T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Nchi ya wachumia tumbo haiwezi zuia maendeleo ya kisayansi sanasana itachelewa na itajiumiza yenyewe. We huoni hata Waarabu wenyewe wameanza diversification ya oil dependent economy. Saudi Arabia hiyo hapo 50 Cent anapiga show😂Naanza kuwaona waarabu wanatoka kwenye ramani aisee. Hali ni mbaya. Kama gari inakwenda 1000km per charge sio mchezo, kwenye website ya haya mabasi ya yutong wametoa basi za umeme, naona zina range ya 18 km itakuwa ni city buses kwa sababu zipo hadi hizi za mwendokasi.
Ni muda tu hapo na bus watatoa za 1000 km/charge.
Kuna mchezo serikali inafanya tuendelee kuhangaika na gari za mafuta, ile issue ya gari za Mahindra kutoka India, itakuwa ni issue ya kupambania biashara za wakubwa, kuna wababe wameshavuta gari za umeme hapa bongo.
Na kinachokwenda kutokea bidhaa kama hizi zikianza kuzalishwa China, ni wewe na bei yako, serikali inawaza sana.
Wanajifunika shuka kumekucha.
Waarabu smart kama UAE na Qatar hawataki ujinga wako na sovereign wealth funds wanawekeza sehemu tofauti.