Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Hivi hua bado kuna watu wanajadili kuhisu hadithi za mungu na shetani?

Mungu hayupo, kitu kinaitwa mungu hakipo.
 
ukweli ni mmoja tu either Mungu yupo, au hayupo. Ikiwa hayupo, wale wanaoamini uwepo wake hawatopata hasara yoyote. Ila kama yupo na yale anayoahidi baada ya kufa yapo , wasioamini watakuwaje? It is just a matter of thinking, ila Mungu yupo haijalishi watu wanakubali au wanapinga!!!

Wasioamini,kuwa Mungu yupo,watakapokufa watasamehewa kama Yesu alivyomsamehe Thomas
 
Uliwahi kwenda huko wanakosema yupo ukamkosa?
Hiyo sehemu yenyewe unayodai kua yupo, unaweza kuthibitisha ipo?

Utakubali kila kitu utachoambiwa kua ni cha kweli kwasababu huna uwezo wa kwenda kuhakikisha ili ujithitishie ukweli?

Nikikuambia katikati ya jua kuna chupa ya chai ambayo inazunguka, utahitaji kwenda angani ili kuthibitisha hayo madai kua ni kweli?

Utakubali kua chupa hiyo ya chai ipo kweli kati kati ya jua kwasababu huna uwezo wa kwenda huko angani?

It's Scars
 
Unahitaji, uvuvio wa roho Mtakatifu kulijua fumbo la utatu Mtakatifu vinginevyo utaambulia hewa Kama ulivyo Sasa.

Nakupongeza Sasa kwa kuanza Kumtambua Mungu wa kweli.

Waislam, Wakristo na Wayahudi hawa wanamuabudi Mungu Mmoja Muweza wa Yote.

Ambaye hata ww unamuabudu pia.

Sihitaji uvuvio wa chochote

Nahitaji majibu ya maswali yangu

Waislamu na wakristo hawaabudu mungu mmoja na ndio maana wote hao pepo zao zinapingana.

Mungu wa wakristo kaahidi kuimba na kusifu kwa wataofika peponi, wakati Allah kaahidi bikra 72 kwa wataofika peponi

Allah karuhusu wake wanne, Yehova kapiga ban hilo agizo na yeyote atayefanya hivyo basi hataiona pepo.

Mwisho kabisa mimi siabudu Mungu yeyote na wala hakuna sehemu ambayo nimeandika maneno kama hayo

It's Scars
 
Matatizo ya akili yapo ya aina nyingi hata wewe unaweza kuwa na matatizo ya akili bila kujua japokuwa unajiona mzima na unafanya shughuli zako kama kawaida,sasa mimi nimezungumzia matatizo ya majini/mapepo kama ambavyo wengi tunaamini hivyo ila wataalamu wa magonjwa ya akili wanatuambia hayo matatizo ni magonjwa tu ya akili hivyo ni kinyume na sie tunaoamini kuwa matatizo husababishwa na majini.
Sasa kama wataalamu wanakuambia kua hayo ni matatizo ya akili na sio majini wala mapepo kwa kutumia taaluma zao na vipimo vyao, wewe usiye na taaluma umejuaje kua hayo ni majini?

Unaweza kuthibitisha hilo?


Ndiyo nasema hayo matatizo ya akili(majini/mapepo) tunaona hutibiwa kwa dua na watu hupona au kupata nafuu hapelekwi hospitali.
Unajuje kua watu wanatibiwa kwa dua na sio kua ni mchezo wanaoufanya masheikh ili kuwakamata maboya wakati wenye taaluma zao juu ya hili tatizo walisema sio majini wala mapepo kama ambavyo mnaongopewa?


Kuna siku kwenye daladala binti mmoja alipatwa na hilo tatizo na kuanza kufanya fujo akanikosa ngumi ya uso,ikabidi wanaume tumshike kumzuia maana angeumiza watu na hata yeye pia angeweza kujiumiza na alikuwa na nguvu kwa hali ya kawaida asingekuwa na nguvu kiasi kile.
Kukoswa ngumi ya uso na mwanamke kwenye daladala ndio kunathibitisha kua majini na mapepo ni ugonjwa wa akili?

Sasa kama alikukosa ngumi ya uso lakini bado mawazo yako yamekua mgando kama mtu akiyepigwa na kitu kizito kichwani, vipi kama ile ngumi ingekupata ungekua katika hali gani saizi?

Personal experiences zingine zimekaa ki-wack sana

Hayo ndiyo matatizo nayozungumzia ambayo hayapelekwi milembe wala hospitali zetu hizi.
Thibitisha kwanza hayo magonjwa yanasababishwa na majini/mapepo na sio religion drama

It's Scars
 
Quran21:35 " Kila nafsi itaonja umauti, na tunakujaribuni kwa mitihani ya shari na kheri, na kwetu sisi mtarejea"

Magonjwa kama Corona ni miongoni mwa mambo ya shari tuliyopatiwa walimwengu kama aya inavyoeleza hapo juu, ni katika majaribu ya Allah juu ya viumbe wake, anafanya atakalo juu ya viumbe wake.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu maombi ndio tunamuomba sana Mwenyezi Mungu Ili atuondoshee haya maradhi.Kuondosha au kutoondosha ni utashi wake, na kama ataamua kuondosha basi hapangiwi na yoyote muda wa kuondosha huu ugonjwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo sehemu yenyewe unayodai kua yupo, unaweza kuthibitisha ipo?

Utakubali kila kitu utachoambiwa kua ni cha kweli kwasababu huna uwezo wa kwenda kuhakikisha ili ujithitishie ukweli?

Nikikuambia katikati ya jua kuna chupa ya chai ambayo inazunguka, utahitaji kwenda angani ili kuthibitisha hayo madai kua ni kweli?

