Code alizonipa mzungu zimenisaidia kuona mwanga wa mafanikio yangu na familia yangu hapo baadaye

Tusizunguke sana.Serikali zinazojitambua na kutumia kodi za wananchi vizuri ndio chanzo cha maisha mazuri.
Serikalia inaanzia na wewe nyumban kwako.
Naomba nikupe mfano hai hapo chini πŸ‘‡
Mimi nilikuwa na mjomba wangu ambae alikuwa anafanya kazi serikalini miaka ya 90, alikuwa na cheo kikubwa kwahiyo na mshahara wake ulikuwa mkubwa ukilinganisha na wenzake wa chini yake.

Mjomba huyu wakati baada ya wenzake aliowazidi mshahara walikuwa wanajitahidi kuwasomesha watoto wao na kuwaandalia misingi bora ya maisha, yeye alikuwa anajenga heshima baa. Hakuna baada ambayo walikuwa hawamjui kuanzia magomeni, kinondoni, ilala nk. madem ndio usiseme, mke alipigana mwisho akaamua kutulia alee wanae.

Alibahatika kuzaa watoto watatu, wa kiume wawili na wa kike mmoja. Wote hakuwapa elimu inayostahili. Alikuwa akitoka asubuhi kwenda kazini anarudi saa 7 au 8 ya usiku akiwa bwii, hajui kama kuna mtoto alienda shule au hakwenda, alijisomea au hakujisomea, anaumwa au haumwi nk.

Sasa hivi kazi imesha, hana nyumba, hana kiwanja, hana chochote kama kumbu kumbu kwa kazi aliyofanya ujanani. Watoto wa kiume wamekosa muongozo wa elimu sasa mkubwa ni teja, mdogo anapiga debe. Bint kaolewa na muuza mitumba fulan ambae ndio hujitahidi kuhudumia na familia ya baba wa mke.

Je hapo tuilaumu serikali? Watoto? Baba (mjomba)? Au nani?
 
Nilikusudia kusema hivyo pia, na ubora wa njia hiyo ni kwamba kama ulifungua biashara ndogo kwa akili ya future ya mwanao utakuwa na mida wa kutosha kuisoma, kuelewa wewe binafsi, kuyajua na kuua shughulikia mapungufu ya biashara hiyo kisha unarudi kum shape mtoto wako ili aendane na mahitaji ya kiusimamizi ya biashara hiyo, Huko mbeleni yeye mwenyewe anaweza kuja kubadili mode ya biashara hiyo lakini akiwa tayari anaelewa basic and what does it meant for, atakuwa na Road map ya kumpeleka anakotakiwa kwenda, mfano wa Mr dudumizi wa kuweka angalao 100,000 kwa mwezi kwenye pig account ya mtoto imenyooka sana, imagine, kwa hesabu zake mwenyewe anaonyesha kuwa kwa miaka 18 ya uwekezaji huo mtoto atakuwa na around 21,000,000 sawa, si kiasi kidogo hata chembe, ila hela hiyo hiyo inatosha kabisa kumwaribu mwanao hadi ujutie good faith saving yako ya 18 years, na kwa age hiyo mtoto kupoteza mwelekeo ni jambo la sekunde tu kama hukumnyoosha vya kutosha.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kwa mrengo wako !!

Hizi codes kwa waTz hawa wasio na ajira na masikini wa vijijini. Wanawezaje kuzifuata ikiwa kula yao, shughuli zao etc ni za bahati nasibu ?!
Mkuu nimeshauri kwa wale wenye uwezo wa kufanya hivyo.

Maana kuna mtu ana mshahara au uwezo wa kuiandalia familia yake kesho iliyokuwa bora, lkn unakuta mtu huyo anautumia mshahara huo katika mambo ya kijinga kama vile ulevi wa kutupa, kamari, vimada nk.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kweli mkuu, baadhi yao nimeshawaona kupitia comment zao.
 
Very painful kaka.
Hii ya kulaum serikali ni excuse tunatumia wengi ila it really doesnt resolve anything.
You are the one responsible for your own life and those under your care.

Japo serikal ingetimiza wajibu wake ingekua bora zaid
 
Ya ni kweli mkuu, ila sometimes miradi nayo hufilisika na kukuacha mtupu.

Kufanya biashara kunahitaji moyo na uzoefu, sio kukurupuka tu.

Btw: fanya kile ambacho moyo wako unakushauri mkuu, kikubwa kiwe na njia nzuri kwa vizazi vyako vijavyo.
 
