Reuben Challe
JF-Expert Member
- Dec 10, 2021
- 2,940
- 5,511
Ni kama mnataka kuforce kutabiri future hiviSielewi. Nifahamishe naongea nini?
Rise of USA imeshaonekana ila hiyo fall unayozungumzia iko kwenye vichwa vya watu tu sio uhalisia
*Kwenye masuala ya utafiti wa anga (space exploration) USA iko vizuri kuliko China, tunaona Marekani ina NASA na Space X, Mchina sijui ana nini
*Kwenye uzalishaji wa electronics hapa kidogo China anajitahidi ila bado anaachwa na Mmarekani,
*Mfano kwenye utengenezaji wa laptop tunaona makampuni mengi makubwa yanayofanya vizuri ni ya Marekani mfano Apple, DELL, Microsoft, HP nk. Kwa China kidogo Lenovo yuko vizuri ila bado anatumia OS za Mmarekani, Windows na Chromebook OS
*Kwenye simu Wachina wanajitahidi ila Mmarekani yuko juu zaidi. Apple zinaongoza kwa mauzo dunia nzima na bado Wachina wanaofanya vizuri wanatumia OS ya Mmarekani kwenye simu zao (Android). Moja ya sababu zinazofanya nipende simu za China ni kwamba zinatumia OS ya Mmarekani [emoji1]
*Kwenye SoC za simu na PC bado wanategemea makampuni ya Kimarekani kama Qualcomm, MediaTek, Intel na AMD.
*Kwenye utengenezaji wa Automobiles USA ipo kilometre milioni 6 mbele ya China
*Kwenye movie industry USA inaongoza dunia nzima. Teknolojia ambayo Mmarekani anaitumia kwenye movie zake inamshangaza hata Mchina mwenyewe
*Marekani ina jeshi bora la ardhi imara kushinda China
*Marekani anaicontrol dunia, ameweza kuangusha moja ya kampuni zilizokuwa moto kwenye utengenezaji wa simu kama Huawei kupitia vikwazo tu, Mchina hawezi kufanya hivyo kwa kampuni yoyote ya USA na akafanikiwa kuiangusha
*USA iko vyema kila idara kushinda China
Sijui hiyo fall of USA mmeiona wapi