CLOUDS: Mishahara ya walimu inadhalilisha utu wao

CLOUDS: Mishahara ya walimu inadhalilisha utu wao

KILICHOBAKI MPWAYUNGU TAFUTA MUME MWALIMU AKUOE LABDA UTATULIZA SHOBO KWA WALIMU MAANA NI WAZI WE JAMAA KIPA KATOKA.
 
Sisi walimu tunafuraha na mishahara yetu ndio maana mwalimu wako wa primary mpaka leo Bado yupoo Tena Yuko fit kweli kweli ... ....

Ualimu ni kazi nzuri sana ,Haina stress ,hauzeeki kabisa ,kiufupi unaenjoy maisha kabisa ......

Kuwa na pesa kitu gani bana ,hapa dunian cha mhimu ni furahaaaaa tu ,just to be happy...hayo mengine ni kujilisha upepo ....

Walimu oyeeeeeeeeeeeeee tuchapee kaziii ndugu zangu walimuuui
Huwez kuwa naa stress wala kuzeeka reasons behind una malengo madogo maishan mwl akipata salary akaowa aka buy boda amemalza maisha ya dunian..... Hii work for tz inafiti ordinary citizens
 
Kada zingine Zina allowance kibao, food allowance, house allowance, transport allowance, nk mbali na hayo wana vikao kila wiki tena vya pesa nzuri tu. Sasa njoo Kwa walimu manina anasahihisha mitihani ya ndani bureee, anasimama bureee, mitihani ya mock mkoa na wilaya bureeee, anafundisha mpaka jumapili bureeee, hawana hata vikao navikiwepo vya SMT ni bureeee, kila kitu halambi hata sumuni
Hahaha. Hebu nitajue allowance za huko serikalini au serikali za mitaa tamisemi!!
Wewe una stress unazipunhuzia Kwa walimu wetu huna lolote!! Wahurumie wagogo wenzio ombaomba kibaaao tuache walimu wetu bwana
 
Ni kweli mkuu, tofauti yao kidogo ni ile accessibility ya posho za safari ndogo ndogo na vikao!!
Mwalimu mwenye shahada ya kwanza anayeeanza kazi huanza na 780, 000 hii inaitwa D1 . Kila baada ya miaka 3 hupanda daraja. Daraja la mwisho kabisa ni "I" ambayo ni 3.2M.

Hii mishahara siyo midogo ukilinganisha na kada zingine. Tofauti ni kwamba mwalimu hana mazingira ya kula rushwa au kupata posho zingine inje na mshahara.
Tofauti haipo kwenye posho maana siyo kweli kwamba kada nyingine ndo wanapata posho mara kwa mara. Based on allowances only, I see no any SIGNIFICANT DIFFERENCE. Tosfauti inakuja kwenye rushwa, ubadhirifu, wizi na udanganyifu!! Sasa mtu mzima na mwungwana huwezi kujisifia kazi yako eti kwa sababu inakupa fursa ya kula rushwa, ya kuiba, kufanya ubadhirifu na mambo kama hayo. Hawa kada nyingine si tunaishi nao mitaani? Hakuna tofauti kubwa kati yao na walimu, na kwanza walimu pengine wako vizuri zaidi!! Ukiangalia nyumba wanazojenga hazina tufauti kihadhi na zile wanazojenga walimu, magari wanayotembelea ni ya hadhi hiyo hiyo, shule wanazosoma watoto wao ni ya hadhi hiyo hiyo. Kuna kisa cha kweli: Mwalimu alianza ujenzi wa nyumba yake ya kuishi, majirani wakawa wanasema itakuwa anasimamia nyumba ya mtu mwingine!! Hii ni kwa sababu nyumba ilikuwa ni kubwa na nzuri sana. Hao wanaomsema hivyo wengine ni wahudumu tu ofisi mbalimbali, wengine ni maofisa utumishi vijana bado wako TSG D. Lakini yule mwalimu alikuwa kwenye ngaji ya juu TGST H, anakula zaidi ya milioni mbili kwa mwezi. Hao wanaomcheka wengine nafahamu take home yao haifiki hata laki sita!!.
Mwisho wa siku mwalimu akamaliza nyumba yake kuijenga lakini hakuhamia mapema maana alitaka afanye finishing yote kabisa!! Wakaanza kusema kama ni nyumba yake mbona hahamii si nyumba imeshakamilika? Jamaa hakuwa na haraka akafanya finishing ya kufa mtu, ilipokamilika finishing akahamia!! Watu hawakuamini kuwa nyumba ile ni ya mwalimu!! Nikasema, laiti wangejua kipato halali cha mwalimu huyo, wakalinganisha ni kipato chao, wasingethubutu kusema hayo wanayosema. Mwalimu pia si kwamba anategemea mshahara tu, kuna tuisheni kibao, lakini walimu wanafanya pia biashara kama watu wengine, wanalima mashamba nk. Huu ujinga wa kudharau walimu ifike mahali ukome!!​
 
Mpaka vyombo vya Habari vimeliona hili, walimu mjitathimini vinginevyo mtadharaulika mpaka kufa kwenu. Mnachekwa mpaka na watoto wanadai mmekuwa ombaomba kwa kuwaomba wanafunzi wawanunulie Chai muda wa break na wakisema pesa hawana mnawachapa.

