Confirmed: Waraka wa Baraza la Maaskofu Wakatoliki(TEC) wasomwa hadharani kwa waumini wote kwa makanisa yote RC Tanzania nzima

Niko hapa kuthibitisha hilo pasi na chembe ya shaka yoyote leo nimehudhuria ibada ya misa takatifu katika kanisa la St Joseph Cathedral Dar.

Waraka umesomwa kwa waumini wote, na kupitia reliable source ya Jesuits agent amenithibitishia makanisa yote na vigango vyote vya kanisa katoliki Tanzania nzima wamesomewa waraka huo leo.

Pascal Mayalla unajisikiaje kwa kuikana imani kwa sababu ya vipande 30 vya fedha?

Mama Samia anakwenda kuwaabisha wanafki na machawa wote, kesho asubuhi Rais anapewa brief na DG wa usalama wa Taifa
reaction ya Taifa baada ya waraka wa TEC na Rais anakwenda kulihutubia Taifa, watch n see, lisipotokea hili JF wanipige life ban.

Roma Locuta, Causa Finita Est.
Halafu waraka umetoa na ushauri pia kwa waanzilishi wake.
 
Watu waovu wanajipanga kutetea Uovu wao Kwa mbinu Zote.
Hii nchi SIO Mali ya MTU mmoja Wala Kikundi cha watu . Tena watu wenye tamaa ya kujilimbikizia Mali.

Haiwezekani MTU mmoja apewe bandari Zote za nchi Hii Ili akusanye pesa apeleke Dubai .

Noo. Yaani hasara tunazopata kwenye Madini,wanyama , Ardhi, viwanda vilivyogeuzwa kuwa magodauni ya Wahindi na Waarabu tuendelee nayo Karne Tena eti Kisa Wapumbavu WATAKUJA na hoja za Dini kwenye Mali za Tanganyika . Bandari inaendeshwa na Serikali na SIO kanisa Wala Misikiti Sasa wanajadili mkataba mbovu Kwa misingi ya Dini ya Mwekezaji wananufaikaje na Dini yake Kama SIO kutumika Kwa manufaa ya Wachache.

Je, Sheria na Katiba iliyotumika kupitisha na kusaini mkataba huo mbovu ni Sheria za Dini ipi?
Kwa Nini watu wanaingia dini Badala ya hoja inayohusu mapungufu.?

Mbona Rais mwenyewe aliwahi kusema hadharani kuwa yeye sio mtaalamu Wa Kila Kitu Hivyo wasaidizi wake wamsaidie na anawategemea wasije wakamwangusha!!

Ni wazi wasaidizi wake wamemwangusha kwenye hili Suala la DPW. Lakini sio hilo tu wamemwangusha sana kwenye Suala la fedha.
Matumizi ya Serikali ni mabaya sana .
Wizi ni mkubwa mno!
Kubebana kumekua Kama desturi ya wezi.
JPM alipofariki watu walikausha fedha Zote na kumdanganya mama kuwa hapakua na pesa. Magufuli alijua kuzikusanya pesa na kuzisimamia Kwa ukali. Hawa wasaidizi wake Kwa Sasa wanawaza kujilimbikizia Mali Kwa hataka bila kujali. Wamemwingiza mama chaka.
Wanatumia nguvu kuficha Uovu wao . Bahati nzuri Kanisa Katoliki ndio Msingi Wa taaluma papote Duniani. kanisa Katoliki linaongozwa na Wasomi waliopinukia na wasiosubiria Teuzi za Ikulu . Hivyo wanasimamia Haki kweli na utaalamu walionao bila kuangalia maslahi ya MTU mmoja au kakikundi kadogo kalikojigeuza Kuwa miungu wasiokosea Wala kukosolewa.

Msingi Wa Haki na tawala Zote Duniani ni Mungu na SIO kakikundi Ka watu wachache Kwa sababu ya utajiri wao.

