#COVID19 Corona iko maeneo gani Tanzania?

Kuusema ukweli, huku mtaani hamna mwenye time kama kuna kitu kinaitwa Corona. Huo ndio ukweri (kwa sauti ya nanii).
Mfano mimi nikija huku jf ndio naona ona mambo ya korona.., ila huku street watu hawana habari
 
Kwa sasa inapiga zaidi viunga vya chato

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo kipindi cha nyuma watu walikua hawafariki, acha uzwazwa.
 
Hapa nilipo, njoo uione
 
Aiseee yaani hadi mama akawaambia wasaidizi wake tokeni tokeni bado unasema ni suspect?? Uzuri mama afichi anatangaza wazi kwamba hali ni mbaya.
Mkuu si tunazungumzia ile clip? hakuna haja ya kuniona mimi mbishi wewe nenda kaitizame tena ile clip na kusikiliza vizuri, Mama kaambiwa wale ni wenye matatizo ya kupumua ila yeye ndio kataka kuambiwa kuwa ni covid ndipo akajibiwa ndio covid ila jamaa akamalizia kuwa ni suspect.

Mama Samia kama anasema hali mbaya basi ni kwa maneno tu ila vitendo hali ni tofauti ndio maana juzi tu kaenda kuangalia mechi ya simba na yanga, sasa kama hali mbaya hadi tunaona Mitungi ya gesi kama yote inakuaje Rais anaenda kubariki mikusanyiko kama ile ya kwenye mechi ya simba na yanga?
 
Umeshawahi kusikia mtu wako wa karibu amelazwa hospitali kwa tatizo la upumuaji? Nauliza kwa wema tu mkuu...maana na mimi nachanganyikiwa
Kipi kinakuchanganya mkuu?
 
Kwa ajili ya kuwaelimisha MATAGA maana wao bila uthibitisho huwa ni wabishi Sana. Korona iwatembelee tu kama yule Sir God wao mbishi na mjuaji. Kichwa kikadakwa
Kwani nyumbu hawana korona? Au hawapati korona?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…