Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Hapo jana waziri wa mambo ya nje wa China alifanya mazungumzo na waziri mwenzake wa mpito wa Iran ndugu Ali Bagheri Kani na kuweka wazi misimamo ya nchi yake katika mzozo unaofukuta hapo mashariki ya kati.
Katika mazungumzo hayo waziri huyo wa China aliweka wazi kuwa kuuliwa kwa kiongozi wa Hamas,Ismail Haniye ndani ya Iran ilikuwa ni kitendo cha kichokozi na ukiukwaji wa maazimio ya kimataifa ya kuheshimiana kati ya nchi na nchi.
Tamko hilo la China linakuja wakati Pentagon imeidhinisha kupelekwa kwa meli zaidi ya kivita katika eneo la mashariki ya kati pamoja na silaha mbali mbali za kivita kutokana na kitisho cha vita vya wazi kutokea baina ya Israel na majirani zake.