Makanisa yamekimbiwa sasa huwa tunakusanyika kufanya nini?...Poleni na majukumu ya hapa na pale sasa na kale yanayowafanya msilale, niende moja kwa moja kwenye mada husika.
Kama kweli maombi yanafanya kazi kwa namna ambayo tunaaminishwa, kwanini viongozi wa dini wameungana kutekeleza agizo la kuvunja mirundamano ikiwemo mijumuiko ya kiibada ili kuikwepa korona?
Kama walifanya maombi kwa lengo la kuizuia corona isiingie nchini, lakini tunaona corona imeingia, nini kinachokufanya uwaamini kua maombi ya sasa wanayojipanga kuyafanya yataitokomeza corona mazima?
Haya mambo probably si magumu ila ugumu tunauweka sisi kwa kuweka mizaha kwa kutumia kivuli cha dini.
Hivi mfano hawa madaktari wetu na sekta ya afya kiujumla wangejumuika kwenye maombi kwa kuamini kwamba maombi ni njia madhubuti ya kutatua matatizo kama haya katika kila janga la ugonjwa. Kama ambavyo watu wa dini wamekua wakituhimiza kufanya, je tungefanikisha kutibu gonjwa lipi kwa maombi?
Ngoma inaingia tanzania wabongo tulijitia wachamungu sana kua tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n'ge hivyo ukimwi kwetu sio tishio.
Lakini tunachokiona mpaka saizi mapasta na masheikh wanachukua vidonge kwa siri sana. Lakini pamoja na hayo hatuwaoni wakijisalimisha kua wameshindwa kudhibiti ukimwi kwa maombi yao.
Mungu ambaye tunamtolea sadaka kila siku halafu katika matatizo kama haya kajichimbia tu wala hatuoni juhudi zake, huyu si mungu wakuabudiwa. Ni sawa na rafiki mnafki ambaye kwenye matanuzi mkiwa viwanja mnakua naye karibu sana halafu ikatokea siku umeishiwa anakukimbia.
Wahubiri wanahubiri huku wamevaa face mask at the same time wanasema damu ya yesu ni tiba ya kila kitu. What a joke but i ain't laughing?
Tunaambiwa ukiwa na imani waweza kuamisha hadi milima lakini sikutegemea kuona vatican, mekka ziwe kipaumbele kukataza watu wasiende kwao kwa hofu ya korona.
Mungu muweza wa yote yuko wapi mbona kawasusia msala madaktari wetu halafu yeye amesizi tu eti mpaka aamshwe kwa maombi?
Kwanini mungu mjuzi wa yote na muweza wa yote ahitaji maombi?
Mbona kwenye zile hadithi za gharika na sodoma na gomora huyu mungu ali-respond haraka sana kwanini asifanye hivyo kwenye janga hili linalomaliza ndugu zetu na kudhoofisha hali ya uchumi wetu?
Hivi kweli mungu huyu yupo kweli? Maana viongozi wetu wa dini nao wanaathirika mpaka inafikia hatua italy makanisa yameshehena maiti inamaana yeye haoni?
Kwanini Mungu ahitaji maombi yetu ili aweze ku-solve matatizo yetu, ilihali anaelewa hitaji la moyo wetu hata kabla hatujasema?
====
Chukua tahadhari kwa kufuata angalizo lililotolewa na mamlaka ya afya Corona haidhibitiwi kwa maombi bali kwa kuepuka makatazo ambayo yameainishwa na shirika la afya
Halafu wakiwa madhabahuni wanatuhubiria uongoHawa wanaojiita manabii wanatumia hela zetu kujiwekea mabodigadi na kununua mahammer.
