China ataiua US kwa presha, katangaza Kirin 9006C(chip) ya 5nm tech

China ataiua US kwa presha, katangaza Kirin 9006C(chip) ya 5nm tech

Mkuu nchi kujitengenezea space station siyo kituo kidogo
Hizi low orbit satellites hata India anafanya.
Mkuu sijasema satelite, nimesema space station. Ukiiondoa china hakuna nchi yenye space station yake peke yake kwa sasa. Hiyo space station nyingne ni muunganiko wa Us, Russia na shirika la anga la Ulaya.
 
Umeona test ya Nio ya CEO wake jana. Gari lao la umeme la ET7 limeenda kilomita 1000 bila kuwa recharged na likabaki na kachaji kidogo. Yani unaweza toka Dar hadi Mwanza bila kuchaji na gari lenyewe sijui ilikuwa sedan, crossover au SUV. Sio truck
Naanza kuwaona waarabu wanatoka kwenye ramani aisee. Hali ni mbaya. Kama gari inakwenda 1000km per charge sio mchezo, kwenye website ya haya mabasi ya yutong wametoa basi za umeme, naona zina range ya 18 km itakuwa ni city buses kwa sababu zipo hadi hizi za mwendokasi.
Ni muda tu hapo na bus watatoa za 1000 km/charge.

Kuna mchezo serikali inafanya tuendelee kuhangaika na gari za mafuta, ile issue ya gari za Mahindra kutoka India, itakuwa ni issue ya kupambania biashara za wakubwa, kuna wababe wameshavuta gari za umeme hapa bongo.

Na kinachokwenda kutokea bidhaa kama hizi zikianza kuzalishwa China, ni wewe na bei yako, serikali inawaza sana.
Wanajifunika shuka kumekucha.
 
At least umeelewa NASA iko juu ya huyo Mchina unayemtetea

Hebu turudi kwa Space X, naomba utaje jina la hilo shirika la China unalosema limefanya hayo yote ili nijue unataka kumlinganisha Space X na nani specifically.

I mean jina kama unavyoitamka NASA au Space X, nitajie hiyo ya Kichina nataka niifuatilie
Private space company ya China nayo ifahamu kwa haraka ni i-space halafu fahamu kuwa uchumi wa China umetawaliwa na mashirika ya umma una tabia za kikomunisti sio ubepari hii pia inaweza chagiza utofauti
 
Mimi shirika la china nalozungumzia ni la serikali kama ilivyo Nasa linaitwa China national space agency CNSA
 
Ulimwengu wa sasa ukiwa mbabe lazima na kwenye masuala ya anga lazima uwe vizuri pia eeeh?? Ila mmarekani ni kama sehemu nyingi yupo, yani kila sekta. Uchumi, kijamii, historia, teknolojia kama hivo, michezo, elimu, kiusalama ndio namba moja nadhani.

Hivi mtu kama Elon zile projects najua lazima serikali iko nyuma yake yani ni national asset kwahyo hata ulinzi ni wa serikali inawezekana etii?? Mabilionea pia ni wengi mnoo wa marekani ila mchina nae siku hizi anatoa sana.

Mataifa ambayo yapo vizuri kudukua taarifa za mwenzie nae ndio mbabe wa dunia? Jinsi ulivyo na siri nyingi ndio ubabe wenyewe....

Kuna documentary moja ya kuhusu yule mapanki wa korea dogo jambazi. Inaelezea jinsi jamaa anapambana na vikwazo alivowekewa na jumuiya za kimataifa. Ana kitengo cha watu wa tehama ambao kazi yao kuu ni kutafuta fedha za kigeni kwa wizi kwenye mitandao. Asee jamaa wako vizuri, yani watoto tangia wadogo, wanawatenga wale wenye 'vichwa' then wanaanza kuwawekea mazingira ya kupata ujuzi na tafiti na vumbuzi mbalimbali mana wanauza mbaka silaha nje.

Hiko kitengo kinakusanya mamilioni ya dola kila mwaka kwa ajili ya taifa lao. Hata yule mnigeria maarufu wa insta aliekamatwa dubai nae ni accomplice wa hiko kikundi inasemekana hivo.

Ebu ile internet ya starlink ije bongo tuone ulimwengu ukoje. Mixa ma AI sahivi ni balaa tupuu yani yangu macho tu
 
Private space company ya China nayo ifahamu kwa haraka ni i-space halafu fahamu kuwa uchumi wa China umetawaliwa na mashirika ya umma una tabia za kikomunisti sio ubepari hii pia inaweza chagiza utofauti
Hata private companies kwenye space china zimeingia juzi juzi tu.
Kitu ambacho watu hamtaki kukiona ni hatua alizopiga kwa muda mfupi wakati kawakuta key players.
China karibia kila anachoanza mwisho anakuja kuwa ndiye kinara.
Aliamza uunzi wa meli, sasa karibu nusu ya meli zote zinazoundwa ni china.
Sasa imekuja hata kwenye EVs.
Wait kidogo utasikia hata ndege za abiroa baada ya miaka michache
 
Mimi shirika la china nalozungumzia ni la serikali kama ilivyo Nasa linaitwa China national space agency CNSA
Yaah nafahamu kuhusu CNSA na mafanikio yake ya anga habari zake nafuatilia ila bado hawaja fikia mafanikio ya ya Nasa ya anga kutokana na sababu mbalimbali.

