Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Pia kumbuka ni hiyo hiyo Qur'an inayosema Allah amemuumba adam kwa mfano wake, je unaipinga?
Kwahiyo kwa mfano wake ndiyo kufanana ? Birika lina mkono,kwani mkono wako ni sawa na mkono wa birika ?

Aya iko wazi na maana zote mbili zinafanya kazi. Hizi ni maana za hiyo aya.

1. Kwa mfano wake yaani kwa umbile lake mwanadamu ambalo ni maalumu na ajabu au zuri sana. Kama vile katika lugha mtu akisema "Daah nimekutana na mtu wa mfano wake",yaani asiye na mfano. Ndiyo maana aya iliposema Allah ameumba mja kwa mfano wake yaani kwa dhati maalumu ya mwanadamu isiyo fanana na viumbe wengine.

2. Kadhalika husemwa maana hiyo ya aya ni kuwa mwanadamu ana baadhi ya sifa kama za Allah,yaani mwanadamu ana huruma na Allah ana huruma ili huruma ya Allah ni kamili.

Kitu kingine,nakushauri ni kuwa wewe Mola humjui,lakini unamkana ndiyo maana siku zote unakuwa huna hoja zaidi ya kubisha na kupoteza muda.

Ni kazi sana kujadiliana na mtu kama wewe ambaye hujui kwanini unamkana Mola na hujui hilo wazo la kumkana Mola limekujaje zaidi dhana,na kutumia misingi dhaifu ya "Logic", ambayo haiwezi kujitetea yenyewe.
 
Mungu sio complicated hivyo ila hizi Abrahamic religions ndo majanga tupu!!! Manabii na Makuhani fake!! [emoji16]
 
Yupo, Wapo, Kipo kilichutuumba sisi na vilivyomo

Ila Dini zimejaa upotoshaji
 
sihitaji kusoma dini yako ili nibishe kua mafundisho hayo ni uongo, ni kama vile ambavyo wewe huhitaji kusoma dini zote ili upate sababu ya kusema uislam ni dini ya kweli kuliko zingine
Kwahiyo wewe kazi yako ni kubisha na si kujenga hoja,ndiyo maana huwa huna hoja katika ukanushaji wako juu yakutokuwepo kwa Mola.

Sasa atasomaje Dini zote wakati Uislamu ni dini ya kweli,maana yake anaruhusu kuitumia akili yake vibaya.

Ila wewe ni wajibu wako kujifunza Qur'aan au Uislamu kama ukitaka kuujua ukweli. Hapa kuna tofauti kubwa sana.Usipende kulinganisha vitu visivyo fanana,kisa mbwa ni mnyama,mbwa ana miguu minne,basi wanyama wote wana miguu minne. Kuhoji huku ni kuhoji kitoto na ni ishara ya ugonjwa wa akili.

Kila siku tunawaambia hawako sawa wenye akili na wasio kuwa na akili,wema na waovu bali wenye elimu na wasio kuwa na elimu.
 
Ndio maana Karl marx alipinga sana mambo ya dini . If at all God exist is he really omnipitent and benevolent ? If he is benevolent he cannot be omnipotent and if he is omnipotent he cannot be benevolent .

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo kwa mfano wake ndiyo kufanana ? Birika lina mkono,kwani mkono wako ni sawa na mkono wa birika ?

Aya iko wazi na maana zote mbili zinafanya kazi. Hizi ni maana za hiyo aya.

1. Kwa mfano wake yaani kwa umbile lake mwanadamu ambalo ni maalumu na ajabu au zuri sana. Kama vile katika lugha mtu akisema "Daah nimekutana na mtu wa mfano wake",yaani asiye na mfano. Ndiyo maana aya iliposema Allah ameumba mja kwa mfano wake yaani kwa dhati maalumu ya mwanadamu isiyo fanana na viumbe wengine.

2. Kadhalika husemwa maana hiyo ya aya ni kuwa mwanadamu ana baadhi ya sifa kama za Allah,yaani mwanadamu ana huruma na Allah ana huruma ili huruma ya Allah ni kamili.

Kitu kingine,nakushauri ni kuwa wewe Mola humjui,lakini unamkana ndiyo maana siku zote unakuwa huna hoja zaidi ya kubisha na kupoteza muda.

Ni kazi sana kujadiliana na mtu kama wewe ambaye hujui kwanini unamkana Mola na hujui hilo wazo la kumkana Mola limekujaje zaidi dhana,na kutumia misingi dhaifu ya "Logic", ambayo haiwezi kujitetea yenyewe.
Sijajua unaposema hakuna wakufanana naye hua unaangalia factor gani. Sijajua ni vigezo gani ambavyo mungu ako navyo unavyotaka kuvikuta kwa mtu?