Ona sasa mwingine huyu
Yani matatizo yanayoua ndugu zetu ikiwemo wachungaji na mashehe ndio njia madhubuti ya kuonesha ukuu wa mungu?
ukweli ni mmoja tu either Mungu yupo, au hayupo. Ikiwa hayupo, wale wanaoamini uwepo wake hawatopata hasara yoyote. Ila kama yupo na yale anayoahidi baada ya kufa yapo , wasioamini watakuwaje? It is just a matter of thinking, ila Mungu yupo haijalishi watu wanakubali au wanapinga!!!Ukweli mchungu
mi naamini corona na ukimwi is God invention sasa angalia Dar huko eti wanaume wanajiuza kama wanawake na sehemu nyingine duniani
Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu aliweka principles na anafanya Kazi kwa principles.
Huwezi kuwa na njaa halafu unaomba muujiza ushibe bila kula.Lazima kifanyike kitu ili chakula kionekane
Vivyo hivyo kwa magonjwa.Mungu amekupa akili uitumie na siyo mahali unapoweza kutumia akili ya kawaida uombe muujiza.Chumba choo, kitumie vizuri ili usipate kipindupindu.Sasa wewe unaenda kujichamba bila kunawa halafu unashika vyombo vya ndani ukiugua kipindu pindu unamlaumu nani?
Mwisho Mungu usimchukulie poa ndugu yangu unless wewe ni devil worshiper.Kama we ni mtu wa kawaida tu,ujue devil mwenyewe anamwogopa na kutetemeka.Anaweza kukushughulikia tu ili ajipendekeze kwa tabia yako ya kumdharau Mungu.
Tubu na nyenyekea kwa Mungu na acha kuangalia udhaifu wa watu wengine jiangalie wewe mwenyewe
Sent using Jamii Forums mobile app
J2 hii naskia kina ibada ya kuvunja corna kanisani kwa mbunge mama rwakatare.Mitume na manabii wao wapo hapa specially kutupatia pesa,maisha mazuri na safari za ulaya
Sent using Jamii Forums mobile app
Unajuaje kua dini yako hiyo hiyo ya kikristu sio utapeli?Haya sasa ndiyo madhara ya kuchanganya DINI, SIASA, UTAPELI, SAYANSI, HALF-KNOWLDGE na PREJUDICE.
Katika ukristu, sote tunajua kuna matepeli wengi, wanaotumia jina la Yesu kuishi mjini, kuwafanya wengine mazoba ili wao wapige dili, na hawa wameuumiza ukristu kwa sehem kubwa. Wanapaswa kulaumiwa sababu hawamuhubiri Yesu wa msalaba ila Yesu wa Harusini kana, wao ukristu ni kupata utajari, kupona magonjwa yote, kuishi kama uko peponi ilihali uko duniani.
Jibu rahisi tu ni kwamba hata Yesu mwenyewe, hakuponya wagonjwa wote aliokutana nao, aliponya wale tu ambao uponyaji wao unahusika moja kwa moja na lengo lake kuja duniani, ambalo ni kuokoa roho (na mwili akitaka Yesu, ila sio kwa kuamrishwa na mwanadamu)
Lengo la Yesu na Ukristu, sio kumfanya mwanadamu astarehe duniani, bali mwanadamu atambue maisha ya duniani kama matayarisho ya maisha ya umilele, hili ndilo lililomleta Yesu duniani, na ndiyo kwa mfano kanisa katoliki linafundisha.
Unadhani kwa nini wamisionari walikuja na dini mkono wa kulia na shule/hospitali mkono wa kushoto? je kuna wamisonari wa kikatoliki walikuja na kusema acheni hospitali njooni tuwaombee mpone?
Mungu anasikia kilio chetu na anaweza kutuponya kwa muujiza Corona endapo akitaka, sisi tunafunga na kusali kumuonesha haja na hitaji letu, japo analijua lakini ameshasema OMBENI NANYI MTAPEWA, BISHENI NANYI MTAFUNGULIWA....hakusema simama mlangoni, nitafungua kwa kuwa ninajua unataka kuingia!!!!