Ila kwa sasa wapo moto na ninaona kwa miaka ijayo kama speed yao waliyo nayo sasa wakiongeza wenda watafika mbali.

Ila binafsi naikubali Nasa wapo vizuri
 
Lakini kwa maelezo hii Tu-144 ilitangula kuruja kabla ya concord.
Halafu kwa maelezo wanasema zilikuwa lazima zifanane kwa sababu hakukuwa na njia ya kudesign ndege yenye supersonic speed lazima katika design ungeishia kupata umbo hilo.
Pia zilikuwa na utofauti katika mabawa yalipowekwa, engine zilizotumika na mambo mengine.
Ndege kuanza kuruka haimaanishi ndio ilianza development. Mfano wakati Urusi inaanza project ya 5th generation fighter ambayo ikaizaa PAK FA, ambayo iliitoa Su-57 muda huo Marekani haikuwa imeanza project ya kuitoa F-35. Project ya Su-57 ilianza 1999 baadae ikawa cancelled kwa ukata na kuendelezwa tena. Project ya F-35 ilianza 2001. Ila sasa, F-35 first flight ikawa 2006 na ikaingia jeshini mwaka 2016 wakati PAK FA first flight ni 2010 na Su-57 imeingia 2020. Hapo zingefanana huwezi sema F-35 imeibia kwa Su-57.

Kwa hizo supersonic airlines hakukuwa na room ya mojawapo kuiiga nyingine sababu zilikuwa developed kwa wakati mmoja. Na wakati huo Anglo-French consortium haikuwa kwenye mashindano na Urusi kumbe Urusi ilikuwa kwenye mashindano. Ndio maana Warusi waliikurupua Tu-144.

Kwenye design ni kweli ndege zenye kazi sawa zinabidi zifanane kwenye umbo la nje na aerodynamics. Tofauti itakuwa kwenye technology na materials. Ukitazama 5th generation fighter projects za Marekani, Japan, South Korea, China, UK zote karibu zinafanana. Warusi ndio wabishi wakaleta dogfighter ya 5th sijui ni superpower mpuuzi gani atakuja kufanya dogfights kwenye 21st century.
 
Kwenye sakata la Marekani na Huawei bado Huawei ndio loser

Sanction za Mmarekani zimeiathiri sana Huawei, haijalishi Huawei ataendelea kutengeneza product bora au la.

Huwezi shindana na Mmarekani
Najua haujaijua Huawei vizuri, upande wa simu ndio sanctions ya Marekani imeumiza lakini Huawei is more than smartphones

Na upande wa smartphones amerudi sasa ni suala la muda kuona Huawei anarudi kivingine kwenye soko la dunia
 
Hata private companies kwenye space china zimeingia juzi juzi tu.
Kitu ambacho watu hamtaki kukiona ni hatua alizopiga kwa muda mfupi wakati kawakuta key players.
China karibia kila anachoanza mwisho anakuja kuwa ndiye kinara.
Aliamza uunzi wa meli, sasa karibu nusu ya meli zote zinazoundwa ni china.
Sasa imekuja hata kwenye EVs.
Wait kidogo utasikia hata ndege za abiroa baada ya miaka michache
Nawaheshimu wachina na jamii mfanano wake Korea na Japan kutokana na sababu zangu binafsi.

Wanafanya vyema katika hiyo sekta kama unavyosema ila safari yao bado ndefu kufikia utabe wa Nasa kwenye kutawala anga na mafanikio yake.

Wajipe muda watafika tu
 
Yaah nafahamu kuhusu CNSA na mafanikio yake ya anga habari zake nafuatilia ila bado hawaja fikia mafanikio ya ya Nasa ya anga kutokana na sababu mbalimbali.

Ila kwa sasa wapo moto na ninaona kwa miaka ijayo kama speed yao waliyo nayo sasa wakiongeza wenda watafika mbali.

