Kipilipili
JF-Expert Member
- May 25, 2010
- 2,272
- 1,897
- Thread starter
-
- #201
Kipilipili tafadhali naomba namba yako nataka nikuulizie
Siko la asali sina details za soko lake hapa China.
Natoa wito kwa wengine wanaotaka ku export bidhaa zao nje ya nchi wanitumie majina ya vitu hivyo kisha nitavituma kwa wahusika
Mkuu vipi machine au printa za kusafisha picha. Ambazo ni refarbished zinapatikana mji gani. Thanx in advance
Kipilipili......very very useful thread, remain blessed dear.
Ninemepata kitu. good Kipilipili
kipilipili, hongera sana, makala yako ni nzuri sana, ila hebu zungumza kidogo na opportunities za ku-export. website zipi mtu anaweza kutembelea akapata taarifa hizo?
Natamani kama tungepata watanzania kumi kama wewe!!!hngera sana sana,huwezi amini my cusine ndo anaanza trip ya china kwa makala yako amebadili mwelekeo wa biashara toka nguo za kike hadi mauwa na phone gadgets na amekwenda tafta ordrs kwanza b4 asafirim!!thanx alot na hotel and other infos kuhusu usafirishaji na mengine!!!!!!
nahitaj kujua gharama za kutuma mzgo toka China how much per kg?
looking ur a good clearing agent
mkuu, uzoefu wangu hasa ni wa kutoa bidhaa huku kuja Tanzania. Hili nitalifanyia kazi kisha ntaleta mrejesho In Sha Allah. nimewahi kuona baadhi ya watu wakileta mizigo china lakini wengi wamekua wakisema sheria na taratibu za uingizaji bidhaa huku zinabana ukilinganisha na nyumbani
Habari wana jukwaa,
Kumekuwa na ongezeko kubwa la wafanyabishara kutoka Tanzania kwenda China kufanya biashara mbalimbali kama nguo, vipuri vya magari na pikipiki, vifaa vya electronics nk. Najua kuna thread nyingi zimewahi kuzungumzia biashara za China, lakini nimuombe mkuu Invisible aifanye hii iwe sticky thread ili iwe refernce point kwa kila anaehitaji kufanya biashara China.
Nitaeleza KIDOGO Kuhusu biashara za China.
BIASHARA YA NGUO: hii inapendwa sana kufanywa na kina dada japo wanaume pia wapo. Wengi walio wageni na biashara hii wamejikuta wakipata hasara hasa wanapofika tu miji kama Guanzhou na kuanza kununua nguo bila kuangalia hali ya soko Tanzania ikoje.
Hujikuta wakinunua nguo on their perspective and not customers perspective! Kinachowavutia machoni mwao ndicho wanachonunua kwa matarajio watauza tu. Wengine wananunua na wanapofika na mzigo kariakoo wanakuta mzigo kama huo uloshaingia a week/month before hivyo kujikuta wanauza kwa bei ya hasara.
Ushauri: jaribu kutafuta wateja kabla Tanzania , wakupe order na sample kisha ukifika China nunua kile walichokuagiza.Pia jitahidi ujue ni fashion gani bongo iko sokoni na mpaka mzigo umefika bongo,je bado hiyo fashion ulionunua itakuwa inauza? Mind you kwamba biashara ya nguo hasa za WANAWAKE zinaendeshwa kwa nguvu ya soko na fashion hubadilika mara kwa mara!Biashara ya nguo za watoto au wanaume kidogo fashion zake zinakaa muda mrefu ukilinganisha na za wanawake.
BIASHARA YA VIFAA VYA ELEKTRONIKI kama simu na accessories zake, music system n.k
Miji mizuri ya kununua mzigo kwa biashara hii ni Shenzhen na Honkong ,japo mji wa Guanzhou pia ni maarufu isipokuwa fake products kwa Guanzhou ni kubwa zaidi. Changamoto kubwa ya biashara hii ni FAKE PRODUCTS. Angalia wateja wako ni watu wa namna gani. Most low income earners ambao kwa Tanzania ndio wengi, wanapenda cheap price.
Kwahiyo, ukinunua genuine products huwezi kuuza bongo kwa sababu bei itakuwa iko juu na wao watashindwa. Kwa hiyo jua needs and wants za customers wako kabla hujaamua kununua mzigo.Kwa mtu mwenye mtaji mdogo unaweza kuanza na kununua phone acssesories na simu chache tu za bei ya chini, utakuwa unaongeza idadi ya simu kidogo kidogo kadri mtaji unavyokua.Pia kama una mtaji mkubwa unaweza kuingiza used products kama photocopier machines ila jitahidi uwe na orders kabla hujaleta kwa sababu ukija nazo nyingi bila order zinaweza kukaa muda mrefu ukajikuta unaanza kula mtaji.
Wakati unasafirisha photocopier machines jitahidi ununue vitu vidogo vidogo kama vile memory cards, USB cards, power banks nk na uviweke pamoja ndani ili ukija bongo wakati unasubiri kuuza photocopier machines unauza hivyo vitu vidogo vidogo ili kupata faida kidogo kidogo na kuhakikisha huli mtaji.
