CHATO: Rais Magufuli asema Serikali haitafunga mipaka wala kuwazuia watu kutoka ndani ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona

CHATO: Rais Magufuli asema Serikali haitafunga mipaka wala kuwazuia watu kutoka ndani ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona

Mbona kama yuko peke yake? Usalama wa viongozi wa kitaifa ni usalama wa taifa, ndio maana makamu wa rais na rais kipindi hiki lazima wana usalama wahakikishe wako salama kiafya ili taifa liwe salama, hawaonekani mara kwa mara wakiwa wamejichanganya katika jamii
sasa hapa umeandika nini mbona hueleweki ?
au ilimradi na wewe u_comment ?
 
Kwamba.....

1. Mipaka haifungwi ng'o na kwamba Watu waruhusiwe Kuingia hapa Kwetu Malawi
2. Watu hawatazuiwa Kutoka Majumbani
3. Makanisani Watu waendelee tu Kujazana
4. Tumuombe sana Mungu auondoe huu Ugonjwa
5. Tuendelee tu Kuchapa Kazi
6. Tusiogope wala tusitishane
7. Tusiwaige wengine katika Kukabiliana nao

Ndiyo maana nataka kurudi zangu tu Nyumbani Kwetu Tanzania na nitoke kabisa hapa nchini Malawi nilipo kwani kama kuna Mwaka ambao nchi ya Malawi imempata Rais wa aina yake basi ni huyu wa sasa.

Namshauri huyu Rais ' Kituko ' wa hapa nchini Malawi amuige Rais mzuri, mchapakazi, mkarimu na mkweli wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambaye kiukweli Yeye na Wasaidizi wake hasa Waziri wake wa Afya wanapambana kweli kweli katika Kukabiliana na hili Janga la COVID-19 na huenda kwa Juhudi zao za pamoja basi ama nchi yake ya Tanzania isiendelee kupata Maambukizi zaidi yatakayopelekea Vifo vingi au hata Dawa halisi ya CORONA ikatokea huko huko Tanzania.

Nawasilisha.
 
My intuition tells me
Washauri wa mh. Wamemshauri tofauti na hiki alichokisema sidhani kama sisi watz tuko so special au exception inapokuja swala la Covid 19. Sema tu kwasabababu yeye Ni final say.
Hatuombei mabaya ila inawezekana kuna majuto mbeleni.


Cha msingi kila mmoja achukue tahadhari because sidhani Kama WHO wanaweza predict uongo kuhusu bara hili kwa 80%

Tuna safari ndefu Sana🚶🚶
 
Kwani wataalamu wa afya wanasemaje ?, nini ushauri wao?
 
Umeona ile adamu na hawa

Wewe unaweza kuandika kwa kutumia hiyo nembo bila kupata misuko suko?

Maana iyo nembo haitumiki kiholela holela, jaribu kuheshimu huyo ni mkuu wa nchi labda usiwe mtanzania lakini kama ni mtanzania jaribu kuheshimu mamlaka.

Kula bata ndio mada iliyopo hapo juu?
marais wa nchi nyingine ushawasikia wanavyo lead from the front kwenye hili janga?

sisi huku twasubiri bora lijiendee tu!
 
Makanisa, Miskiti yote ingefungwa. Ningepiga marufuku abilia kuingia na kutoka Dar, Mipaka yote ingefungwa isipokuwa wanaoleta chakula, dawa na bidhaa muhimu, Kumbi zote za starehe zingefungwa kila mlevi anunue pombe dukani akanywe kwake.

Mishahara yote ya umma ambayo ni kuanzia milion 3 ingekatwa 50% ili kununua chakula kwa watu masikini.
Mwanza tumetangaziwa kwanzia leo sehemu kama Mwanza Hotel,Goden,Bunda Sriga,Malaika Beach na sehemu zote za starehe kufungwa ili kuepusha mikusanyiko isiyo ya lazima
 
Mbona kama unazunguka mbuyu?,sasa wewe unataka yukae ndani au.Kila nchi ina kiongozi wake na staili za uongozi zinatofautiana.
 
Halafu Kama Hamna lockdown plus mipaka kutofungwa
Mashule yafunguliwe pamoja na vyuo
Hakuna umuhimu wa watoto kuendelea kukaa nyumbani
 
Sisi wamalawi Kaka ni special case na exceptional dunia nzima.
Uzao wa Abraham...ndugu wa damu na Bwana Yesu Kristu...
vitukuu vya mtume yakhe
 
marais wa nchi nyingine ushawasikia wanavyo lead from the front kwenye hili janga?

sisi huku twasubiri bora lijiendee tu!
Walivyofanya Corona imeisha kwao?

Kila mtu ana mfumo wa ku deal na matatizo yake, hivi unataka kusema wewe na rais nani mwenye ACCESS mzuri wa kupata habari kuhusiana ukubwa au udogo wa hili tatizo?
 
Chibudee,
nilikua nawaza kweli mkisema tusitoke nje nitaishije na familia yangu maana mpaka nitoke nikatafute ndio mkono uende kinywani!

Asante sana Rais wangu wa kufa acha wafe wa kubaki wabaki wabaki maana hakuna wa kupambana na kifo kama ulipangiwa kufa na #covid19 mwaka 2020 utakufa tu ila kama hukuandikiwa kufa mwaka huu hutakufa.

cha msingi ni kuchukua tahadhali tu huku ukiacha maovu na kua karibu na Mwenyezi Mungu zaidi.
 
Back
Top Bottom