Utakubali kua chupa hiyo ya chai ipo kweli kati kati ya jua kwasababu huna uwezo wa kwenda huko angani?

It's Scars
Umejibu swali au ndio umeeleza nini sasa?nini ulichotaka nikielewe kwenye haya maelezo.
 
Sasa kama wataalamu wanakuambia kua hayo ni matatizo ya akili na sio majini wala mapepo kwa kutumia taaluma zao na vipimo vyao, wewe usiye na taaluma umejuaje kua hayo ni majini?

Unaweza kuthibitisha hilo?



Unajuje kua watu wanatibiwa kwa dua na sio kua ni mchezo wanaoufanya masheikh ili kuwakamata maboya wakati wenye taaluma zao juu ya hili tatizo walisema sio majini wala mapepo kama ambavyo mnaongopewa?



Kukoswa ngumi ya uso na mwanamke kwenye daladala ndio kunathibitisha kua majini na mapepo ni ugonjwa wa akili?

Sasa kama alikukosa ngumi ya uso lakini bado mawazo yako yamekua mgando kama mtu akiyepigwa na kitu kizito kichwani, vipi kama ile ngumi ingekupata ungekua katika hali gani saizi?

Personal experiences zingine zimekaa ki-wack sana


Thibitisha kwanza hayo magonjwa yanasababishwa na majini/mapepo na sio religion drama

It's Scars
Point ni tiba ya hayo matatizo,na nimeeleza kuwa dua hutibu hayo matatizo na hatuoni wenye matatizo hayo kupelekwa hospitali.
Na nimezungumzia dua si suala la masheikh maana dua hawaombi masheikh tu.
 
Poleni na majukumu ya hapa na pale sasa na kale yanayowafanya msilale, niende moja kwa moja kwenye mada husika.

Kama kweli maombi yanafanya kazi kwa namna ambayo tunaaminishwa, kwanini viongozi wa dini wameungana kutekeleza agizo la kuvunja mirundamano ikiwemo mijumuiko ya kiibada ili kuikwepa korona?

Kama walifanya maombi kwa lengo la kuizuia corona isiingie nchini, lakini tunaona corona imeingia, nini kinachokufanya uwaamini kua maombi ya sasa wanayojipanga kuyafanya yataitokomeza corona mazima?

Haya mambo probably si magumu ila ugumu tunauweka sisi kwa kuweka mizaha kwa kutumia kivuli cha dini.

Hivi mfano hawa madaktari wetu na sekta ya afya kiujumla wangejumuika kwenye maombi kwa kuamini kwamba maombi ni njia madhubuti ya kutatua matatizo kama haya katika kila janga la ugonjwa. Kama ambavyo watu wa dini wamekua wakituhimiza kufanya, je tungefanikisha kutibu gonjwa lipi kwa maombi?

Ngoma inaingia tanzania wabongo tulijitia wachamungu sana kua tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n'ge hivyo ukimwi kwetu sio tishio.

Lakini tunachokiona mpaka saizi mapasta na masheikh wanachukua vidonge kwa siri sana. Lakini pamoja na hayo hatuwaoni wakijisalimisha kua wameshindwa kudhibiti ukimwi kwa maombi yao.

Mungu ambaye tunamtolea sadaka kila siku halafu katika matatizo kama haya kajichimbia tu wala hatuoni juhudi zake, huyu si mungu wakuabudiwa. Ni sawa na rafiki mnafki ambaye kwenye matanuzi mkiwa viwanja mnakua naye karibu sana halafu ikatokea siku umeishiwa anakukimbia.

Wahubiri wanahubiri huku wamevaa face mask at the same time wanasema damu ya yesu ni tiba ya kila kitu. What a joke but i ain't laughing?

Tunaambiwa ukiwa na imani waweza kuamisha hadi milima lakini sikutegemea kuona vatican, mekka ziwe kipaumbele kukataza watu wasiende kwao kwa hofu ya korona.

Mungu muweza wa yote yuko wapi mbona kawasusia msala madaktari wetu halafu yeye amesizi tu eti mpaka aamshwe kwa maombi?

Kwanini mungu mjuzi wa yote na muweza wa yote ahitaji maombi?

Mbona kwenye zile hadithi za gharika na sodoma na gomora huyu mungu ali-respond haraka sana kwanini asifanye hivyo kwenye janga hili linalomaliza ndugu zetu na kudhoofisha hali ya uchumi wetu?

Hivi kweli mungu huyu yupo kweli? Maana viongozi wetu wa dini nao wanaathirika mpaka inafikia hatua italy makanisa yameshehena maiti inamaana yeye haoni?

Kwanini Mungu ahitaji maombi yetu ili aweze ku-solve matatizo yetu, ilihali anaelewa hitaji la moyo wetu hata kabla hatujasema?

====

Chukua tahadhari kwa kufuata angalizo lililotolewa na mamlaka ya afya Corona haidhibitiwi kwa maombi bali kwa kuepuka makatazo ambayo yameainishwa na shirika la afya
Mwache Mungu aitwe Mungu, na atabaki kuwa Mungu, yeye hujibu kwa wakati wake, Mungu hajaribiwi, ipo siku hizi kauli zako utazitubia mbele za Mungu
 
Acha upotoshaji kijana

Imani ingekua inaponya kama wewe unavyotuaminisha hapa basi tusingeona vatican na mekka wakipiga marufuku watu kwenda kuhiji kwao kwa kuogopa corona wakati wakijua kabisa kua ukiwa na imani unapona

It's Scars
Wangepiga ban kwenda kwa Mungu ndio tungeshangaa.
 
Magonjwa yalikuwepo tangu zamani, kuna gonjwa liliua watu milioni 50 ndani ya miaka miwili, corona cha mtoto
 
Back
Top Bottom