Hii issue ya Makonda kuhusishwa na ukatibu mkuu imenifungua macho kwenye mambo kadhaa...
- Kumbe hili kundi linaloitwa SG lipo, linaishi, na lina nguvu ndani ya Chama Cha Mapinduzi, ndio maana kwa namna fulani linaweza kuwavuruga kila litapoamua kufanya hivyo, nanyi kujibu mapigo inawalazimu kuhitaji muda kujipanga.
- Samia kama mwenyekiti wa CCM ni dhaifu, hajui ashike wapi wala aende na nani, au amsikilize yupi na asimsikilize nani, yupo yupo tu, ndio maana haya makundi yanaendelea kumyumbisha licha ya kuonesha dalili ya kujipanga muda mrefu uliopita kwa kuwaondoa wakina Lukuvi na Kabudi barazani.
- Kuna wastaafu ndani ya CCM wasiochoka kuitafuna kila wapatapo nafasi, hawaaminiki na yeyote, hawa wakiona upepo unavuma upande wao watasimama na mwenyekiti wao, lakini wakiona upepo unavuma upande mwingine, hawakawii kumgeuka mwenyekiti, ni mafisi wasio na aibu na ndio wanaunda kundi lingine na watoto wao.
- Kuelekea 2025, Samia anaweza kujikuta analazimika kutafuta uungwaji mkono toka sehemu nyingine, endapo hataendana na kile wale aliowaamini mwanzo watakachokitaka, atajikuta analazimika kutafuta uungwaji mkono mpya, na hapa ndio atakuwa kwenye hali mbaya zaidi, kwani muda hautakuwa upande wake, hivyo asishangae ikitokea akipigwa chini.
- Kwa hali ya mambo ilivyo, bado naiona panga pangua kwenye chama na serikali kuelekea 2025. Samia lazima aendelee kuwachuja wale atakaokuwa na mashaka nao, na kuwasogeza karibu wapya atakaoamini wataweza kumfikisha kule anapotaka kwenda.
Sent from my SM-G900H using
JamiiForums mobile app