Anayetaka kuuza nchi asubiri uchaguzi ujao aombe kura Ili akauze nchi. Kwa Sasa hakuna aliyepata ruksa ya kuuza nchi kutoka Kwa Wananchi mana hakuna aliyepigiwa kura na Wananchi .
Aliyechaguliwa na Wananchi alikua ni JPM na alikataa kuuza Mali za Wananchi Kiholela .

Katiba ilindwa na SIO Dini ya MTU . Katiba inatoa mamlaka Kwa viongozi Hivyo waiheshimu sana.
 
Spika wa Bunge Akson Tulia akiwa ametulia tuliii akisikiliza kwa makini Waraka wa TEC kanisani leo asubuhi

Mbaya zaidi na Waraka kapewa kaupokea kisha kausogeza pembeni hapo
 
Attachments

  • IMG-20230820-WA0009.jpg
    IMG-20230820-WA0009.jpg
    33.2 KB · Views: 1
Nimefuatilia Youtube live nimesikia likisomwa Katoliki Moshi ambako kulikuwa na kuapishwa/kusimikwa kama sikosei kwa Paroko katika mojawapo ya Kanisa na hata Tanga pia nineona waraka umesomwa,

hili ni jambo jema pale mnapokuwa na jambo la maslahi ya Kitaifa basi lifikishwe kwa waamini kwa njia ya amani kupitia majukwaa ya imani tofauti na mihadhara ya kisiasa ili nao waweze kulitafakari na kutambua hali halisi
 
Niko hapa kuthibitisha hilo pasi na chembe ya shaka yoyote leo nimehudhuria ibada ya misa takatifu katika kanisa la St Joseph Cathedral Dar.

Waraka umesomwa kwa waumini wote, na kupitia reliable source ya Jesuits agent amenithibitishia makanisa yote na vigango vyote vya kanisa katoliki Tanzania nzima wamesomewa waraka huo leo.

Pascal Mayalla unajisikiaje kwa kuikana imani kwa sababu ya vipande 30 vya fedha?

Mama Samia anakwenda kuwaabisha wanafki na machawa wote, kesho asubuhi Rais anapewa brief na DG wa usalama wa Taifa
reaction ya Taifa baada ya waraka wa TEC na Rais anakwenda kulihutubia Taifa, watch n see, lisipotokea hili JF wanipige life ban.

Roma Locuta, Causa Finita Est.
Am waitin' for it
 
HAIWEZEKANI KUWATENGA VIONGOZI WA KANISA NA SIASA ZA NCHI YAO!

Wapendwa Watanzania!
Limekuwa ni jambo la kawaida kwa watawala au watu walio karibu na watawala wa Tanzania wakibanwa na viongozi wa dini hasa maaskofu huanza kutoa maneno ya propaganda dhidi ya viongozi wa dini wakiwaambia 'wasichanganye dini na siasa'. Msemo huu wanautumia kama kichaka cha kujifichia wasiguswe na viongozi wa dini!

Kauli hizo zimeibuka tena kwa kishindo zaidi kuanzia mwezi Juni 2023 baada ya maaskofu kuingilia sakata la Mkataba wa Bandari. Hivi karibuni tuliikemea Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilipoitisha mkutano wa viongozi wa vyama vya siasa ili kujadili hoja ya viongozi wa dini kuonekana wakiwa na viongozi wa vyama vya siasa.

Tumeona ni wajibu wetu ili kuwaelimisha watu kuhusu suala hili kusudi wasije wakapotoshwa na wanasiasa katika suala zima la kudai haki katika taifa lao. Wanasiasa ni wajanja sana na wanajua nafasi na nguvu ya viongozi wa dini katika jamii ndio maana wanatumia nguvu ili kupotosha ukweli kuhusu nafasi ya viongozi wa dini katika ukombozi wa kifikra katika taifa.

Tunapenda kukiri kuwa hili tunaloliandika ndilo eneo ambalo sisi tuna ubobezi nalo, kwa hiyo hatubahatishi bali tunakiandika tunachokijua, tulichokisomea na kukifundisha katika ngazi za Chuo Kikuu.

