Code alizonipa mzungu zimenisaidia kuona mwanga wa mafanikio yangu na familia yangu hapo baadaye

Idea mbaya sana mkuu imejaa kichwani mwa watz wengi hii inachangia jamii kuendelea kuwa na tegemezi wengi na lindi la umaskini
Yah kweli mkuu, mawazo ya aina hii ndo yamesababisha watoto wa mitaani kuongezeka.

Kwa sababu wengi wanazaliwa na kukosa malezi ya wazazi.
 
Mkuu hilo la malezi nalifahamu na nimeshaliongelea kwenye namba 2.

Ukisoma kwa kutulia hiyo namb 2 utaelewa nilichomaanisha.

I mean yah ni kweli mtoto wa kizungu hauwezi kumpiga hovyo hovyo, na akifikisha umri fulan hauwezi kumpangia nini cha kufanya. Lkn uhuru huo wenzetu wanautumia vizuri ukilinganisha na sisi ambao tunajifanya hatuna uhuru huo kwa watoto wetu.

Ukichunguza aina ya tabia na heshima walizonazo watoto wa kizungu kwa wazazi wao na zile walizonazo waafrika kwa wazazi wao utaona utofauti mkubwa.

Mara ngapi tumekuwa tukisikia mtoto wa ki afrika au kitanzania kampiga, kamtukana au kamuuwa baba yake, mama yake nk. Kitu ambacho ni nadra sana kukisikia kwa watoto wa kizungu.

Kwanza hiyo sheria ya mtoto kumshitaki mzazi ingewekwa bongo leo hii kungekuwa na wazazi kibao jela wamefungwa kwa kesi za kuwachapa au kuwafokea watoto wao.

Waafrika sisi sio mkuu.
 
Japo umeongea kweli mtupu lakini hizi code kwa bongo haziwezekani.
 
Hilo suala la kuwekea watoto hela kwenye account sio wote wanaofanya hivyo na ndio sababu ya kupelekea umasikini wa kutupa kwa baadhi ya wazungu ingawa wanazaa watoto 2 tu au mmoja

Tatizo hili hata serikali ililiona na wakaamua watoto wote waliozaliwa 1/09/2002 wafunguliwe account na serikali ikatoa £250 kwa kila mtoto

Kwa hiyo wazazi wanachangia pia kila mwezi kwa hiari yao mpaka 18

Kusaidia watoto mataifa mengi wanafanya ila hata Africa wapo ila sio wengi

Hata Asians wanawasaidia sana watoto wao na kuwaonyesha njia

Waswahili ni tofauti kabisa kwani asilimia kubwa wanaamini wamefeli maisha kabla ya kujaribu

Hawana confidence na wanaona watoto kama ni adui tu wala hawaongei nao na kuwafundisha hali halisi ya maisha
 
Spar?? au Spur?
 
Yan Africa Kwa kudanganywa na mabeberu Yan hivo Vitu alivokwambia ndo unaviamin sjui Kwa nn tunaamin Sana ngoz nyeupe
 
Mengi uliyoongea hapa ni kweli mkuu, hasa kuhusu sisi waafrika.
 
Ni ujinga sana kuzaa bila kuandaa mazingira bora kwa ustawi wa maisha ya huyo mtoto anayezaliwa
Kweli mkuu sema wazee wa kiswahili wengi hawana muda wa kufikiria swala la malezi ya watoto.
Wao wanaamini mtoto hata asipokula au kusoma atakuwa tu na ataishi vizuri kutokana na riziki anayozaliwa nayo.
 
Ni kweli aisee , unakuta mzazi anafariki anaacha watoto helpless wanaishia kuwa mapanya road malezi zero ,elimu zero taflani tupu .
Wenzetu wana life insurance policy huko kwenye mashirika yao ya bima ,siku mtu ukitoka duniani hata walionyuma wanapata vibunda vya kutosha kama back up .

Haya ndio maisha bora sasa ,sio mtu anafanya kazi miaka 40+ anastaafu na kufariki hata vimafao kiduchu anavyodai anadhulumiwa na serikali , ni ujinga kabisa
 
Mengi uliyoongea hapa ni kweli mkuu, hasa kuhusu sisi waafrika.
Mzazi anakuwa adui na mtoto
Yaani mtoto akimuona baba anakimbia
Huku nako kuna kina mama wana roho mbaya kuliko shetani
Yaani mtoto anakua hajui maisha yanaendaje kutwa atalalamika sijui aanzie wapi maskini

Nawapa pole sana waliokuwa abused na bila kupewa msaada wowote kimaisha
Ndio maana kuna tofauti kati ya mwafrika na mzungu
Mzungu anaondoka nyumbani akifika 18 huku akijua maisha ya kufanya

Mwafrika anasubiri mzazi afe au amuuwe ili arithi nyumba

Maisha haya namshukuru sana Mungu na ninawaombea wazazi wangu kila saa na wanangu wananiombea vivyo hivyo
 
Kwenye code namba 4 umeitaja na serikali! Naomba uniambie hii serikali ya chama chako cha ccm ina msaada wowote ule kwa watoto kutoka kaya masikini katika kuwaendeleza kielimu.
 
Waswahili wanakwambia kila mtoto huja na riziki yake. Kwahiyo anajua akizaa watoto 10 atakuwa na riziki ya watoto kumi hata kama watoto hao hajawapa elimu ya kuwasaidia.

Mawazo mufilisi kabisa haya!

Akili muflisi ni ile inayofikiria kua binaadamu anauwezo wa kumruzuku binaadamu mwenzie wakati yeye hana uwezo wa kujiruzuku na wala hajui sekunde moja ijayo atapata nini au atapatwa na nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…