Uchaguzi 2020 Chato: Yaliyojiri Mapokezi ya mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 Chato: Yaliyojiri Mapokezi ya mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Tundu Lissu

Kama una akili sawasawa. Ungeelewa kwamba hajawahi kuponda uwanja kwa maana ya ubora anachosema . Yeye ni mchakato wake kuanzia tenda na gharama zake .pia unazungumzia uhalali wa kujenga huko chato kijijini kwa MAGUFULI. Hizi degree za kudesa zinawaacha uchi kichwani nyie
Degree ipi uliyonisomesha?
 
Wote tuchukue ushahidi wa ninani anafanya uovu,ili kujenga taifa lenye kuheshimu ,Uhuru,haki na Sheria.
Tayari ICC kuna majarada ya IGP na maRPC, OCD wote wanaoshiriki vitendo vya hovyo hovyo vya kuwapiga mabomu risasi wapinzani, mara baada ya uchaguzi mkuu wote watafikishwa ICC The Hague mara moja.uchaguzi huu ni wa tofauti na watu wakivyozoea kuona Polisiccm wakionea wananchi na kuachwa hivi
 
Mradi mkubwa wa kutafuna pesa CCM kwa sasa ni mbinu za kuihujumu kuidhoofisha chadema kila anayekwenda na mbinu za kuteketeza chadema anapewa pesa na cyprian Musiba chini ya uratibu wa polepole .
Matumizi mabaya kabisa ya fedha zetu
 
Kauli ya kishujaa ya Lissu muda mchache uliopita kuhusu kwenda Chato.


ICC The Hague tayari wamingiza kwenye list Polisiccm wote walioshiriki hivyo vitendo vya hovyo vya kishamba na kishetani
 
Kuna vipaumbele vya nchi na vya mtu binafsi sio vyote lazima viwe vipaumbele vya Chato vingine ni vya kitaifa

Mfano Serengeti kuna uwanja wa ndege lakini si kipau mbele cha wana Serengeti ni cha kitaifa

Mfano kipaumbele cha wana Chato ni Lissu? au CHADEMA?
Very small reasoning capacity.
 
Matumizi mabaya kabisa ya fedha zetu
Pesa za chadema hutumika kujihami dhidi ya hujuma lukuki tokea CCM pia hutumika kugharamia kesi kesi za kubambikiwa na CCM kila kona ya Tanzania na zingine hutumika kuimarisha chama ndiyo maana chadema ipo licha ya CCM kutumia gharama kubwa kuiangamiza
 
i) Kwanini haustahili kuwa Chato?

ii) Ulitakiwa kuwa wapi?
Chato international airport
Yaani tutegeeme mashirika makubwa ya ndege kutua pale chato kuleta watu kutoka sehemu mbalimbali duniani

Mpaka leo Ni safari ngapi za ndege zimeshafanyika kupitia huo uwanja

Ajira ngapi zimetengenezwa kupitia uwanja

Wana chato wanafaidika vipi na uwepo wa huo uwanja
Wana uhitaji kiasi gani wa usafiri wa ndege Kama baadhi ya maeneo ambayo Yana changamoto ya barabara ukiwapelekea lami wakushukuru, chato wanashukuru kiasi gani baada ya kuwajengea uwanja na kutatua changamoto yao ya usafiri wa ndege iliyowasumbua kwa muda mrefu?

Sijui chato imependelewa kiasi gani katika awamu hii
Lakini sio kweli kwamba matatizo yote ya wanachato yametatuliwa
Elimu kuanzia waalimu majengo mpaka vifaa,
Mahospitali sio kujenga majengo tu kuanzia madaktari vifaa vya huduma na huduma zenyewe
Maji je Kila Kaya chato inapata maji Safi na salama kutoka idara ya maji? Au angalau asilimia 50 au zaidi?
Kama Ni wafugaji mifugo Ina maeneo mazuri ya malisho na hakuna migogoro?
Vipi kuhusu mabwana mifugo na Kama Ni wakulima wanalima kilimo Cha aina gani uhakika wa maji kwaajili ya mashamba na mabwana shamba ili wazingatie kilimo Cha kisasa
Ni billion ngapi zimelala pale bila faida yoyote?
Kama wapinzani wakijianga pale chato wanaenda kuchukua kata zote na Jimbo lenyewe
 
Mgombea wa Urais anayetarajiwa kupata ushindi mkubwa Tundu Lissu leo ataitetemesha Chato na viunga vyake katika kampeni zake zilizoivuta Dunia.

Taarifa kutoka ndani ya Team yake ya Kampeni kabla ya kuhutubia mkutano wa Hadhara atautembelea Uwanja wa ndege wa Chato uliozua gumzo nchini kote kutokana na Ujenzi wake.

