Kuwa mwili mmoja si kufanya kazi au huduma ya aina moja pamoja. Bali ni kuwa na makubaliano ya pamoja ya kuheshimu na kujali kazi au huduma ya mwenza wako kama ya kwako.
Kuwa mwili mmoja ni kusaidiana, kutiana moyo na kujenga mahusiano mema pasina kutengana. Christina angeweza kuendelea na ndoto zake, huduma yake au uchungaji wake pasina kumwacha mumewe. Mume anaweza kuwa mchungaji na mke pia, au wakawa na huduma tofauti pasina kutofautiana.
Mume anaweza kuwa askari, mke akawa muuguzi.
Mume anaweza kuwa mhandisi wa umeme, mke akawa mchungaji.
Mke anaweza kuwa mfanyabiashara, mume akawa mchungaji, nk. Kila mtu katika ndoa ana kipaji chake, fani yake, utaalamu wake, huduma yake, wito wake au ndoto zake tofauti pasina kuathiri ndoa.
Christina kakosea kwa kutojua au kwa makusudi. Au la, kuna sababu nyingine asiyoisema ya kutengana kwake na mumewe.