Kwa upande wa Wakristo, chimbuko la dini hiyo ni mji wa Yerusalemu, Israeli ya Kale. Lakini, ni vizuri watu wakaelewa kuwa Ukristo una mizizi yake miaka 5000 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Hivyo, msingi mkubwa wa mafundisho ya Ukristo ni Biblia Takatifu yenye sehemu kuu mbili - Agano Jipya na Agano la Kale.

Dini haifanywi kwa wanyama na wala siasa pia haifanywi kwa ndege. Dini ni mfumo mzima wa maisha ambao ndani yake kuna mambo mengi. Tunaposoma au kufundisha kuhusu dini lazima tusome maisha ya jamii nzima ambayo kwanza dini ilifika kwayo. Kwa upande wa Wakristo, sisi tunasoma kuhusu jamii mbalimbali kama Misri, Syria, Ukaldayo (Babeli), Rumi, Wagiriki, Jordan, Waisraeli, Waajemi, Waarabu, Lebanon, nk.

Katika kusoma na kujifunza dini tunafundisha waumini kuishi kwa mifano ya jamii hizo ikiwa ni pamoja na kuiga mema na kuyaacha mabaya na hayo yanawezekana tu kwa kusoma kuhusu maisha yao kupitia viongozi au manabii wao.

Tunaposoma na kujifunza Biblia tunakutana na mambo yafuatayo:
1. Familia (family institutions): familia, ndoa, watoto, wajane, urithi, kifo, maziko, nafasi ya wanawake katika jamii, nk

2. Taasisi za Kiraia (Civili institutions): idadi ya watu, utumwa, taasisi ya kifalme, familia za kifalme, utawala, ajira na uchumi, kilimo, Afya na tiba, sheria na haki, mgawanyo wa muda, vipimo vya uzito, mahakama, nk.

3. Taasisi za Kijeshi (military institutions): majeshi ya Israeli, ngome za kijeshi, mbinu za kivita, siraha za kivita, vita, vita vitakatifu, nk

4. Taasisi za dini (Religious institutions): ibada, madhabahu, nyumba za ibada, uongozi wa taasisi za dini, Ofisi ya Ukuhani, Ofisi ya Walawi, sadaka, imani potofu, uchawi, utaratibu wa ibada, siku za ibada, sherehe na siku za sikukuu, nk.

Watu waliokuwa juu ya yote hayo ni viongozi wa dini na ndio waliopewa majukumu ya kuifundisha na kuionya jamii. Taasisi hizo ziliwekwa kwa ajili ya watu na kilichotofautisha ni ratiba. Wakati wa vita walipigana na wakati wa amani watu hao walifanya sherehe. Wakati wa mambo mazito ikiwemo kujua mustakabari wa nchi walikwenda kutafuta ushauri kwa viongozi wa dini. Alipotokea kiongozi mkorofi au jeuri alikemewa na viongozi wa dini au hata kutangaziwa kuondolewa madarakani na hao viongozi wa dini.

Sisi Askofu Mwamakula tunaitoa kwenu elimu hii ili msiyumbishwe ili muelewe kuwa viongozi wa dini kuingilia kati mtafaruku wa kisiasa au kiutawala ni ishara kuwa jamii yenu iko na afya!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 20 Agosti 2023; 12:35 jioni.
 
Nimesikiliza Radio Vatican wameusoma vizur sana kwakweli, nadhani Radio maria, radio Tumaini, radio mbiu nakadhalika watakua wameusoma vizur zaidi 🌹
 
Nyundo juu ya nyundo
 
Niko hapa kuthibitisha hilo pasi na chembe ya shaka yoyote leo nimehudhuria ibada ya misa takatifu katika kanisa la St Joseph Cathedral Dar.

Waraka umesomwa kwa waumini wote, na kupitia reliable source ya Jesuits agent amenithibitishia makanisa yote na vigango vyote vya kanisa katoliki Tanzania nzima wamesomewa waraka huo leo.