Kuzaa watoto wengi au wachache sio kipimo cha uduni wala ubora wa mtu.wala sio kipimo cha umasikini as long as unaweza kumudu mahitaji yao
 
-Tanzania yetu mzazi anakuambia tena shukuru unalalia godoro, sisi tu.ekua tanalalia ngozi na kula mihogo gmya kuchemshwa. Waafrika tuna mentality mbovu aisee kwani mateso na maisha uliyopitia wakati wewe mzazi unakua ni lazima na watoto wayapitie???
Usilaumu sana wazazi,inawezekana walichokupa,ndio walichokuwa nacho,
Maisha ya kibongo ni magumu sana,baba Mwalimu,mama polisi,mshahara haufiki 700K,unafikiri wataweza kukuandalia hayo yote?
Cha muhimu,ukifanikiwa kutoboa,for hook or crook,legal or illegal,weka bima ya maisha,wekeza kwa ajiri ya uzao wako,wapo wazazi wanafanya hii,unaoa,au kuolewa,Mzazi anakukabidhi nyumba hata kama haijaisha,uishi,au umalizie uishi,ufsnyie biashara maisha yaende,
Huku kwetu tuna Siasa za hovyo,mifuko ya hifadhi ya jamii,na bima ya afya ilibidi iwe kimbilio la maskini na wananchi,lakini serikali hii ya kijambazi imefilisi mifuko yote
 
Mkuu haya mambo ndio unaita code? Kweli mkuu kujua haya ndo ulisubiri kuambiwa na mzungu?

Mbona ni obvious kabisa haya
Kuyajua haya sio tatizo, tatizo ni aina ya upangiliaji wake ndio tunaita code.
 
Wananichekesha pale unapomshauri swala la kuzaa kwa mpangilio afu anakujibu kuwa kila mtoto huja na riziki yake πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Muhusika : Wewe kwenu wa ngapi

Mimi : wa 4

Muhusika : wazazi wako wangeamua kuzaa watoto watatu, wewe ungezaliwa

Mimi : Hapana lakini zama zimebadilika, mahitaji ya kulea mtoto kipindi nazaliwa na sasa ni tofauti

Muhusika : hujayajua maisha wewe, unadhani wazazi wako wangefikiria gharama wangekuzaa au unadhani enzi hizo hazikuwepo. Kwanza acha uoga wa maisha, wewe zaa tu maana hakuna mtoto atakaekufa kwa njaa akishazaliwa au asikue.
Mimi hapa nazaa hadi wote waliopo kiunoni waishe maana kila mmoja Mungu humpa ridhki yake na kwanza naweza kuzaa watoto watatu na wote wakanisahau ila yule wa tano ambaye sijamzaa ndio fungu langu

Mimi : 😷😷😷
 
Very painful kaka.
Hii ya kulaum serikali ni excuse tunatumia wengi ila it really doesnt resolve anything.
You are the one responsible for your own life and those under your care.

Japo serikal ingetimiza wajibu wake ingekua bora zaid
We can't change our government system, before we change ourselves.

Government itasimama kwa upande wa taifa, na sisi tutasimama kwa upande wa familia.
 
Kwa tz iyo code haitawezekana ata kwa mikwaju kutokan na mfumo mbovuvwa kuzaa bila ya mpangilio wenzetu wanzaa kwa mpango ndio maana izo code kwao inakua ni rahic kutekelezeka
 
Sijui Kama nnayo ongea wengine wamegusa lakin huyu Mzungu kakuficha pia baadhi ya mambo ..badala ya kuchangia account why msiweke Bima?Bima za maisha ,za elimu n.k?...kingine wazungu wanajali Sana quality ya elimu ...kumsomesha mtoto sio kumpeleka Kayumba...
 
Waswahili wanakwambia kila mtoto huja na riziki yake. Kwahiyo anajua akizaa watoto 10 atakuwa na riziki ya watoto kumi hata kama watoto hao hajawapa elimu ya kuwasaidia.

Mawazo mufilisi kabisa haya!

Idea mbaya sana mkuu imejaa kichwani mwa watz wengi hii inachangia jamii kuendelea kuwa na tegemezi wengi na lindi la umaskini
 
Hongera sana kwa kupata code za kulea watoto
Ila ukumbuke pia yafuatayo ambayo hajakuambia;
1. Mtoto wa Kizungu mzazi wake hawezi kumchapa na ukimchapa anakuitia Police (Anapiga 911)
2. ,Mtoto akifikisha miaka 18 anarusiwa kuwa na Girl friend/boy friend, kuvuta sigara na hata kunywa pombe
3. Mtoto wa kizungu ana andaliwa kujitegemea yeye na mke/mume wake pekee hakuna mambo ya extended family; na maanisha Mzazi akizeeeka anapelekwa nyumba ya wazee, na hakuna ndugu sijui mjomba nk kusumbua kuomba chochote nk
4. mtoto akishafikisha miaka 18 huna madaraka naye tena zaidi ya kumlipia ada huku akijivinjari na boy/girl friend wake nyumbani kwako

Ninachomaanisha ni kuwa
1. wanamambo mazuri hasa utaratibu wa Elimu yao wa kutambua Vipaji na kuviendeleza
Na kusomesha masomo machache ili mtu ayaelewe vizuri sio huku kwetu katoto ka darasa la nne kamebeba bagi zima la vitabu na madaftari
2. Utaratibu wa kumfungulia account mtoto pia ni mzuri kwani wakati anafika Sekondari walau una ada ya kumsomesha nk
3. Elimu yao humjengea mtoto Kujiamini na sio nidhamu ya woga kama Elimu ya huku kwetu, ambapo unaweza kukuta Mtu ana elimu ya juu kabisa ila anashindwa kusimamia ukweli kwa sabau ya woga

ILA kwa upande wa malezi KWA UJUMLA kuna namna wana BORONGA hivyo usi copy paste!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…