Uchaguzi 2020 Chato: Yaliyojiri Mapokezi ya mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 Chato: Yaliyojiri Mapokezi ya mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Tundu Lissu

Kuna watu sijawahi ona, uwanja wa Chato uwanja wa Chato, hivi Chato ni wananchi wa wapi? Wao hawana haki ya kuwa na uwanja? Mbona mnakuwa wapumbavu kiasi hiki?

Mnatukana kila siku Chato utafikiri wao hawatakiwi kuwa na uwanja. Kwa taarifa yenu wananchi wa Chato si wajinga, muulizeni mgombea wenu alichokipata Buselesele na Katoro hadi akasitisha kwenda Chato, haya yote ni siasa mbovu isiyo na staha, hata kama unachallenge tumia lugha rafiki, don't be so biased to that extent, watu wa Chato amewatukana sana, Buselesele na Katoro yalikuwa maeneo ya upinzani lakini kutokana na dharau za Lissu matokeo yake CHADEMA leo inazomewa, Lissu asingezomewa Buselesele kwa namna ile, Awe na akiba ya maneno kwani anaowatukana wanasikia .

Inashangaza sana unatukana halafu bado eti unaenda kuwaomba kura,,,,, unatukana barabara kujengwa huku unazitumia, unatukana ndege huku unazipanda huo ni U CHICHIDODO.

Hopeless kabisa , let's stay tuned leo.
Alipofika buseresere na katoro akaghairi kwenda chato kwasababu alizomewa??? Hv mtu anaetokea muleba atapita buseresere na katoro kabla ya chato et??? Be a gentleman aseeee wadanganye ambao hawajawahi kufika huko!!!
 
Kuna tetesi kuwa Polisiccm wanawatishia watu wasiende kwenye mkutano huo maana Duniani kote wanautizama kama live mechi ya Liverpool vs man u au Barcelona vs Real Madrid
Nyie nendeni, msianze kuogopa kivuli chenu.
 
Naomba Lissu asisahau kuwaambia wanaChato kuhusu CCTV za nyumbani kwa Dr Kalemani pale Dodoma zilivyoondolewa.
 
Wewe ndio mpumbavu, watu wa Chato wanataka maji safi, zahanati zenye vifaa tiba, madawati na vitabu mashuleni lakini sio uwanja wa mabilioni kwa ajili ya kumleta Museveni na Odinga Mara moja moja kwa mwaka na sasa hawatakuja tena
Ya jikoni hatuwezi kuyajua. Mbona hawakupinga au kuukataa toka unaanza kujengwa?! Au waliamka asubuhi wakaukuta pale?!
 
Ndugu yangu achana na historia, safari hii mambo ya kukimbia na mabox ya kura au kura za kuchonga hayapo tena.
Safari hii kuna watu kama sio kufungwa muda mrefu basi watanyongwa!
He! We unamchukia muuaji kisha unakata na nyie muwe wauaji?
 
Mgombea wa Urais anayetarajiwa kupata ushindi mkubwa Tundu Lissu leo ataitetemesha Chato na viunga vyake katika kampeni zake zilizoivuta Dunia.

Taarifa kutoka ndani ya Team yake ya Kampeni kabla ya kuhutubia mkutano wa Hadhara atautembelea Uwanja wa ndege wa Chato uliozua gumzo nchini kote kutokana na Ujenzi wake.

Tundu Lissu amepata uungwaji mkono mkubwa kutoka Makundi yote ya Jamii hususan Wafanyakazi ambao wanalaani kupitishwa kwa sheria Haramu ya kupora Mafao yao. CCM na serikali yake walipitisha sheria ya kuzuia Mafao ya Wafanyakazi hata Kama ameacha kazi akiwa na miaka 30 haruhusiwi kupewa haki yake ya mafao mpaka afikishe miaka 60.Sheria hii Haramu imelaaniwa na kila mfanyakazi na Tundu Lissu ameapa kuifutilia mbali Mara tu baada ya kuapishwa.

Ingawa Chato ni nyumbani kwa mgombea Urais wa CCM Lakini kwa muda mrefu CHADEMA imekuwa na uungwaji mkono mkubwa na inao wafuasi wa kutosha.Mmoja wa makamanda mashuhuri wanaotokea Chato ni mwanamama Husna Amri ambaye anajulikana nchi nzima kwa ujasiri wake.

Tunatarajia kuwaletea kila kitakachojiri katika mapokezi na Mkutano wa Kampeni hapa Chato.

-------------------------- --------------------
Yanayoendelea saa 4 Asubuhi



Mgombea wa Urais Tundu Lissu amekutana na wanachama nje ya Hoteli aliyofikia mjini Kahama kabla ya kuondoka kuelekea kwenye kampeni.

Lissu amesema Jana usiku mgombea Ubunge CDM Jimbo la Chato alivamiwa na kuharibiwa Mali zake na maharamia wanaifanyia hivyo ili kumtishia asiende Chato.

Lissu ameonya hatatishika na ataingia Chato na kufanya mkutano Mkubwa wa Kampeni.Lissu ameitaka Dunia kutega masikio kuelekea Chato leo jioni.

Kabla ya kuhutubia Chato jioni hii Lissu anatarajiwa kufanya kampeni maeneo ya Mbogwe na Bukombe

View attachment 1598334



 
Back
Top Bottom