Chato: Serikali kujenga Uwanja wa kisasa wa Michezo

Chato: Serikali kujenga Uwanja wa kisasa wa Michezo

Uwekezaji wa Mpira unaanza na miundombinu. Na pia tukubaliane kuwa sio kila uwanja uweDar tuu, sahizi kanda ya ziwa halafu miaka inayo Kusini na mashariki pia viwanja vitajengwa. Mtafurahi wenyewe ngojeni!
 
Chato haihitaji uwanja mkubwa sana wa mpira, wajenge uwanja mdogo wa kutosha watu 10,000 - 15,000 utatoshaa, wananchi wa chato ni masikini, msisitizo ungewekwa kwa kuanzisha viwanda, masoko, kujenga vyuo n.k ili wana chato wapate ajira na kujenga maisha yao kiuchumi, chato pia inatakiwa ipangiliwe, huwezi kutaka kuufanya mji wa kitalii wananchi hawana makazi mazuri, huku kuna bonge la uwanja state of the art, wataingia punda?

Vuta watu wakaishi na kuijenga chato, fungua fursa watu wakimbile huko mji utajijenga wenyewe
 
Hatutaacha kuona maajabu
D-nBGoCWkAAbtUN.jpeg
 
Mama Salman, nawe kajenge international saloon huko Zanzibar.
 
Kule Butiama baada ya lile kaburi lake yule mzee alijenga nini tena
 
Hiyo kauli sio ya waziri huyo. Mhusika yupo. Vipi mbona kimyaaa?

Halafu
Upo kirumba
Kaitaba

Sasa chato?

Au ni ule wa dodoma umehama?

Hapo sio sawa kabisaaaaa. Vipo vitu vya chato sio uwanja wa kisasa wa michezo.

Hoteli za kulala watu hao ziko wapi?

Huduma za chakula, nk hapo chato kweli zipo?
 
Uwekezaji wa Mpira unaanza na miundombinu. Na pia tukubaliane kuwa sio kila uwanja uweDar tuu, sahizi kanda ya ziwa halafu miaka inayo Kusini na mashariki pia viwanja vitajengwa. Mtafurahi wenyewe ngojeni!
 
sasa hivi mambo yanaenda kihuni kihuni, kama wilaya yako haina waziri, basi kodi zenu mnawatolea wengine
 
Chatoal ka dar....mtaipenda tu mabegesa
 
Naihurumia Geita mjini
CHATO STADIUM KUJENGWA HIVI KARIBUNI‬

‪Waziri Medard Kalemani amesema Serikali ipo mbioni kujenga Uwanja wa mpira wa Chato Stadium ambao amedai utatumika sana katika kuhamasisha Wawekezaji na hasa Watalii wanaotoka nje ya Tanzania

---------
Serikali imetangaza kujenga uwanja mkubwa wa mpira wilayani Chato, mkoani Geita ili kukuza sekta ya michezo nchini na kuvutia watalii na wawekezaji. Uwanja huo unatarajiwa kuwa wa pili kwa ukubwa baada ya wa Benjamin Mkapa ulipo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati Medard Kalemani amesema hayo wakati akihutubia sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya taifa ya Burigi-Chato na kueleza kwamba uwanja huo utaitwa Chato Stadium na ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

"Hivi karibuni tunajenga Uwanja wa mipra Chato Stadium ambao utatumika sana katika kuhamasisha Wawekezaji na hasa Watalii wanaotoka nje ya nchi yetu" amesema Waziri Medard Kalemani.
 
Back
Top Bottom