Kumbuka hapa utasafirisha kwa meli na huwa wanapima CBM na sio uzito kwa hiyo hivyo vitu vidogo vidogo cost yake ya kusafirisha itakuwa imemezwa na hizo machines.Photocopier machines nimetoa kama mfano wa moja ya bidhaa lakini vipo vimashine vingi tu ambavyo unaweza kusafirisha kama:Mashine za juice ya miwa, hizi zimekuwa na demand kubwa sana kwa sasa Tanzania. Wateja wake wapo , kama utakuwa na mtaji mzuri unaweza kununua hizi na kuleta. Nyingi ni portable na modern. Ni kiasi cha kutafuta orders na kisha kuleta.
Kuangalia bei mbalimbali za bidhaa tembelea:
Manufacturers, Suppliers, Exporters & Importers from the world's largest online B2B marketplace-Alibaba.com
Made-in-China.com mobile- Connecting Buyers with China Manufacturers, Suppliers & Products
www.taobao.com (hii ni ua kichina, tumia browser ya google chrome na tumia kitufe cha translation ili ije kwa kingereza)
USAFIRI: Zipo kampuni nyingi zinazosafirisha mizigo kwa njia ya ndege na meli. Kampuni kama THE LAND, SILENT OCEAN ni baadhi tu na hizi zina ofisi zao pale pale Guanzhou na bei zake zinatofautiana kutegemeana unasafirisha kwa njia gani yaani ndege au meli. Na unapolipia wao ndio huhusika na clearance na kila kitu, wewe ukifika bongo unachukua tu mzigo wako kwenye Ghala lao.
Website ya baadhi ya makampuni ni:
http://www.silentoceanlimited.com/
NAULI:nauli zinategemea season na pia unataka kusafiri lini. Kipindi cha high season kama ,july, august bei zinakuwa juu. Kama kwa mfano unatarajia kusafiri July basi ikifika april kata tiketi mapema . Mara nyingi kunakuwa na offer kwenye mashirika ya ndege kwa hiyo pendelea kutembelea website zao.
Pia nauli inategemea na shirika la ndege unalotaka kusafiria na pia daraja unalotaka kukaa.
Kwa wafanyabiashara wengi hutumia ethiopian airline kwa sababu huwa wanatoa kg nyingi kuliko wengine.
Pita kwa mawakala posta na kariakoo au search google kupata bei mbalimbali za nauli. Unaweza kutenga bajeti ya USD 900-1200 Kwa nauli kwa economy class
Angalia bei za NAULI hapa:
http://www.ethiopianairlines.com/en/default.aspx
Qatar Airways | Book Flights with the World's 5 Star Airline
https://www.klm.com/?_e_pi_=7,PAGE_ID10,8626374365
MALAZI: Hapa nitazungumzia mji wa Guanzhou ambao ndio wenye wafanyabiashara wengi wa mataifa mbalimbali hasa Afrika. Zipo hoteli za hadhi tofauti, bei kutoka 120 yuan(36,000 Tsh) ikiwa ni bei ya chini labisa na kuendelea kutegemeana na mfuko wako. Maeneo kama "shaobei lu" ni maarufu kwa watu weusi na utakisikia kiswahili kila baada ya hatua kadhaa. Hoteli za pembeni ya mji bei huweza kuwa chini mpaka yuan 100.
Angalia range ya bei za hoteli hapa:
GuangZhou hotels: cheap rates in GuangZhou by China Hotels Reservation
CHAKULA: zipo hoteli nyingi Guanzhou na shenzen zinazomilikiwa na foreigners na wanauza chakula kizuri japo kiko ghali kidogo, ila kama unahitaji chakula cha bei ya chini na ambacho ni HALAL (wengi huhofia kulishwa mbwa,kitimoto,nk) unaweza kula kwenye sehemu nyingi ambazo huuza wachina waislamu wenye asili ya Xinjiang ambao huuza HALAL food kwa bei poa kuanzia Yuan 15(4500 Tsh) na kuendelea kutegemea na aina ya chakula ulichoagiza. Kuwa makini na vyakula mana wale wenzetu huwa wanakula vyakula vingi vya "ajabu ajabu".
LUGHA: wachina hutumia lugha yao kwa kila kitu. Katika miji ya biashara kama Guangzhou wachina wafanyabiashara huongea kingereza cha mawasiliano(kibovu) ila mnawasiliana na kuelewana. Pia lugha ya ishara inatumika pale panapokuwa na language barrier . Hata kama hujui kabisa kingereza unaweza kuchagua bidhaa na kisha mkapatana bei. Wenzetu wana utaratibu wa kutumia calculator kukuandikia bei, hivyo na wewe utaandika ya kwako mpaka mtafikia makubaliano. Nashauri download application yoyote ya TRANSLATION kama pleco nk ili ikusaidie kwenye mawasiliano unapokwama andika neno unslohitaji kwa kingereza kisha tafsiri kwa kichina na muoneshe mchina hilo neno, itasaidia kurahisisha mawasiliano
Nimegusa juu juu vitu vichache mno kuchokoza mada ili wengine waongezee uzoefu na iwe msaada kwa kila anaetaka kufanya biashara China.
Karibuni tujadili na kusaidia wengine
Kipilipili...kuna soko la bidhaa ghafi nalihitaji kutoka china hasa viwanda vya biochemical...wapi naweza kupata directory yao
Ndugu Pilipili
tunashukuru sana kwa jambo hili ambalo unalifanya.
naomba kujuwa hali ya usalama katika hiyo miji, yaani kama kuna wizi wa mara kwa mara, uporaji na mengine kama hayo
Asante sana Kipilipili. Nilishaanza mdogo mdogo nikijiandaa kustaafu.