Kwahiyo kwa mfano wake ndiyo kufanana ? Birika lina mkono,kwani mkono wako ni sawa na mkono wa birika ?Pia kumbuka ni hiyo hiyo Qur'an inayosema Allah amemuumba adam kwa mfano wake, je unaipinga?
Aya iko wazi na maana zote mbili zinafanya kazi. Hizi ni maana za hiyo aya.
1. Kwa mfano wake yaani kwa umbile lake mwanadamu ambalo ni maalumu na ajabu au zuri sana. Kama vile katika lugha mtu akisema "Daah nimekutana na mtu wa mfano wake",yaani asiye na mfano. Ndiyo maana aya iliposema Allah ameumba mja kwa mfano wake yaani kwa dhati maalumu ya mwanadamu isiyo fanana na viumbe wengine.
2. Kadhalika husemwa maana hiyo ya aya ni kuwa mwanadamu ana baadhi ya sifa kama za Allah,yaani mwanadamu ana huruma na Allah ana huruma ili huruma ya Allah ni kamili.
Kitu kingine,nakushauri ni kuwa wewe Mola humjui,lakini unamkana ndiyo maana siku zote unakuwa huna hoja zaidi ya kubisha na kupoteza muda.
Ni kazi sana kujadiliana na mtu kama wewe ambaye hujui kwanini unamkana Mola na hujui hilo wazo la kumkana Mola limekujaje zaidi dhana,na kutumia misingi dhaifu ya "Logic", ambayo haiwezi kujitetea yenyewe.