hapo sawa-nimekuelewa; ila wanatakiwa pia kupeleka malalamiko yao kwenye ofisi za tume kitaifa iwapo hao wa vijijini, tarafani na wailayanoi wanawazingua kabbla ya kuvunja sheria.
..sheria zetu za uchaguzi zina matatizo mengi sana. lakini kwa bahati mbaya wanaoathirika ni wapinzani peke yao. ccm wao hawaathiriwa na sheria mbaya za uchaguzi.
..ushauri kwamba wapinzani wakinyimwa haki ktk ngazi ya chini wanatakiwa kulalamika ktk ngazi ya taifa ni mzuri.
..tatizo ni kwamba maamuzi yakitoka ktk ngazi ya taifa yanarudi kwa msimamizi ktk ngazi ya wilaya au jimbo kuyatekeleza. sasa maagizo ya ngazi ya juu yakirudi ngazi ya wilaya, au jimbo, figisu zinaanza upya tena kuwakwamisha na kuwahujumu wagombea wa upinzani.
..kwa mfano, kuna wagombea udiwani wa Cdm mpaka wiki iliyopita walikuwa wameshindwa kuanza kampeni. Na tatizo lilikuwa ni msimamizi ktk ngazi ya jimbo kuchelewa kutekeleza maamuzi yaliyotoka ktk ngazi ya tume taifa. Tume inadai imepeleka barua kwa msimamizi ktk ngazi ya wilaya kwamba wagombea wameshinda rufaa, lakini msimamizi anadai hajapokea maagizo hayo.
..Pamoja na kuwepo kwa matangazo ktk magazeti kuonyesha kwamba tume ngazi ya taifa imeridhia rufaaa za wagombea, bado wasimamizi walikataa kuwapa ruhusa wagombea kuanza kampeni.
..Tunakwenda kupiga kura tarehe 28, lakini kuna wagombea wa vyama vya upinzani wameanza kampeni zao wiki jana, au wiki hii, kutokana na figisu za wasimamizi wa uchaguzi. Na hapo tunazungumzia figisu za wagombea, bado hatujui nini kitatokea kwa mawakala wa vyama vya upinzani.
..Kwa kweli kama taifa tunatakiwa ku-clean up our election laws and processes lakini sijui ni nani ataifanya kazi hiyo.