Tundu Lissu amepata uungwaji mkono mkubwa kutoka Makundi yote ya Jamii hususan Wafanyakazi ambao wanalaani kupitishwa kwa sheria Haramu ya kupora Mafao yao. CCM na serikali yake walipitisha sheria ya kuzuia Mafao ya Wafanyakazi hata Kama ameacha kazi akiwa na miaka 30 haruhusiwi kupewa haki yake ya mafao mpaka afikishe miaka 60.Sheria hii Haramu imelaaniwa na kila mfanyakazi na Tundu Lissu ameapa kuifutilia mbali Mara tu baada ya kuapishwa.

Ingawa Chato ni nyumbani kwa mgombea Urais wa CCM Lakini kwa muda mrefu CHADEMA imekuwa na uungwaji mkono mkubwa na inao wafuasi wa kutosha.Mmoja wa makamanda mashuhuri wanaotokea Chato ni mwanamama Husna Amri ambaye anajulikana nchi nzima kwa ujasiri wake.

Tunatarajia kuwaletea kila kitakachojiri katika mapokezi na Mkutano wa Kampeni hapa Chato.

-------------------------- --------------------
Yanayoendelea saa 4 Asubuhi

Mgombea wa Urais Tundu Lissu amekutana na wanachama nje ya Hoteli aliyofikia mjini Kahama kabla ya kuondoka kuelekea kwenye kampeni.

Lissu amesema Jana usiku mgombea Ubunge CDM Jimbo la Chato alivamiwa na kuharibiwa Mali zake na maharamia wanaifanyia hivyo ili kumtishia asiende Chato.

Lissu ameonya hatatishika na ataingia Chato na kufanya mkutano Mkubwa wa Kampeni.Lissu ameitaka Dunia kutega masikio kuelekea Chato leo jioni.

Kabla ya kuhutubia Chato jioni hii Lissu anatarajiwa kufanya kampeni maeneo ya Mbogwe na Bukombe

View attachment 1598334
Sema Bangi hukidhi matakwa ya Mtumiajiiii hahaha ujingaaa kabisa huu
 
Hii hesabu feki. Tanzania ni kubwa sana, hakukuwa na sababu ya Lissu kurudi kanda ya ziwa mara ya tatu. Anapoteza muda wake na resources, wasukuma hawezi kuacha kumpa kura mtu wao.

Kwani tz kuna ukabila?
 
Hiyo ndio Robert Amsterdam!
Ni mdogo wake Polepole.
JamiiForums409068559_680x455.jpg
 
Pesa za chadema hutumika kujihami dhidi ya hujuma lukuki tokea CCM pia hutumika kugharamia kesi kesi za kubambikiwa na CCM kila kona ya Tanzania na zingine hutumika kuimarisha chama ndiyo maana chadema ipo licha ya CCM kutumia gharama kubwa kuiangamiza
Chadema ndio kimbilio la Wananchi walionyimwa haki na kuonewa na Serikali ya CCM wanaCCM wenyewe waliowengi tuko nao humu Chadema

Mwaka huu nasikia wamamuandaa Jecha mwingine huku Bara
 
Hairusiwi kimataifa toka mashamba I ya kigaidi Marekani viwanja vyote vya ndege duniani unaenda ukiwa unasafiri au unadindikiza msafiri Huwezi kwenda kutalii sio mbuga ile ndio maana zamani uwanja wa Ndege wa Dar es salaam tulikuwa tukienda kutalii unapanda juu hata harusi tukienda nazo lakini vyote vilipigwa marufuku .Hivyo Huwezi kwenda eti nakuja kutalii sisafiri Wala Nini nakuja tu kutalii
Uza ubongo huo maana unaumiliki kwa hasara. Inaonekana unaishi ili ule na sio kinyume chake.
 
Pesa za chadema hutumika kujihami dhidi ya hujuma lukuki tokea CCM pia hutumika kugharamia kesi kesi za kubambikiwa na CCM kila kona ya Tanzania na zingine hutumika kuimarisha chama ndiyo maana chadema ipo licha ya CCM kutumia gharama kubwa kuiangamiza
Halafu wenyewe wanasingizia matumizi ya ruzuku yao ni mabaya. Ila Kila Mara najaribu kuwakumbusha, kuwa uhai wa chama wanachoona ni adui wao nii Mara Sana, kwasababu wanatumia vizuri rasilimali chache waliyonayo kujenga chama, hata wanaona no chama tishio kwao na wanatumia nguvu zote kujaribu kukwamisha harakati zao. Kama uongo jitokezeni mjibu kwa hoja.
 
Back
Top Bottom