Chonde chonde Rais Samia, Kipengele cha Dini kwenye sensa ni muhimu sana kwa sababu hii

Chonde chonde Rais Samia, Kipengele cha Dini kwenye sensa ni muhimu sana kwa sababu hii

Serikali hana dini, ila watu wake wanadini na serikali ipo kwa ajili ya kuwahudumia watu hao. Na ndio maana mtumishi wa serikali akifa itashughulikia maziko yake kwa mujibu wa imani yake. Au hata wewe ukikutwa leo mfano umekufa na ukasachiwa mfukoni ukakutwa na kitamburisho unaitwa John Richard (Mkristo) utazikwa kwa imani hiyo. Huoni kuwa serikali inauhitaji wa kufahamu dini yako? Ukizungumzia mipango ya maendeleo aidha kijamii, uchumi, nk huwezi kuepuka matumizi na uhitaji wa takwimu sahihi. Utachekesha.
Na tusio na dini umetuandalia sehemu ya kutuweka?

Maana katika hoja yako ujagusa kundi letu..!
 
Naunga mkono hoja. Suala hili serikali isiendeshwe kwa mihemko ya baadhi ya watu badala yake ijikite kwenye kuona tija za takwimu kwenye maamuzi na mipango ya mambo mbalimbali. Nasisitiza kipengele cha dini ni muhimu sana kiwepo kwenye sensa. Kiujumla sensa ni gharama sana, sasa serikali ichukue kila aina ya data hata kama zitakuja kutumiaka miaka ijayo. Hakuna mtu atakuja kunyang'anywa dini yake eti kisa serikali imexhukua takwimu. Hatuweza kufanya mambo ya kubahatisha na mabunio ya kitakwimu wakati tunafursa ya kupata yakwimu halisi.
 
Serikali hana dini, ila watu wake wanadini na serikali ipo kwa ajili ya kuwahudumia watu hao. Na ndio maana mtumishi wa serikali akifa itashughulikia maziko yake kwa mujibu wa imani yake. Au hata wewe ukikutwa leo mfano umekufa na ukasachiwa mfukoni ukakutwa na kitamburisho unaitwa John Richard (Mkristo) utazikwa kwa imani hiyo. Huoni kuwa serikali inauhitaji wa kufahamu dini yako? Ukizungumzia mipango ya maendeleo aidha kijamii, uchumi, nk huwezi kuepuka matumizi na uhitaji wa takwimu sahihi. Utachekesha.
Kwamba Serikali itasaidiwa kwa kupata takwimu ya fulani dini gani ili iweze kumsaidia kumzika ?

Serikali inazika watu ? Badala ya kuwaza jinsi ya kuhakikisha kila mtu anapata Bima / Matibabu ambayo ni affordable wewe unaweza huduma ambazo Serikali inaweza ikatoa kwa Imani ya mtu husika (wakati inashindwa hata kutoa kwa tabaka ambalo ni Mtanzania na wote tumo humo)

Tusianze kujigawa gawa..., Umoja ni Nguvu na sisi ni Wamoja wa kila mtu na Imani yake Kivyake bila bughuza kwa Imani nyingine..., mimi sihitaji kujua wewe ni Imani gani wala haitanisaidia kitu..., tutajuana na kukutana mahekaluni na misikitini au usiku wakati tunawanga....
 
Kipengele cha dini hakina tija yoyote. Kuna wengine hatuna dini ne itakuwaje?

Pia kipengele cha kabila nacho hakina tija. Mimi baba yangu ni Mmasai na mama ni Mchaga ila nimezaliwa na kukulia uchagani mpaka nimekuwa mtu mzima na hata kwa baba yangu huko Nainokanoka sijawahi kufika.

Najua mila na tamaduni za kichaga na lugha ya kichaga naijua pia ila kimasai sikijui.

Je mimi ni Mmasai au ni Machagga?
Kama huna dini unaitwa tu Mpagani mbona simple? Kwa ni wewe usipokuwa na dini ndio wengine wote wasijulikane wala serikali isiwe na takwimu sahihi?

Angalia takwimu za waumini (idadi) kwa nchi ya Israel ilivyo hapa chini ambapo kipengele cha dini. Ingawa ukisikia baadhi wanavyojitapa na kujilikisha Israel utadhani wapo kwa 90%. Let data speaks for itself and use it for better
Screenshot_20220309-160150.jpg
 
Kwanini msijihesabu huko makanisani/ misikitini mkajuana idadi kuliko kuleta mkanganyiko kwa wanajamii
Basi hata kipengele Cha kabila, elimu nacho kitolewe. Watu wajihesabu huko makwao
Taarifa ili ziwe sahihi ni lazima zisimamiwe na mamlaka sahihi
Wakijihesabu huko Nani ataverify uhakika wa taarifa zao?
 
Wa kundi fulani kujiona wako wengi na wengine labda wachache, unadhani miaka yote kwanini serikali huwa haiweki hiki kipengele cha dini?
Kwani kwa mfano hata sasa tunajua kuwa Kabila ka Wasandawe na Wazanaki ni wachache sana na Kabila Kama Wasukuma ni wengi sana. Eleza athari kubwa waliyoipata Wazanaki kwa Kujua kuwa ni Wachache.
 
