CHINA: BYD waweka rekodi mpya wazindua gari linaloweza kwenda zaidi ya km 2000 bila kuongeza mafuta wala kuchaji na matumizi kidogo sana ya mafuta

CHINA: BYD waweka rekodi mpya wazindua gari linaloweza kwenda zaidi ya km 2000 bila kuongeza mafuta wala kuchaji na matumizi kidogo sana ya mafuta

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
3,651
Reaction score
11,548
Kampuni ya kutengeneza magari ya BYD imezindua gari la mfumo wa Plug-in Hybrid Electric Vehicle (PHEV) PHEV ni magari ambayo yana mifumo miwili umeme na mafuta.

Kwa maneno rahisi kama chaji kwenye battery imeisha unatumia mafuta and vice versa. Model hiyo imepewa jina la BYD Qin L.

Ukijaza full tank na ukachaji mara moja tu battery (single charge) chuma inatembea zaidi ya km 2000.

Ilipofanyiwa majaribio ilitembea umbali wa km 2409 kutoka Xian mpaka Changchun.

Km 2400 ni sawa na umbali wa kutoka Dar mpaka Harare, Zimbabwe non-stop.

Rekodi nyingine ya gari hillo ni matumizi kidogo ya mafuta. Linatumia lita 2.9 za mafuta kwa umbali wa km 100 (2.9/100km)

Bei yake ni 14,000 USD (Tsh 36 milioni) hadi 19,000 USD (Tsh 49 milioni) unaanza nayo 0 km.

BYD Qin L imevunja rekodi iliyowekwa na gari lingine la mfumo wa PHEV iliyotembea km 1100.

20240529_224237.jpg

20240529_224200.jpg
20240529_224234.jpg
 
Gari za mfumo wa PHEV ni gari nzuri sana hasa kwa nchi zetu ambazo hatuna miundombinu ya full EVs

BYD waanze kuwa serious na soko la nchi zetu za Afrika. Chuma 0km kwa milioni 40 mbona wadau wengi Bongo watazinunua
Ndio maana nchi za Latin America kama Brazil na Mexico wametokea kuzikubali sana BYD phev na Australia pia
 
Gari za mfumo wa PHEV ni gari nzuri sana hasa kwa nchi zetu ambazo hatuna miundombinu ya full EVs

BYD waanze kuwa serious na soko la nchi zetu za Afrika. Chuma 0km kwa milioni 40 mbona wadau wengi Bongo watazinunua

Sema mchawi TRA
FAW wana mpango wa kufungua kiwanda cha EVs nchini Egypt ambacho bei zake zitakuwa nafuu naona hapo wamefocus soko la Africa
 
Back
Top Bottom