Christina Shusho: Nilimuacha mume nitimize ndoto zangu

Christina Shusho: Nilimuacha mume nitimize ndoto zangu

Mke mwenza wa zuchu.. anajificha kwenye kwenye dini.. soon yatavumbuluka.. simba haachi nyama inayotembea.
Muda ni rafiki mzuri sana wa ukweli. Ipo siku tutakutana tena kujadili hiki tulichokuwa tunakisema, again, hawa wanawake wanaoleta ubishi hapa watakuja kuapprove kuwa hakunaga mwanamke imara anafanya maisha nje ya ndoa.
 
Wakati tunaendelea na comment fupifupi, na wewe msomaji kama Una mke anayetafuta ndoto zake tena ana masters yake, tia nywele zako maji.
Ukicheka na mharibifu atakuharibia maisha. Hawa sio wa kucheka nao hata kidogo. Akianza zengwe zake hapo hapo unafanya maamuzi magumu. Ukichelewa hawanaga akili hawa ya kutazama hasara watakazoleta maana anajua ukiendelea kuwa nae akiharibu utamtetea na kugharamikia uharibifu wake.
 
Mwimbaji nguli wa nyimbo za injili ambaye kwa sasa amegeukia kazi ya uchungaji, mchungaji Christina Shusho, amesema aliamua kuachana na mume wake ili atimize ndoto zake. Haya sio maneno yangu bali amenukuliwa akitamka maneno hayo na mtandao wa "5newsTZ"

View attachment 2959387

"Kusema ule ukweli mimi niliondoka kwa mume wangu ili nianzishe kanisa langu, nilijiongeza ili ndoto zangu ziweze kutimia maana kama ningeendelea kuungana na mume wangu sehemu moja ningeendelea kudidimia. Siku hizi hakuna mambo ya mke na mume ni mwili mmoja!! hiyo haipo utapotea ndugu yangu, wewe na mume wako au na mke wako hamuwezi kuwa sawa, hiyo haipo kila mtu ana njia zake"

"Na mimi siogopi watu nasema ukweli, haya ninayoyasema ndiyo yapo kichwani kwangu, huyu ndio mimi, kwanini niendelee kudanganya watu. Kwanza mimi licha ya kuwa Mchungaji lakini sipendi watu waniite Mchungaji Christina Shusho, sipendi na sitaki"-Christina Shusho Mwimbaji nguli wa muziki wa Injili

MAONI YANGU
Mimi namuunga mkono mchungaji kwa asilimia 100 kwani mume sio ndugu yako bali ni kama rafiki mliyekutana ili kuunda familia. Ukiona mume/mke anasababisha malengo yako yasitimie, achana naye mara moja. Nawashauri wanaume msiwe vikwazo kwenye ndoto za wake zenu. Namtakia kila la kheri mchungaji Shusho kwenye kazi yake mpya ya kueneza injili ya Bwana. Mungu ambariki sana.
Hapo hamna cha dini, ulokole wala uchungaji kabisa, ni kupiga pesa na kuliwa na manjemba yenye kiu aka Jimbo liko wazi.
 
Kuwa mwili mmoja si kufanya kazi au huduma ya aina moja pamoja. Bali ni kuwa na makubaliano ya pamoja ya kuheshimu na kujali kazi au huduma ya mwenza wako kama ya kwako.

Kuwa mwili mmoja ni kusaidiana, kutiana moyo na kujenga mahusiano mema pasina kutengana. Christina angeweza kuendelea na ndoto zake, huduma yake au uchungaji wake pasina kumwacha mumewe. Mume anaweza kuwa mchungaji na mke pia, au wakawa na huduma tofauti pasina kutofautiana.

Mume anaweza kuwa askari, mke akawa muuguzi.
Mume anaweza kuwa mhandisi wa umeme, mke akawa mchungaji.
Mke anaweza kuwa mfanyabiashara, mume akawa mchungaji, nk. Kila mtu katika ndoa ana kipaji chake, fani yake, utaalamu wake, huduma yake, wito wake au ndoto zake tofauti pasina kuathiri ndoa.

Christina kakosea kwa kutojua au kwa makusudi. Au la, kuna sababu nyingine asiyoisema ya kutengana kwake na mumewe.
Mwisho wa siku tukubaliane kuwa mwanamke anapenda sana tamaa kuliko subira. Tena maisha ya sasa media na taasisi mbali mbali zinawajaza sana upepo kwa maneno ya kishujaa "unaweza" "mwanamke hiki mwanamke kile" basi na wao vichwa vinaota pembe wanataka ligi na mwanaume.
 