Walimu wengi mnawalazimisha wanafunzi wanunue vibiashara vyenu vya ubuyu na ice-cream za ubuyu wa mia mia vibiashara ambavyo faida yake haifiki hata Buku tano.

View attachment 2632018
Yaani nakushangaa kazi ni kusimanga walimu ila huleti suluhisho katika hoja yako? Kama ma tatizo kila. Mtu anajua tupe suluhu sio kudhalilisha walimu, kwani Kuna asietaka kuwa na mshahara mzuri na marupurupu? Heshimu basi hata kama hawana uwezo wako.. Lakini Wali husika kukupa maarifa😎
 
Huwez kuwa naa stress wala kuzeeka reasons behind una malengo madogo maishan mwl akipata salary akaowa aka buy boda amemalza maisha ya dunian..... Hii work for tz inafiti ordinary citizens
Huna adabu! samahani japo huo ndio ukweli!! Una nini wewe cha kuwazidi walimu katika maisha ya leo!! Hapo hapo ulipo tembelea shule ya msingi au ya sekondari uone magari wanayotembelea walimu!! Tembelea nyumba walizojenga, tembelea miradi yao mingine wanayofanya mbali na ajira yao!! Bila shaka utaficha uso wako!! Umekariri ujinga!! walimu wamekutoa tongotongo umejua kusoma na kuandika halafu unakuja kuwadharau hapa!! Hii nchi imeshawahi kuongozwa na walimu, si mmoja, si wawili!! Wewe hapo ulipo huna cha kuwazidi walimu nina uhakika!!. Are you serious? kwamba mwalimu anaishia kununua boda? Hivi hapo ulipo hakuna shule ya sekondari au msingi uende hapo kama hutaona magari ya walimu ambayo wewe huna!! Tafadhali jifunze kuwa na adabu!!​
 
Yaani nakushangaa kazi ni kusimanga walimu ila huleti suluhisho katika hoja yako? Kama ma tatizo kila. Mtu anajua tupe suluhu sio kudhalilisha walimu, kwani Kuna asietaka kuwa na mshahara mzuri na marupurupu? Heshimu basi hata kama hawana uwezo wako.. Lakini Wali husika kukupa maarifa[emoji41]
Suluhu ni kuandamana tu wadai maslahi Yao
 
Huna adabu! samahani japo huo ndio ukweli!! Una nini wewe cha kuwazidi walimu katika maisha ya leo!! Hapo hapo ulipo tembelea shule ya msingi au ya sekondari uone magari wanayotembelea walimu!! Tembelea nyumba walizojenga, tembelea miradi yao mingine wanayofanya mbali na ajira yao!! Bila shaka utaficha uso wako!! Umekariri ujinga!! walimu wamekutoa tongotongo umejua kusoma na kuandika halafu unakuja kuwadharau hapa!! Hii nchi imeshawahi kuongozwa na walimu, si mmoja, si wawili!! Wewe hapo ulipo huna cha kuwazidi walimu nina uhakika!!. Are you serious? kwamba mwalimu anaishia kununua boda? Hivi hapo ulipo hakuna shule ya sekondari au msingi uende hapo kama hutaona magari ya walimu ambayo wewe huna!! Tafadhali jifunze kuwa na adabu!!​
Punguza mihemko
 
Mbona nao hawawalipi kabisa waandishi wao...au Ile kamati ya Tido inaongopa? Si juzi tu mpk bunge likajadili Hali ngumu ya waandishi na wanapeleka Sheria ya habari kuingiza kipengele cha maslahi ya waandishi?
 
Nina uhakika asilimia mia mshahara wa cloud hauuzidi wa mwalimu wa primary anaeanza kazi!! Primary ilakuwa laki Tano niambieni clouds wanalipwa sh ngapi!! Kama sio laki 3 !!!
Kwanza clouds wanalipa hata hiyo laki tatu? Media ziko hoi hizi hakuna kada ina tabu kama waandishi lakini wana midomo mirefu kama chuchunge..
 
Back
Top Bottom