DustBin
JF-Expert Member
- Jun 3, 2021
- 609
- 604
Kuusema ukweli, huku mtaani hamna mwenye time kama kuna kitu kinaitwa Corona. Huo ndio ukweri (kwa sauti ya nanii).Hey,
Nawasalimu kwa Jina la Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania.
Hivi majuzi juzi tumesikia taarifa lukuki kuhusu corona. Wengine nimesikia wanasema kwa sasa hili ni wimbi sijui la tatu — Wengine wanaita sijui DELTA kitu gani gani??
Majina yamekuwa mengi kidogo. Kuna DELTA na kuna wimbi.
Kiuhalisia huku Buza nilipo, hatujui hata maana ya corona. Achana na hayo sijui ma-DELTA na manini nini mengine.
Tunajiachia vibaya sana. Hakuna cha barakoa wala sanitaiza. Na tuko fiti ajabu.
Haya makorona ya DELTA huwa nayasikia kwenye magazeti na majarida tu. Mtaani hakuna cha DELTA wala bibi yake na DELTA.
Sasa hawa wajuvi wa corona wanasemaje kuhusu hili? Hiyo DELTA iko wapi hasa hapa nchini?
Maana inawezekana mimi niko Buza huku, kumbe hiyo DELTA imejificha njombe!
Wananchi tunavurugwa. Mtaani hatuoni cha DELTA wala nini, lakini usiku kucha Televisheni zote zinazungumzia DELTA.
Which is which? Tuamini TV ama tuamini uhalisia tunaouona mtaani?
Mnatuchanganya mjue?
Mfano mimi nikija huku jf ndio naona ona mambo ya korona.., ila huku street watu hawana habari