Chato: Serikali kujenga Uwanja wa kisasa wa Michezo

Chato: Serikali kujenga Uwanja wa kisasa wa Michezo

Serikali kujenga uwanja mkubwa wa mpira Chato

C&P

[https://pressmuusport]

Serikali imetangaza kujenga uwanja mkubwa wa mpira wilayani Chato, mkoani Geita ili kukuza sekta ya michezo nchini na kuvutia watalii na wawekezaji. Uwanja huo unatarajiwa kuwa wa pili kwa ukubwa baada ya wa Benjamin Mkapa ulipo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati Medard Kalemani amesema hayo wakati akihutubia sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya taifa ya Burigi-Chato na kueleza kwamba uwanja huo utaitwa Chato Stadium na ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

"Hivi karibuni tunajenga Uwanja wa mipra Chato Stadium ambao utatumika sana katika kuhamasisha Wawekezaji na hasa Watalii wanaotoka nje ya nchi yetu" amesema Waziri Medard Kalemani.
hehee chato futuboli kilabu
 
na kwa maelekezo lazima iwe premier!!!! ili kuwavutia watalii!!
 
Ingewezekana na SGR ingepita chattou ingekuwa poa sana, watalii wangekuwa na options kadhaa za kwenda kuangalia wanyama na mpira.. Wakitaka wanakuja na dege toka moja kwa moja ulaya, au wanashuka dar, kisha wanapanda treni ya umeme mpaka chattou.. Tutaingiza fedha nyingi za kigeni.. Korosho tupa kuleee..
 
tanzania , tanzania !!!!!!!!!!! nakupenda kwa moyo wote!!!
 
Watu hamna jema, hampendi maendeleo. Chato inakwenda kuwa kitovu cha utalii,sasa huo uwanja utavutia wawekezaji kama ambavyo uwanja wa taifa hapo temeke umekuwa ukivutia wawekezaji wengi tuu kuja Dar es Salaam. Na si uwanja tuu, hata ile hospitali ya Kitalii ya kikanda pia itajengwa Chato. These are strategic projects! Tuelewane.
 
Geita wamshukuru sana viki ckamata, kwa kukata kiuno vizuri adi mkwere akaamua kuupa hadhi ya mkoa na makao makuu ya mkoa kuwa Geita, angechelewa kidogo tuu chato ndiyo ingekuwa mkoa
acha upumbavu wako wewe wakati anakata hivyo viuno likuwepo kumsaidia au mlikata wote ,kwahiyo maeneo mengine yote yaliyopewa hadhi ya mkoa pia walikata viuno au huko ulikata wewe shenzi kabisa
 
Ule wa Dodoma uhamishiwe Chato.

Itapendeza zaidi. Wengine tunaona aibu kula rushwa ya Mfalme wa Morocco kuwasaliti ndugu zetu wa Sahara Magharibi.

Hii aibu iende kwake mwasisi wake.
 
Bado sioni kipaumbele cha kujenga huo uwanja. Ni kukurupuka tu na kufanya mambo ambayo hayana kipaumbele. Yule waziri kalemani kadai uwanja huo utavutia wawekezaji chato. Wawekezaji na kiwanja cha mpira chato wapi na wapi!? Kwenye mikoa ambayo kuna viwanja vya mipira wawekezaji wangapi wamevutiwa na viwanja hivyo!?

Ni sera za kukurupuka tu na za hovyo mara tumefanya hili mara lile badala ya kuwa na vipaumbele vyenye tija kwa Taifa. Ndiyo sababu baada ya miaka 59 ya uhuru bado kuna shule chungu nzima ziko katika hali ya kutisha na kusababisha elimu yetu kuendelea kuanguka ukilinganisha na nchi nyingi jirani.

Upo sahihi lakini kila sekta ina umuhimu wake, wapo ambao hawaamini kwenye elimu maisha yao yanategemea sports zaidi.
 
Bado sioni kipaumbele cha kujenga huo uwanja. Ni kukurupuka tu na kufanya mambo ambayo hayana kipaumbele. Yule waziri kalemani kadai uwanja huo utavutia wawekezaji chato. Wawekezaji na kiwanja cha mpira chato wapi na wapi!? Kwenye mikoa ambayo kuna viwanja vya mipira wawekezaji wangapi wamevutiwa na viwanja hivyo!?

Ni sera za kukurupuka tu na za hovyo mara tumefanya hili mara lile badala ya kuwa na vipaumbele vyenye tija kwa Taifa. Ndiyo sababu baada ya miaka 59 ya uhuru bado kuna shule chungu nzima ziko katika hali ya kutisha na kusababisha elimu yetu kuendelea kuanguka ukilinganisha na nchi nyingi jirani.
Nadhani nia zaidi ni kutangaza hifadhi ya burigi. Wanataka ijenga chato
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hebu tutulie jamani Chato ijengwe ...Maendeleo hayana chama ! haya hayana budi kutokea ili neno litumie! Kipaumbele cha Chato sasa ni Uwanja wa Soka ...kama unabisha hebu tupia hapa unayo ona yana kasoro huko Chato na unaona ndio yangetangulia!
 
Angesema kinajengwa chuo hapo ningeunga mkono ila naona uwaziri hauhitaji elimu kubwa maana hata Makonda anaweza kuwa waziri kutokana ni kutoa tamko bila kuwaza mbeleni itakuaje
 
Back
Top Bottom