Chonde chonde Rais Samia, Kipengele cha Dini kwenye sensa ni muhimu sana kwa sababu hii

Katiba mpya ni muhimu sana kwa sasa ...... yaani hata namna ya kufanya sensa inabidi aombwe Rais ..... !!
 
Moderator futa hii post ni kidini, kibaguzi,ina ubaguzi. Hii neo colonialism na no unazi momboleo. Ndio Mtumishi Putin' anawachapa hawa hawa wanazi.mkabila, mdini. Hawa hatari katika duniani. Analeta vitakwimu uchwana. USA, China, JAPAN, GERMANY, INDIA, IRAN, SAUDI ARABIA, RUSSIA,RUSSIA. 80% Kuna dini moja huku 40%Hakana dini .Huku China, India No Christian no Islamic. mbona kuna maendeleo.
 
Mfumo wa kijana hauruhusu sensa ya dini. Yakupasa utambue kuwa Tanzania tumechanganyika sana. Usipandikize chuki na ubaguzi katika kutoa huduma kwa wananchi. Dini ni kwaajili ya kuabudu na si kutoa huduma za kijamii.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Hivi nchi zote zikifanya sensa huwa zinafanyaje ?

Zinaacha kuhusisha kipengele cha dini ?

Au sie ndio wa pekee ?

Tanzania ni sehemu ya Dunia.
 
Halafu inasemekana ni dini moja tu kati ya nyingi zilizopo nchini Tanzania ndio haitaki kuwepo na hicho kipengele cha dini wakati wa sensa.

Tujiulize Kwanini wanahofia kufanyika Kwa jambo hilo ?

Kwanini dini nyingine hazioni shida kuwepo kwa kipengele hicho kwenye sensa isipokuwa watu wa dini hiyo tu?
 
Science and studies na wavumbuzi wa maswala ya sensa wanataka kipengele cha dini kiwemo ,

Inakuwaje kikundi cha watu wajitokeze kukataa halafu wakubaliwe ?

Nadharia ya sensa inasemaje?
 
Serikali ndio iliyokataa kuweka hicho kipengele, kama Kuna dini imekataa hilo itaje.
 
Serikali ndio iliyokataa kuweka hicho kipengele, kama Kuna dini imekataa hilo itaje.



Inakataa Kwa sababu gani ?

Je wamekewa wakieleza wananchi sababu hizo ili tuone kama zina mashiko au la ?

We are not isolated in the World.

Ni nchi gani inafanya sensa na kuacha hicho kipengele?!

Waloanzisha nadharia ya sensa wameainisha vigezo vya kuzingatiwa katika kufanyika sensa.

Sasa kama unaamua kufanya ili upate matokeo sahihi ni lazima ufuaate na uzingatie yale yanayotakiwa.
 

Sizani kama kuna nchi duniani haihesabu sensa ya dini.
 
Naunga mkono 100%., tupaze sauti mama anatakiwa kuliona hili na aache mazoea, nyerere alikuwa mwanadamu mahitajio ya sasa na miaka ile ni tofauti sana, dunia inaenda kwa kasi sana.
 
Nendeni mkahesabiane kwenye mistiki..masinagogi na makanisa yenu kisha mtuletee takwimu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kama huna dini utaingia kwenye category ya wasio na dini., muhimu kujua mahitaji ya wanadini katika maeneo mbali mbali nchini na hata wasio na dini ili kuleta maendeleo kwa ufanisi zaidi, nchi nyingi ulimwenguni zinahoji dini si kwa shari lakini kwa mahitaji.

Nyerere alikuwa mwanadamu sasa dunia imebadilika theory yake hayakuwa maneno yaliyoandikwa kwenye vitabu vitakatifu
 
Nendeni mkahesabiane kwenye mistiki..masinagogi na makanisa yenu kisha mtuletee takwimu.

#MaendeleoHayanaChama
Kwenye sensa ya nchi mkuu, ondoeni hofu ni kujua tu mahitaji wanadini na wasio na dini pia
 
Elimu haina dini, afya haina dini. sote tusiokua na dini na wenye dini tunapata sawa.

Hakuna sababu ya kipengele cha dini. Sensa inaenda kuhesabu idadi ya raiawote wa Tanzania, haiendi kuhesabu wenye dini fulani wako wangapi.
Raia wa Tanzania unao waongelea hapo asilimia 90 ni wana dini, hili suali la dini kuwepo litasaidia kwenye mahitaji ya maendeleo kama alivyofafanua mtoa mada. ni hivyo tu mama azingatie.
 
Sio ubaguzi ni uhitaji wa maendeleo kutokana na dini zao hili jambo ni mashuhuri mtoa mada ametola mfano wa nchi za mataifa ya Morocco na mengine ya kiislamu mbona wao hawakuja na hoja hizo unazoziwaza wewe.

Ni vile wakiristo wengi wanahofu kujiona katika Taifa la Tanzania idadi yao ni chache lakini hili suali likiwekwa halitamaanisha hivyo ni kwa sababu ya mahitaji tu
 
uko juu mkuu wape figure hizi waondoe hofu
 
Naunga mkono 100%., tupaze sauti mama anatakiwa kuliona hili na aache mazoea, nyerere alikuwa mwanadamu mahitajio ya sasa na miaka ile ni tofauti sana, dunia inaenda kwa kasi sana.

Watanzania kila kitu tuko nyuma, yani wamwisho. Kwenye suala la sensa sidhani kama mama atakua amejiamulia mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…