Kila utafiti huwa na malengo yake. Hayo uliyoyaainisha yanatakiwa kuwa katika National Surveys siyo census ambayo ni total head count. Dhumuni kuu la Sensa yeyote ni kwa ajili ya kupata takwimu kwa ajili ya Mipango ya Maendeleo ya sehemu husika.Rais wetu usifungwe kwa miiko, watu wengi ikiwemo wewe wameleta mabadiliko chanya kwenye jamii kwa kuvunja miiko, tuangalie faida na hasara zake sio kwa kuwa halikuwahi kufanyika
Hili suala haina haja ya kulichukulia kwa shari na kutokuaminiana, tujadili kwa utulivu na kwa reason
Dini imekuwa sehemu muhimu sana ya maisha ya mtanzania na kwa maana hiyo utamaduni wa Watanzania wengi umeathiriwa na dini waliyo nayo
Na utamaduni una effect kubwa kwenye maendeleo ya mtu, jamii na taifa
Mfano mikoa ambayo ipo percived kuwa na waislam wengi, nasema percived kwa sababu hakuna takwimu rasmi
Mikoa hii ni kama Kigoma, Lindi, Tanga, Mtwara na wilaya za mkoa wa Pwani zilizo mbali na Dar, mikoa hii kumekuwa na umasikini mkubwa na huduma za kijamii kama Hospitali, shule, barabara pia ni duni, sasa tunataka kujua kuna uhusiano wowote kati ya maendeleo ya mkoa huu na dini (ambayo ina infuence culure yake?) au ni mikoa ambayo Serikali ilijisahu kwa bahati mbaya tu kupeleka maendeleo kama mikoa mingine?
Na kama haina maendeleo kwa sababu ya kusahaulika na serikali, basi tuseme umasikini wao umechangiwa na culture yao ambayo kwa kiasi kikubwa inaathiriwa na Dini? Basi ikionekana utamaduni/dini ndio imechangia, basi Serikali ina kazi ya kufanya maana Dini ya Kiislam haimaanishi kukataa maendeleo, maana mataifa yaliyoendelea zaidi Afrika kama Egypt na Morocco ni ya Kiislam
Hii ni analysisi ya muhimu inayotakiwa kufanywa na Serikali kama serikali ina nia ya dhati ya kuleta kuondoa umasikini kwa usawa maeneo yote TZ
So hapa ndipo kipengele cha Dini kinakuwa cha muhimu,
Na sio hapa tu, pia serikali imekuwa ikishirikiana na taasisi za kidini za Kikristo na Kiislam kwenye maendeleo na ustawi wa Tanzania, kwa hiyo kuwa na takwimu kuhusu waumini wa imani fulani na ku share takwimu hizi na taasisi hizo za kidini ambazo zinashirikiana nao, italeta manufaa mengi kwa pande zote
Mfano Bakwata, Balozi za mataifa mbalimbali, na watu binafsi wamekuwa wakishirikiana na Serikali kujenga visima na misikiti kwenye maeneo yenye Waislam, hivyo serikali ingetupa takwimu tukajua maeneo ambayo yangepewa kipaumbele
Maswali yanayoulizwa ni kwa ajili ya kupata data ili serikali iweze kupanga mipango ya maendeleo. Mfano umri, serikali inataka kujua Watoto ni wangapi, ili iandae Chanjo; nguvu kazi ni wangapi, ili Ijidhatiti na Ajira; wanaopaswa kuwa shule ni wangapi ili iandae madarasa; wazee ni wangapi etc.
Maswali haya ni yale ambayo kwa utashi wako huwezi kuyabadili. Mfano mwanamke hawezi kujibadili kuwa Mwanaume au ukiwa na miaka 10 huwezi Kurudisha nyuma umri wako.
Dini ni kitu kinachobadilika Leo mimi ni muislam, kesho naweza kwenda kwa Zumaridi nikawa mlokole wa kizumaridi. Je, huoni hii kitu hakina tija? Leo utasema kuna waislamu 100 kesho wote wamekuwa wahindu! Uliza wakatoliki waumini wanavyoondoka kuwa walokole wakupe experience. Hivyo swali la dini katika Sensa halina maana ila katika tafiti ambazo zinatanywa ili kupata majibu ya matokeo fulani. Mfano kwanini sehemu hii watoto wengi wanakufa, hapo swali la dini ni muhimu