Sina Dini, mie ni Atheist.
Sasa unafanya nini kwenye uzi wa kiimani/kidini kama wewe ni Atheist a.k.a nonbeliever?

Yaani unasema wewe sio mlevi na unachukia pombe halafu kila siku unaenda pub unakaa high table, kwann unaenda sehemu ambayo una kili haupendi kuwepo? [emoji848]
 
umemuacha flora mbasha
Flora mbasha tunaweza mtetea mume wake naona alikuwa ni changamoto sana katika kumuongoza yeye kama mke.

Jamaa ndio wale wanaume ambao hawajakua vizuri so alikuwa hajafiti vizuri katika kumuongoza vema mkewe mixer alikuwa anachombezana sana na wanawake ikiwamo mdogo wake flora alikuwa anatakana na jamaa kingono ukizingatia jamaa ana mvuto so mabinti walikuwa wanamletea ligi sana Shangazi na unajua mziki wa watoto wa 2000 wakimtaka mwanaume wanambinu za kimafia kuwazidi shangazi zao.

Na inadhihirika kuwa jamaa alikuwa kama Marioo fulani kwa mke yaani mshika mikoba wa mke badala na yeye akaze kutafuta chochote ili kumsapoti mke yeye akawa kama chawa tena kwa mke sababu mke ni maarufu anapiga show so waishi kwa kipato cha mke.

So alishindwa kuendelea na jamaa kwenye mazingira hayo akaamua kuyamaliza na kutafuta mshikaji mwingine ambaye ndie wanaishi nae, sasa sijafahamu kama wamefunga ndoa ama wanaishi kwa cohabitation.
 
Watu mnahasira na Christina aiseeh!

Kwani ndoa ni lazima ?

Haya Yesu alimuoa nani ?

Hao watawa, mapadre wameoa na kuolewa na nani ?
Hatuna hasira za huyo uliyemtaja, binafsi nina shida kwenye sababu alizozitoa zilisomfanya aamue kuvunja ndoa..!!
 
Baada ya miaka mingapi tuje kuwauliza kama mmetimiza malengo yenu “makubwa”?

[emoji23]
Hizi ndoto zao za mchana huwa hazitoboi wakifika 40+ tu hapo utaona wanavyovurugwa chupi kichwani kilemba mkononi hawana ramani.

Hizi fujo wanazofanya ni ili kutafuta attention za kijinga, kutaka mashindano na wanaume na kupata uhuru wa kuliwa na kujipatia mapato kwa wanaume tofauti, umri ukianza kwenda utulivu sijui huwa unatoka wapi utashangaa ghafla wanapata akili ya Maisha ya ndoa na wanaanza kuforce kusettle na mwanaume yoyote yule hata kama hana hela wataforce waishi nae ikibidi yeye mwanamke ataanza kumpa pesa mwanaume ili atulie nae.

Wewe tulia usiongee chochote, nashangaa hata kwann tunawashtua na hizi nyuzi tungekaa kimya wakaone balaa bila kuhadithiwa. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hamna mtu anayeweza muelewa Christina kwakuwa ukiitwa na Mungu Kuna vitu unatakiwa uache ..

Hata wanafunzi wa Yesu waliacha hata kazi wakamfuata Yesu...

Mambo ya Rohoni na mwilini ni tofauti kabisa...
Mama mchungaji Donatila, pitia vile vile post #528 na uisikilize mwanzo mwisho. Tina anahitaji huruma ya Mungu.
 
Ila wanaume mmepanic na Shusho!! Mbona nyie mnaachaga wanawake zenu na mnaenda kuendelea na maisha mengine lkn hatulalamiki!!! Hebu tulieni acheni kupangia wanawake maisha
Tunalo jukumu la kulinda taasisi Ndoa kwa nguvu zote ndio maana tunawasha moto kila siku hapa JF. Ninyi ndoa mnaiharibu kwa maneno na vitendo na ndio mnafaida nayo kutuliko.
 
Alivyotangaza habari za ufufuo wa Yesu...

Tena alikuwa na macho ya Rohoni...

Maana hata hao mitume wengine hawakuwa na macho ya Rohoni, ni Petro tu alimjua kuwa Yesu ni nani...

Mariam Magdalene mwanamke ambaye alikuwa wa kwanza kutanganza injili ya ufufuo wa Yesu...
Kutangaza sio hoja, je yule ndugu yake Maria aliekwenda kumwambia ameonyeshwa kuwa dada yake ni mjamzito wa Yesu, yeye alikuwa ni mtume wa kusambaza injili?

Hapa sasa naona mwanamke unataka kutupanda kichwani hebu tuambie kanisa gani unasali tukufuate tukunyooshe kiinjiri? [emoji848]
 
Back
Top Bottom