Pascal Mayalla unajisikiaje kwa kuikana imani kwa sababu ya vipande 30 vya fedha?

Mama Samia anakwenda kuwaabisha wanafki na machawa wote, kesho asubuhi Rais anapewa brief na DG wa usalama wa Taifa
reaction ya Taifa baada ya waraka wa TEC na Rais anakwenda kulihutubia Taifa, watch n see, lisipotokea hili JF wanipige life ban.

Roma Locuta, Causa Finita Est.
Itasaidia nini boss?

Mkataba upo pale pale na hivi ruling ya court imesema hakuna hoja za msingi za kukwamisha mkataba kuendelea basi hiyo ni green light kwa serikali kuendelea na taratibu zingine za mkataba.

TEC sio chochote mbele ya amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama nchi hii.

Katiba ya nchi inampa mamlaka makubwa mno Rais kwahiyo ni busara ya Rais tu imuongoze otherwise ana mamlaka ya kutenda jambo lolote hata liwe kinyume na katiba na hashtakiwi awapo madarakani ama anapostaafu.
 
Kuhusu faida za mkataba huo naweza kuwa na wasiwasi. Lakini kanisa la katoriki kutoa tamko kuhusu jambo lenye maslahi mapana ya taifa lina nipa wasiwasi zaidi. Vp ikiwa kundi lingine la kiimani na kidini likitoa tamko ambalo pengine likakinzana na tamko la kanisa katoriki, je nchi itakuwa katika hali gani?
Hebu tufikirie kwa mlengo huo. Tamko linalotoka kwa taasisi fulani ya kidini, ina maana ni tamko la wanataasisi hiyo, je ni lini kanisa la katoliki lilifanya white paper process ya kupata maoni ya wakatoliki wote mpaka wafikie hitimisho la kuwa mkataba huo haufai kwa niaba ya kanisa?
Nashauri, tukiwa kama nchi, tusioneshe mfano mbaya kwa kulinyamazia suala hili. Maana hili likifumbiwa macho, watakuja na mambo makubwa zaidi ambayo kama nchi yanaweza kutugawa wananchi kwa misingi ya imani zetu.

Binafsi nasema. "NAPINGA KITENDO CHA KANISA LA KATOLIKI KUTOA TAMKO LINALOPINGA MKATABA KATI YA TANZANIA NA DPW."
WAJUE CHOMBO CHAO NI KWA AJILI YA KUWALEA WAKATOLIKI KIIMANI. HIYO NI TAASISI YA KIROHO, SIYO TAASISI YA HARAKATI. KAMA WANATAKA IWE HIVYO WAENDE KWA KABIDHI WASIHI MKUU , KUBADILISHA USAJILI WAO.

NB: SIUNGI MKONO MIKATABA ISIYO NA TIJA KWA TAIFA.
Watoe,tutapima pumba na mchele
 
Roma ikiongea, ni Amri na ndio sauti ya mwisho.
Jidanganyeni na ukubwa ambao kiuhalisia haupo.

Uhalisia ni kwamba kila imani ina nguvu yake kulingana na eneo fulani ila kwa nchi hii hakuna imani yenye nguvu kuzidi nyingine ndo maana unaona hata uongozi wa nchi akitoka muislamu anaingia mkiristo.

Tena waislamu wanaonekana wana nguvu kubwa kuliko upande wowote wa dini nchi hii maana Rais anaweza kuwa Muislamu na makamu wake akawa muislam vile vile na hii imetokea kwa Kikwete na Sheini na pia kwa Kikwete na Bilal.

Lakini haitatokea nchi hii Rais akawa mkiristo na makamu wa Rais akawa mkiristo pia.

Sasa kwa muktadha huu uislamu una nguvu kubwa isiyoonekana kwa macho ya kawaida ila tu hawana show off za kijinga.
 
Jidanganye hii , first move Bado Kuna plan nyingine hiyo ni hatari zaidi

Kiufupi , Samia 2025 hatuko naye kama Mgombea

Imeshapitishwa Sasa ni utekelezaji tu
Teh teh teh...

