Chato: Serikali kujenga Uwanja wa kisasa wa Michezo

Chato: Serikali kujenga Uwanja wa kisasa wa Michezo

Muda unavyozidi kwenda ndio tunapata picha vizuri kuwa TL alikuwa na yupo sahihi
 
Hivi uwanja wa mpira unahamasishaje watalii?

Yaani watalii waache huko kwao kwenda kushangaa Wembley Stadium waje washangae Chato Stadium?

Haya bana.
Yaani mtu akiwa anaweweseka utamjua tu kwa kauli zake. KUzindua mbuga haitoshi, ila kujenga Chato Stadium ambayo ITAVUTIA WATALII. kila mmoja anataka kumzidi mwenzake kwa UJUHA
 
Makao Makuu ya nchi hakuna uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu lakini kipaumbele ni chato!!! 😳😳😳😳

Ninachojiuliza tayar tulikuwa na mpango wa kujenga uwanja mkubwa pale Dodoma na hadi ikulu raman ilifika na kutangaziwa kuwa utakuwa mkubwa kuliko wa Mkapa je umeshia wapi au tumebadili gia angani?
 
CHATO STADIUM KUJENGWA HIVI KARIBUNI‬

‪Waziri Medard Kalemani amesema Serikali ipo mbioni kujenga Uwanja wa mpira wa Chato Stadium ambao amedai utatumika sana katika kuhamasisha Wawekezaji na hasa Watalii wanaotoka nje ya Tanzania
Hutaki ?
 
Waziri Medard Kalemani amesema Serikali ipo mbioni kujenga uwanja wa mpira hivi karibuni Chato.

"Hivi karibuni tutajenga uwanja wa mpira wa miguu Chato Stadium ambao utatumika sana kuhamasisha wawekezaji na hasa watalii wanaotoka nje ya nchi yetu".View attachment 1149718
Mpaka kufikia 2025 tutayaona na kuyasikia mengi sana kuhusu Chato
 
Kwa mpira upi uliokuwepo chato? Ubadhirifu mwingine wa mabilioni ya pesa za walipa kodi.
Mkuu..sio wachezaji wote wa Simba na yanga wamezaliwa daslam
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Makao Makuu ya nchi hakuna uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu lakini kipaumbele ni chato!!! 😳😳😳😳
Plan ya kujenga uwanja Dom ipo tayari
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Waziri Medard Kalemani amesema Serikali ipo mbioni kujenga uwanja wa mpira hivi karibuni Chato.

"Hivi karibuni tutajenga uwanja wa mpira wa miguu Chato Stadium ambao utatumika sana kuhamasisha wawekezaji na hasa watalii wanaotoka nje ya nchi yetu".View attachment 1149718
Maendeleo yumbani kwanza
 
Back
Top Bottom