Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu wana JF wenzangu,
Kwanza nianze kusema kwamba mimi ni miongoni mwa watanzania waliozaliwa katika familia ya maisha ya kati, sio familia tajiri wala masikini.
Pilika pilika za hapa na pale, zilinifanya nihamishie maisha yangu Kaburu ili kuweka mambo fulan sawa. Nikiwa Kaburu nimejikuta nafanya kazi na watu tofauti tofauti kutoka nchi na mabara tofauti.
Mwaka 2014 nikiwa nafanya kazi katika restaurant ya Spar (ambayo hata bongo ipo) kuna sister fulan wa kizungu alitokea kuwa rafiki yangu wa karibu (sio kiuhusiano wa mapenzi). Yule mzungu tulizoeana sana kiasi kwamba tukawa tunapeana uzoefu mbali mbali wa kimaisha, mimi nilikuwa najaribu kumchimba ili kujua ni kwanini watu wengi weupe hasa wazungu ni matajiri ukilinganisha na sisi waafrika weusi, pia na yeye alikuwa akijaribu kudodosa inakuaje waafrika wengi (weusi) ni masikini japo kuna baadhi unakuta wametokea katika familia za watu matajiri.
Sasa katika kumchimba chimba ndo siku 1 akanipa code ya mafanikio yao kimaisha, japo code hii kwa ndugu zangu wabongo ni vigumu sana kuizingatia.
Code hiyo aliyonipa ina vipengele vitano navyo ni 👇
1) MAANDALIZI:
Wenzetu huanza maandalizi ya kumuandalia mtoto maisha toka akiwa tumboni. Yani mke na mume wanapogundua kwamba katika nyumba yao kuna kijacho kinatarajia kuja baada ya mke kushika mimba, huanza maandalizi mapema ya kumtengenezea maisha kwa kuanza kuandaa mazingira ya kumfungulia mtoto ajae account yake ya bank. Hapa katika kumfungulia mtoto account ya bank kuna mawili, kuna wale ambao hufungua na kuanza kuweka hela katika account hiyo kabla mtoto hajazaliwa, na kuna wale ambao hufungua na kuanza kuweka hela baada tu ya mtoto kuzaliwa.
Na kwa vile wenzetu wamejiandaa mapema ambapo unakuta baba na mama wote wana kazi, basi account hii huanza kuwekewa pesa na wazazi wote wawili kila mwisho wa mwezi. Zoezi hili huendelea mpaka pale mtoto anapofikisha umri wa miaka 18, japo kuna baadhi wenye pesa zao huendelea mpaka pale mtoto atapokuwa na familia yake nk.
Sasa chukulia baba na mama wawe wanaweka elfu hamsini hamsini kwa kila mwezi, ina maana elfu hamsini hamsini kwa watu wawili ni laki moja, laki 1 kwa miezi 12 (mwaka) ni sawa na milioni 1 na laki 2. Hiyo milioni 1 na laki 2 ukiifanya mara 18 inakuwa milioni ishirini na moja na laki 6 (huu ni mfano tu) maana wao huweka zaidi ya hizo.
2) MALEZI:
Wenzetu pamoja na kwamba watoto wana uhuru wa kuamua jambo, lkn linapokuja swala la malezi huwa makini sana ili kuhakikisha mtoto haendi nje ya matarajio yao, na kuacha kufuata utaratibu wao.
Huu ni utaratibu ambao wameshajiwekea vizazi na vizazi, kwahiyo wazazi hufanya kila wawezalo ili kuhakikisha mtoto wao anakuwa kwenye mazingira bora na yenye kueleweka kwa faida yake na familia yake hapo baadae. Ni vigumu kwa mzungu kwenda kulewa na kurudi nyumban kulala bila kujua mtoto ameshinda wapi, na nani, amekula au hakula, anaumwa au haumwi nk.
3) ELIMU:
Wenzetu hulipa kipaumbele sana swala la elimu, tena huwa wanampa mtoto uhuru wa kuchagua kile anachopenda kusomea. Mfano mtoto anaonesha kupenda kuwa pilot wa ndege, basi wazazi wataelekeza nguvu zaidi katika hilo na ikiwezekana watampeleka katika shule ya kusomea mambo ya ndege bado mapema, waswahili tunasema 'samaki mkunje angali m'bichi', so mpaka atakapokuja kukuwa atakuwa ashafika mbali kwa kile anachojifunza.
4) USIMAMIAJI NA SUPPORT:
Mtoto anapokuwa ashakuwa na tayari ana elimu yake fulan, basi wazazi, ndugu, serikali nk vitamsimamia huyu kupata kazi kutokana na kile alichosomea. Supporter yao huwa ni kubwa na hawapumziki hadi wahakikishe lengo lao limetimia. Na alietafutiwa kazi akianza kazi huwa ni kazi kweli kweli, hakuna muda wa kukaa kwenye vikorido vya ofisi kupiga porojo mbali mbali zisizokuwa na msingi wala faida kwake.
Lakini jambo zuri kwake ni kwamba huanza kazi huku akiwa tayari ana account yake toka utotoni. Accont hiyo tayari ina zaidi ya milioni 20, so atachofanya ni kujazia zingine atazoanza kupokea kwenye mshahara wake.
5) MUENDELEZO:
Mtoto huyu au kijana huyu akishafika hapo alipofika, na yeye hufanya muendelezo kwa kizazi chake, ili kuepusha kuwa kuwa na watoto tegemezi katika familia yao/ zao.
ANGALIZO hapo chini 👇
Sasa basi, wazungu nao kama walivyo binadam wengine, na wao wana mapungufu yao. Nikimaanisha kuwa wapo wazungu ambao hawafuati hizi code kama wenzao, au wapo waliojaribu kufuata ila vizazi vyao vika fail katika hilo na kudumbukia katika umasikini, uteja, ulevi nk. Ila majority 85% ya wazungu wanaishi kwa kufuata huu mfumo wa code na unawanufaisha vizuri bila kwenda kwa shehe, mchungaji, mganga wala mtabiri.
Mimi nilipoowa na mke wangu kuzaa mtoto wa kwanza nilianza kuzifuata hizi code, nilipozaa wa pili pia nimeendelea kuzifuata hizi code tena tukishirikiana na mke wangu ambae na yeye anafanya kazi.
Japo ni changamoto kubwa kufanya mambo mengi kwa pamoja, kama vile kulipa kodi ya nyumba kila mwezi, kuwalipia watoto ada za shule kila mwezi, kununua stock ya chakula kila mwezi, kufanya shopping kila mwezi nk.
Lakini nina amini hii ndio njia bora ya kuwataharishia maisha yaliobora hapo baadae, na elimu hii nimekuwa nikiitoa kwa baadhi ya marafiki zangu, so its up to them eidha kufuata au kutofuata.
Najua kwa ndugu zetu wabongo walio wengi hii inaweza kuwa changamoto kubwa kwao, lkn kama una uwezo na nafasi ya kufanya hivi just do it now, ili uje kuokoa vizazi na vizazi vyako vitakavyokuja baada yako, sio uendekeze ulevi na kamari.
Asanteni sana.