweza kupungua kuliko hii njia tunayoitumia.

Wataalamu wa afya wangeruhusiwa kutueleza hatua sahihi za kujikinga na ugonjwa huu badala kuamuliwa na wanasiasa.

Tujiulize swali dogo Watanzania kule Makao Makuu ya Kabisa Katoliki ibada ilivyoendeshwa bila Misongamano kabisa kwa nini?
 
Kwa hili hata mimi namuunga mkono, kufunga mipaka sasa hivi kutaiweka Tanzania pabaya kuliko ilipo hivi sasa.
Mkuu kwani majirani wakifunga mipaka na sisi Tanzania hatujafunga mipaka ni faida gani tutapata?
 
Mbona kama yuko peke yake? Usalama wa viongozi wa kitaifa ni usalama wa taifa, ndio maana makamu wa rais na rais kipindi hiki lazima wana usalama wahakikishe wako salama kiafya ili taifa liwe salama, hawaonekani mara kwa mara wakiwa wamejichanganya katika jamii
Unafikiri raisi analindwa na mabodigadi waonyesha machuchu kama awo vijana wa wasafi sasa nikwambie Apo kanisa zima lina walinzi na limesha kaguliwa siku nyingi kabla kufika hapo kifupi hiyo Ni tahasisi ukijaribu kumsogele utashushwa bega kijana

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Rais Magufuli sentensi zake ziko very clear! Kwamba,

"chapa kazi pale ulipo, huku ukichukua tahadhari zinazotolewa na wataalamu wa afya"

Sasa kama wewe unaona huelewi hiyo sentensi badala yake unaona kujikinga na corona ni mpaka Rais atangeze tujifungie ndani, nakushauri usisubiri Rais atangaze bali jifungie wewe na familia yako wala hujakatazwa na hakuna mtu atakuja kukutoa ndani kwako kwa nguvu.

Kuna watu yani sijui wana akili za namna gani, yani yeye njia ya kuzuia kuenea kwa corona anaona ni kujifungia ndani basi! Wala hana mawazo mbadala zaidi ya kutaka total lock down. Hawa mimi nawaita kula kulala, lakini kwa mhangaikaji ambae anajua kula yake inatokana na kutoka kwake hawwezi hata kuwaza kujifungia ndani.

Narudia usisubiri Rais atangaze! Jifungie mwenyewe hakuna mtu atakuja kukutoa kwa nguvu.

Mods uachani huu uzi ujitegemee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
digba sowey,
Kweli mkuu maana Corona sio tishio kwa maisha ya mwanadamu. Watu waendelee kazi zao kama kawaida..kuna DC na RC wanakataza watu wasicheze mpira, kufungua Kumbi za starehe,mabaa ata kwenda fukweni...Natamani Mh.Rais awatumbue watu hao wanao toa matamko kinyume na Mh.Rais
 
Unafikiri raisi analindwa na mabodigadi waonyesha machuchu kama awo vijana wa wasafi sasa nikwambie Apo kanisa zima lina walinzi na limesha kaguliwa siku nyingi kabla kufika hapo kifupi hiyo Ni tahasisi ukijaribu kumsogele utashushwa bega kijana

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
Ulikuwa una uwezo wakujibu kuliko kutoa lugha chafu kwa watu wengine wasiohusiana katika mada hii jaribu kuwa na heshima kwa watu wengine itakusaidia Sana katika maisha.
 
Back
Top Bottom