Tutumie utashi wetu wa kibinadamu, ambao ni zawadi ya Mungu, kukwepa corona, na tumuombe Mungu atuepushe na Corona kwa namna zile ambazo ziko nje ya uwezo wetu kama wanadamu, ila tusatake kumfanya Mungu shemeji yetu kuwa aje sasa aponeshe Corona ndo awe Mungu kweli.
Nawaambia hivi, hata Mungu akishuka leo hii akaponesha Corona dunia nzima, hamtamwamini, sababu Corona sio kipimo cha uwezo na mamlaka ya Mungu, Mungu hapimwi kwa uwezo wake wa kuponya Corona
Una hoja dhaifu sana.mbona yashawahi kupita magonjwa makubwa corona cha mtoto.watu walikufa na dawa ikapatikana,maisha yakaendelea..corona ni ugonjwa kama magonjwa mengine..sioni sababu yakukashifu dini.
corona ipo na itaondoka itabaki story.corona iuwe iwezavyo haiwezi fikia maleria na ambayo dawa zake zipo zakila aina na zinajulikana na inauwa kila siku.mbona hamzisemi dini?.corona ni gonjwa la mlipuko limekuja litaondoka maisha yataendelea.
Ndio ujue HAKUNA MUNGU hapo! Ni fix tu za kale tulizolishwa na mapadri.
Ukiambiwa dawa ya corona imepatikana na ili ukubali kua inafanya kazi kweli inabidi uaminiInafurahisha mtu ambaye humwamin Mungu kutaka kuhakikishiwa kama yupo .hicho ni kituko kwa sababu step ya kwanza unatakiwa umwamin Mungu yupo nje ya hapo huwez kumwamin wala kumwelewa
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha ila we jamaa banaMtu usipokiwa mwangalifu dini ni kama ulevi ...unaweza hata kuteleza familia ukahamia kwenye mwenye kutangaza dini..
Yesu Kristo bwana wetu alionya sana kwamba tuwe waangalifu mno...sababu hao pia wataweza kutumia jina lake na kuponya & kuhamisha milima, kunena kwa lugha nk
Tuseme tu ni mengi ambayo ni hatari yanayoweza kutokea kutokana na mikusanyikoMakanisa yamekimbiwa sasa huwa tunakusanyika kufanya nini?...
Au ndo tunaendekeza kutojali afya ... Je ni corona tu ndo hatari ktk mikusanyiko?
Atakuambia mungu anajibu maombi kwa wakati wakeMtu kila siku utamsikia anasema "nimeongea na Mungu", sasa huyo Mungu unawasiliana nae ameshindwa kusema chochote kuhusu corona?
Kumbe ww unaona kwamba uwepo wa Mungu ni "dhana"????Hapana
Principle zilikuwepo kabla hata dhana ya mungu haijaumbwa. Principles ndizo zilizopelekea dhana ya mungu kuwepo.
Mungu ni mjuzi wa yote, muweza wa yote na mwenye upendo wote. Hiyo ndiyo principle yake karibia dini zote zinakubalina na hii dhana
Katika huu ulimwengu wenye njaa na magonjwa yasioyotibika pamoja na mabalaa mengine yakutisha huoni kwamba yanapingana na hizi dhana za huyu mungu?
Kwanini mungu hakuumba ulimwengu ambao haupingani na principles zake?
Kama yeye mwenye uwezo wote,ujuzi wote na upendo wote kashindwa kuuweka ulimwengu usipingane na principles zake kwanini aone rahisi kwa sisi kufuata principles alizoziweka ilihali anajua kua sisi ni wadhaifu?
It's Scars
ukweli ni mmoja tu either Mungu yupo, au hayupo. Ikiwa hayupo, wale wanaoamini uwepo wake hawatopata hasara yoyote. Ila kama yupo na yale anayoahidi baada ya kufa yapo , wasioamini watakuwaje? It is just a matter of thinking, ila Mungu yupo haijalishi watu wanakubali au wanapinga!!!