Chato: Serikali kujenga Uwanja wa kisasa wa Michezo

Chato: Serikali kujenga Uwanja wa kisasa wa Michezo

Hivi kuna miaka kulikuwa na miguno kuhusu barabara kupindishwa kutoka Biharamulo na kuelekezwa Chato....mimi nilikuwa bado mdogo sikumbuki sawia ...hivi kulitokea nini vile! Kama tuliguna tu tukaacha yapite haya ya leo tunashangaa nini!
 
Nia zaidi ni kuhakikisha hotel ya nduli na dikteta wa Ikulu kupata wateja vinginevyo itakuwa empty throughout the year. Nani aende chato hiyo hifadhi ya chato katika vivutio vya watalii vilivyopo Tanzania katika dunia hakuna anayeijua.



Nadhani nia zaidi ni kutangaza hifadhi ya burigi. Wanataka ijenga chato
 
Serikali kujenga uwanja mkubwa wa mpira Chato

17 minutes ago

[https://pressmuusport]


Serikali imetangaza kujenga uwanja mkubwa wa mpira wilayani Chato, mkoani Geita ili kukuza sekta ya michezo nchini na kuvutia watalii na wawekezaji. Uwanja huo unatarajiwa kuwa wa pili kwa ukubwa baada ya wa Benjamin Mkapa ulipo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati Medard Kalemani amesema hayo wakati akihutubia sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya taifa ya Burigi-Chato na kueleza kwamba uwanja huo utaitwa Chato Stadium na ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

"Hivi karibuni tunajenga Uwanja wa mipra Chato Stadium ambao utatumika sana katika kuhamasisha Wawekezaji na hasa Watalii wanaotoka nje ya nchi yetu" amesema Waziri Medard Kalemani.
Naona Gbadolite ya bongo inaendelea kujengwa kwa nguvu zote
 
Sioni kujenga uwanja kule chato kama ni kipaumbele kwa Watanzania. Vipi kuhusu shule ambazo hazina madarasa, vyoo na madawati? Kwanini hayo mabilioni yasielekezwe huko!?
Mbona hilo tatizo limeshaisha. Wakuu wetu wa mikoa wanalishughulikia ipasavyo
 
Nia zaidi ni kuhakikisha hotel ya nduli na dikteta wa Ikulu kupata wateja vinginevyo itakuwa empty throughout the year. Nani aende chato hiyo hifadhi ya chato katika vivutio vya watalii vilivyopo Tanzania katika dunia hakuna anayeijua.


Kwasasa hakuna anayeijua kwasababu ni mpya, itatangazwa na itajulikana.
 
Natamani ahamishe makao makuu Ya CCM yawe Chato kwa kweli
 
Magufuli ukimaliza kuzindua mbuga, Nenda ukazindue na bahari kule Ununio, Kuna bonge la bahari halijazinduliwa. Halafu usisahau kuuzindua rasmi mlima Kilimanjaro.
 
Kiukweli mm napenda sana Tanzania kuwa na viwanja vingi vya michezo ,maana ili nchi iendelee lazima kila secta iwe juu. Angalia RSA wameendelea kila kitu ,siyo 2025 tuwe uchumi wa kati alafu hatuna vuwanja bora Africa. Ila nongwa yangu sasa ni kwann Chato? Chato no mji mdogo ambao hata tukiomba kuandaa Afcon hakuna hotel za kutosha kulaza wachezaji hivyo kama mm ningekuwa muamuzi uwanja wa kisasa unatakiwa kujengwa Arusha,Mwanza , Mbeya ,Morogoro , Dom Tanga,Iringa ,Moshi hayo ndo maeneo ambayo yanheleta maana ya uwekezaji lakini siyo Chato
 
Back
Top Bottom