Rais wetu usifungwe kwa miiko, watu wengi ikiwemo wewe wameleta mabadiliko chanya kwenye jamii kwa kuvunja miiko, tuangalie faida na hasara zake sio kwa kuwa halikuwahi kufanyika

Hili suala haina haja ya kulichukulia kwa shari na kutokuaminiana, tujadili kwa utulivu na kwa reason
Kipengele cha dini hakina maana....

Dini ni imani ya mtu...

Watanzania wanahitaji mahitaji muhimu ya kibinaadamu yanayofanana ambayo dini haihusiki chochote kile.......

1)Elimu
2)Afya
3)Miundombinu
4)Umeme
5)Fursa za kibiashara
6)Uchumi imara

#Siempre JMT🙏
 
Watu wanajua kuvaa kanzu, kufuga ndevu na majini maendeleo watayatafutaje?
Kwa hiyo wewe kijijini kwenu mnaovaa rozali na kuabudia lile sanamu pale mbele ya jengo mnawazidi Maendeleo Egypt, Oman na Dubai ambao katika hao waislamu? Acha Uzwazwa. Ukichukua matajiri wakubwa Tanzania ktk top 10 Wakristo ni 2 Tu. Same applies to the rank of Africa. Ndio maana takwimu ni muhimu
 
Kama kipengele hiki hakitakuwepo kwenye sensa hii, basi kifutwe na kwingine kokote ambapo huwa tunaulizwa dini zetu kwa mfano wakati wa kuomba kazi, kujiandikisha uraia, kupiga kura, kuomba passport, ukifika Police kuandikisha maelezo, kununua ardhi / mashamba nk
 
Bado Sana hoja Yako haina mashiko.

Mnataka Dola La Kiislamu.

S
Serikali hana dini, ila watu wake wanadini na serikali ipo kwa ajili ya kuwahudumia watu hao. Na ndio maana mtumishi wa serikali akifa itashughulikia maziko yake kwa mujibu wa imani yake. Au hata wewe ukikutwa leo mfano umekufa na ukasachiwa mfukoni ukakutwa na kitamburisho unaitwa John Richard (Mkristo) utazikwa kwa imani hiyo. Huoni kuwa serikali inauhitaji wa kufahamu dini yako? Ukizungumzia mipango ya maendeleo aidha kijamii, uchumi, nk huwezi kuepuka matumizi na uhitaji wa takwimu sahihi. Utachekesha.
 
Mnajisumbua tu, hicho kipengele hakiwezi kuwekwa na hakitawekwa, kama mnajiona inferior bakini hivyo hivyo, nendeni mkahesabiane huko kwenye misikiti yenu kisha mtajua mfanyeje na wingi au uchache wenu.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama huna dini unaitwa tu Mpagani mbona simple? Kwa ni wewe usipokuwa na dini ndio wengine wote wasijulikane wala serikali isiwe na takwimu sahihi?

Amgalia takwimu za waumini (idadi) kwa nchi ya Israel ilivyo hapa chini ambapo kipengele cha dini. Ingawa ukisikia baadhi wanavyojitapa na kujilikisha Israel utadhani wapo kwa 90%. Let data speaks for itself and use it for better
View attachment 2144519
Kwani Serkali ya Israel haina Dini kama Serikali yetu ?

Mmekatazwa kujihesabu kwani ?, Sensa hii inataka idadi ya watu ili kutoa / kupeleka huduma fulani.., sasa the last time I checked kuhudumia Dini / Imani za watu sio mojawapo ya Objectives za Taifa hili..., bali kuhudumia wananchi kwa ujumla
 
Hivi kipengele cha dini kinaathiri nini taifa kikiwekwa?
 
Dini ni suala la imani na imani ni jambo binafsi la moyoni, na wakati mwingine linaweza kubakia kuwa ni siri binafsi ya mtu moyoni, linaweza kubadilika kwa mtu binafsi kwa dakika, saa, siku nk.

Kwa mfano: Asubuhi ninaweza kuwa muislamu, mchana nikawa mkristo, jioni nikawa mpagani na usiku nikawa mshirikina. Sasa hapo dini yangu ni ipi?

Wapo 'waislamu' kibao wanashinda kutwa nzima au kukesha usiku kanisani kwa mzee wa upako, Mwamposa nk wakiombewa. Sasa sijui hawa tuwaweke kundi gani?

Mwisho wa yote dini zipo nyingi sana, tusikariri dini ni ukristo na uislamu tu, hata huko kwenye ukristo na uislamu kuna utitiriri wa vidini vingi vidogo vidogo vinavyoibuka na kufifia kila siku. sasa sijui unawezaje kulifanyia tathmini kitakwimu jambo lisiloweza kuelezeka kwa uhalisia.

Takwimu za idadi ya waumini wa dini fulani libakie mikononi mwa dini husika, wao wenyewe wajihesabu na kujipangia mambo yao ya kidini, tusilazimishe serikali kujiingiza kwenye mambo yao ya ndani.
 
Watu wanajua kuvaa kanzu, kufuga ndevu na majini maendeleo watayatafutaje?
Matajiri wakubwa Tz ni wa dini gani vile?
Endeleza kibanda chako cha kuuza Bidhaa za Said Salim Bakhreesa na Mohammed Dewji
 
Back
Top Bottom