Aise huko mnapodanganywa hamnaga hata akili ya kuhoji tu?

Rais wa nchi hii hakuna wa kumpinga awapo madarakani na ikionekana kuna kimbelembele anaweka kiwingu amaweza kufanyiwa lolote akazimwa na ikawa imeisha kihivyo.
 
Itasaidia nini boss?

Mkataba upo pale pale na hivi ruling ya court imesema hakuna hoja za msingi za kukwamisha mkataba kuendelea basi hiyo ni green light kwa serikali kuendelea na taratibu zingine za mkataba.

TEC sio chochote mbele ya amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama nchi hii.

Katiba ya nchi inampa mamlaka makubwa mno Rais kwahiyo ni busara ya Rais tu imuongoze otherwise ana mamlaka ya kutenda jambo lolote hata liwe kinyume na katiba na hashtakiwi awapo madarakani ama anapostaafu.
Ktk maswala ya kiimani, kitu chochote unacho kiona kibaya,unatakiwa ukikemee na ukiongee,so hata kesho kikitokea unakuwa hauna hatia mbele za Mungu na hiyo ndio ilikiwa kazi ya mitume.

Kazi yao ilikuwa kuhubiri,so kama haujafuata mahubiri yao hilo swala lako, ila wao wanakuwa wametimiza wajibu wao na hawana hatia mbele za Mungu.

Maskofu wametimiza wajibu wao wa kiutume, so serikali kutosikia au kusikia walicho kiongea hilo ni swala ni lao.Ila wao maaskofu wametimiza part yao kama mitume.

Kumbuka ndani ya kanisa kuna mapadre na maskofu wenye uweledi katika nyanja mbalimbali.Mule kuna main jinsia,madaktari, wahasibu, maIT,wanasheria nk,tena kuna wengine ni maprofesa, wengine wanaPhD,masters ndio zipo za kumwaga,degree ndio husiseme,so wanacho kiongea hawaja bahatisha.

Cha msingi hoja zijibiwe kwa hoja,mkataba haukuandikwa na malaika,bali mwanadamu serikali inaweza ikaamua (kama ikitaka) na kuyafanyia kazi mapungufu.Ila maskofu washatimiza wajibu wao wa kiiutume.
 
Jidanganyeni na ukubwa ambao kiuhalisia haupo.

Uhalisia ni kwamba kila imani ina nguvu yake kulingana na eneo fulani ila kwa nchi hii hakuna imani yenye nguvu kuzidi nyingine ndo maana unaona hata uongozi wa nchi akitoka muislamu anaingia mkiristo.

Tena waislamu wanaonekana wana nguvu kubwa kuliko upande wowote wa dini nchi hii maana Rais anaweza kuwa Muislamu na makamu wake akawa muislam vile vile na hii imetokea kwa Kikwete na Sheini na pia kwa Kikwete na Bilal.

Lakini haitatokea nchi hii Rais akawa mkiristo na makamu wa Rais akawa mkiristo pia.

Sasa kwa muktadha huu uislamu una nguvu kubwa isiyoonekana kwa macho ya kawaida ila tu hawana show off za kijinga.
Kwa Waraka wa Kanisa Katoliki uliosomwa leo Kanisani kiukweli kabisa pasipo kuwa na ushabiki ni Waraka uliosomwa na watu wenye weledi wa hali ya Juu sana na misumari imekazwa vibaya mno! Mpaka watu wasio na Elimu kabisa wameelewa. Sasa kama serikali itashupaza Shingo ikapitisha kwa mabavu basi wajiandae mpasuko mkubwa sana ndani ya Serikali na Chama na 2025 ccm ijiandae kukabidhi nchi kwa Chama kingine.
 
ni sawa na kikundi kidogo kilivyotuletea huu mkataba haikubariki, usisahau hili.

Uko sahihi. Maana ni ty way traffic.
Lakini binafsi nampongeza rais Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu mjadala mpana na wa wazi kuhusu suala hili.
 
Back
Top Bottom