Chato: Serikali kujenga Uwanja wa kisasa wa Michezo

Chato: Serikali kujenga Uwanja wa kisasa wa Michezo

Hivi uwanja wa mpira unahamasishaje watalii?

Yaani watalii waache huko kwao kwenda kushangaa Wembley Stadium waje washangae Chato Stadium?

Haya bana.
labda huu utakuwa wa makuti, ni kivutio.
 
Ahamishe na mlima Kilimanjaro na Meru pia na mount Usambara........................ na asisahau ana mwaka mmoja tena tuu huenda vyote hivyo vikawa historia.............
we mis mbona kama umepanic?relax mom
 
Kwa waziri mkuu mbona tayari....!

Kwani ile fainali ya shirikisho Lipuli vs Azam ilichezwa wapi?!
Daah nilionaga tu unajengwa mkuu,sikua najua hata kama ulishakamilika.

Mama Samia yeye kwao sijui atawajengea nini?
 
Pole sana ile fainali ilichezwa lindi mjini sio kule kwa waziri mkuu. Kule kwa waziri mkuu kumejengwa uwanja mkubwa ule wa lindi mjini cha mtoto.
Lindi kucheleeeeee
 
Hahaahahah
CHATO STADIUM KUJENGWA HIVI KARIBUNI‬

‪Waziri Medard Kalemani amesema Serikali ipo mbioni kujenga Uwanja wa mpira wa Chato Stadium ambao amedai utatumika sana katika kuhamasisha Wawekezaji na hasa Watalii wanaotoka nje ya Tanzania
 
Serikali kujenga uwanja mkubwa wa mpira Chato

17 minutes ago

[https://pressmuusport]

Serikali imetangaza kujenga uwanja mkubwa wa mpira wilayani Chato, mkoani Geita ili kukuza sekta ya michezo nchini na kuvutia watalii na wawekezaji. Uwanja huo unatarajiwa kuwa wa pili kwa ukubwa baada ya wa Benjamin Mkapa ulipo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati Medard Kalemani amesema hayo wakati akihutubia sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya taifa ya Burigi-Chato na kueleza kwamba uwanja huo utaitwa Chato Stadium na ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

"Hivi karibuni tunajenga Uwanja wa mipra Chato Stadium ambao utatumika sana katika kuhamasisha Wawekezaji na hasa Watalii wanaotoka nje ya nchi yetu" amesema Waziri Medard Kalemani.
 
All this time nimekua nikidhani Chato ni mkoa kumbe ni wilaya ndani ya njoa wa Geita. Iko kwenye headlines kuliko mkoa unaoibeba
 
Humu mapovu mengi mlitaka ajenge wapi eeeh ajenge wapi? Kwani hamjui tunajenga kwa hela zetu wenyewe ili watanzania maskini nao wafurahie matunda ya nchi yao. Mnapiga kelele tu . Acheni tuinyooshe nchi kwanza mmetumwa na mabeberu nyie. MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU. Nawaomba mnioombee NIACHE BANGI.
 
Hongera kwa ujenzi wa uwanja wa mpira Chato, lakini viongozi wa serikali wajenge magereza mazuri na wayaboreshe haya yaliyokuwepo kwani viongozi wengi wa Afrika humalizia umri wao magerezani.
 
Serikali kujenga uwanja mkubwa wa mpira Chato

C&P

[https://pressmuusport]

Serikali imetangaza kujenga uwanja mkubwa wa mpira wilayani Chato, mkoani Geita ili kukuza sekta ya michezo nchini na kuvutia watalii na wawekezaji. Uwanja huo unatarajiwa kuwa wa pili kwa ukubwa baada ya wa Benjamin Mkapa ulipo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati Medard Kalemani amesema hayo wakati akihutubia sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya taifa ya Burigi-Chato na kueleza kwamba uwanja huo utaitwa Chato Stadium na ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

"Hivi karibuni tunajenga Uwanja wa mipra Chato Stadium ambao utatumika sana katika kuhamasisha Wawekezaji na hasa Watalii wanaotoka nje ya nchi yetu" amesema Waziri Medard Kalemani.
 
CHATO STADIUM KUJENGWA HIVI KARIBUNI‬

‪Waziri Medard Kalemani amesema Serikali ipo mbioni kujenga Uwanja wa mpira wa Chato Stadium ambao amedai utatumika sana katika kuhamasisha Wawekezaji na hasa Watalii wanaotoka nje ya Tanzania
😂😂😂 hivi kuna mchezaji gani maarufu Tz anayokea Chato
 
Back
Top Bottom