Ila binafsi naikubali Nasa wapo vizuri
Nasa ipo kwenye game kitambo.
CNSA imepiga hatua kubwa. Na NASA now analegalega historia imebaki kumbeba ndio maana projects nyingi now anazioutsource kwa private companies. Mfano space x ndiye atatengeneza chombo kitachoenda mwezini.
Moja kati ya sababu ya nasa kulegalega ni budget, serikali ilikata budget ya nasa kwa kiasi kikubwa toka utawala wa bush nadhani.
Halafu projects nyingine ni collabo. mfano james web ni collabo kati ya Nasa na shirika la amga la ulaya.
China naye anaunda darubini inayofanya kitu kile kile kama jamesweb ila yake itakuwa ni darubini ndogo ndogo zilizokaa angle tofauti na zinatazama kwenye point moja at a time kisha zinaunganisha picha kuwa moja.
 
Hata China itafika muda shirika la taifa litafanya ushirikiano na mashirika binafsi katika tafiti na urushwaji wa vyombo.

Mambo ya space yana gharimu fedha nyingi ambazo ni kama hasara kubwa kwa serikali kufund lazima ifike muda serikali inyooshe mikono tu
 
At least umeelewa NASA iko juu ya huyo Mchina unayemtetea

Hebu turudi kwa Space X, naomba utaje jina la hilo shirika la China unalosema limefanya hayo yote ili nijue unataka kumlinganisha Space X na nani specifically.

I mean jina kama unavyoitamka NASA au Space X, nitajie hiyo ya Kichina nataka niifuatilie
China ina space technology inayokua haraka ila haina kelele kabisa na taarifa zake zimekuwa ignored na dunia. Watu ukiwaambia China inaizidi Russia kwenye space technology wanabisha.

Kwa sasa kwenye space itakuwa dominated by the US and China.
 
Najua haujaijua Huawei vizuri, upande wa simu ndio sanctions ya Marekani imeumiza lakini Huawei is more than smartphones

Na upande wa smartphones amerudi sasa ni suala la muda kuona Huawei anarudi kivingine kwenye soko la dunia
Kwenye smartphones Huawei ameshaumizwa na Mmarekani

*Huawei P60 Pro ni simu expensive kama shilingi milioni mbili hivi na bado inaishia internet speed ya 4G tu kutokana na limitation za chipset ambazo Mmarekani amempatia, Nani anataka simu expensive isiyo na 5G tena haiko optimised na Google services

Huawei ataendelea kutengeneza simu zenye hardware nzuri ila kwenye software atakosana na wengi. Sio kwamba software yake ni mbaya ila haiko optimised kwa matumizi ya Google services, plus app developers wako busy na kutengeneza apps kwa ajili ya Android na iOS sio HarmonyOS.

Huawei itabidi aendelee kutumia Android kwenye simu zake za Ulaya maana bila Mmarekani hatoboi. Hiyo HarmonyOS aiache kwa Wachina hukohuko

Huawei kwenye soko harudi tena. Kwa China kwenye simu ongelea kampuni kama Xiaomi, Oppo, Vivo, One Plus, Honor, nk ila sio Huawei tena
 
Hata China itafika muda shirika la taifa litafanya ushirikiano na mashirika binafsi katika tafiti na urushwaji wa vyombo.

Mambo ya space yana gharimu fedha nyingi ambazo ni kama hasara kubwa kwa serikali kufund lazima ifike muda serikali inyooshe mikono tu
Kilichopo kati ya US na china ni sawa na vita baridi ua tech.
Inahitaji uwekezaji. China ana pesa ya kutapanya nyingi tu kwa sasa anaweza kuitapanya kokote kwenye agency zake. Na ndio maana ulaya wamekuja kushtuka china anataka kunua kampuni zao zote ambazo zinashikilia technology adimu hadi sasa wameweka vikwazo haijalishi ni private company haziuzwi kwa mchina hivi hivi.
The game is on... Tutazame nini kitafuata
 
Kwenye smartphones Huawei ameshaumizwa na Mmarekani

*Huawei P60 Pro ni simu expensive kama shilingi milioni mbili hivi na bado inaishia internet speed ya 4G tu kutokana na limitation za chipset ambazo Mmarekani amempatia, Nani anataka simu expensive isiyo na 5G tena haiko optimised na Google services

Huawei ataendelea kutengeneza simu zenye hardware nzuri ila kwenye software atakosana na wengi. Sio kwamba software yake ni mbaya ila haiko optimised kwa matumizi ya Google services, plus app developers wako busy na kutengeneza apps kwa ajili ya Android na iOS sio HarmonyOS.

Huawei itabidi aendelee kutumia Android kwenye simu zake za Ulaya maana bila Mmarekani hatoboi. Hiyo HarmonyOS aiache kwa Wachina hukohuko

Huawei kwenye soko harudi tena. Kwa China kwenye simu ongelea kampuni kama Xiaomi, Oppo, Vivo, One Plus, Honor, nk ila sio Huawei tena
Huawei P60 ina run 5G mpaka satellite call nafikiri kwa makampuni yote duniani ya simu upande huo kwa matokeo mapya wao wanaongoza
 
Back
Top Bottom