Kwa jinsi ulivyoeleza hapo unajiweka kwenye angle ya kukataa kila kitu, utajikuta hakuna kitu chochote kinachoweza kufananishwa na kingine endapo tu kutakuwa na mppishano au utofauti baina ya viwili hivyo
 
Kwahiyo wewe kazi yako ni kubisha na si kujenga hoja,ndiyo maana huwa huna hoja katika ukanushaji wako juu yakutokuwepo kwa Mola.

Sasa atasomaje Dini zote wakati Uislamu ni dini ya kweli,maana yake anaruhusu kuitumia akili yake vibaya.

Ila wewe ni wajibu wako kujifunza Qur'aan au Uislamu kama ukitaka kuujua ukweli. Hapa kuna tofauti kubwa sana.Usipende kulinganisha vitu visivyo fanana,kisa mbwa ni mnyama,mbwa ana miguu minne,basi wanyama wote wana miguu minne. Kuhoji huku ni kuhoji kitoto na ni ishara ya ugonjwa wa akili.

Kila siku tunawaambia hawako sawa wenye akili na wasio kuwa na akili,wema na waovu bali wenye elimu na wasio kuwa na elimu.
Duniani kuna zaidi ya dini 10,000, Mpaka umeona uislamu ni dini ya kweli kuliko zingine niambie umesoma dini ngapi?
 
Again this shows your ignorance... Unapata je ujasiri wa kubisha kitu kama hujakisoma na kukielewa ? Isn't that stupidity ?
Una uhakika gani kama sijasoma hzo dini zengine ?
Moja kati ya maajabu ya Qur'an ni kwamba imeandikwa kwa lugha ya mafumbo.. Hivyo Allah alivyosema katika hiyo aya hajamaanisha kwamba anafanana kama mwanadamu,, nahitaji darsa kukuelezea hili,, ndo maana nakwambia shida yenu mnabisha vitu pasipo kuelewa..
Hapo juu nimeweka list ya miungu (kwa uchache) inayoabudiwa na dini tofauti tofauti, kwasababu umekiri uislam ni ini ya kweli nataka unithibitishie hilo kwa kuthibitisha kila mungu wa hizo dini hapo juu kua ni wa uongo

Kama unakiri Qura'n imeandikwa kwa lugha ya mafumbo unajuaje ulichokitafsiri ndio maana halisi iliyokusudiwa?

Kwanza ili kitu flani kionekane kimefanana na kingine ni factor gani zinazoangaliwa?

Kwasababu kama kwako ili kitu kiwe na mfanano na kingine kinapaswa kumatch kwa 100% na kingine basi kwa point hiyo utakua sahihi kusema mungu hafanani na binadamu.

Ni sawa na mtu aseme nyumba A imefanana na nyumba B halafu uje umpinge kua haijafanana kwakua nyumba A rangi yake ya paa ni tofauti na nyumba B. Kwamba ulitaka kila kitu kutoka nyumba A kifanane na nyumba B ndio ukubali kua zinafanana
 
Kwani kuna kiumbe gani wa kumfananisha na binadamu? Binadamu huyo ambaye Mola amempa akili kuliko viumbe wote hapa duniani !!
Ebu nitajie!!
Unatafsiri vipi na kutofautisha kujua hiki kimefanana na kile?

Criteria gani unazotumia kujua?

Naweza kukuambia binadamu kafanana na nyani ukanipinga kwa kusema nyani ana manyoa mengi

Kwa fact hiyo hata binadamu hakuna wa kumfananisha na binadamu mwenzake kwasababu hata utofauti wa fingerprints na DNA unatosha kuhitimisha kua binadamu hawafanani
 
hua unaangalia factor gani. Sijajua ni vigezo gani ambavyo mungu ako navyo unavyotaka kuvikuta kwa mtu?
Nimekuuliza birika lina mkono je mkono wa birika ni saea na wako ?

Sasa unapouliza vigezo wakati ushaambiwa hafanani na chochote,hilo ni swali la uongo.
Kwa jinsi ulivyoeleza hapo unajiweka kwenye angle ya kukataa kila kitu, utajikuta hakuna kitu chochote kinachoweza kufananishwa na kingine endapo tu kutakuwa na mppishano au utofauti baina ya viwili hivyo
Hili ni dai ambalo liko dhidi na kile nilichokiandika na unazua uongo kwa jambo ambalo halipo. Kuna vitu vinafanana na kuna makosa ya kulinganisha visivyo fanana ukavifanya kuwa sawa,ndiyo maana nikakwambia hawafanani wenye akili na wasio na akili. Hapa hujaelewa wapi ? Jitahidi ukiwa unasoma ninachokiandika kisome na ukielewe.

Kitu kimoja kwa kingine kinaweza kisiwe sawa katika elimu lakini kika lingana kwenye mali. Unachotakiwa kuwa makini ni kujaribu kuvifanya vikawa sawa vile ambavyo haviko sawa.

Ngoja nikuulize swali,hivi huwezi kujenga hoja bila dhana ?
 
Duniani kuna zaidi ya dini 10,000, Mpaka umeona uislamu ni dini ya kweli kuliko zingine niambie umesoma dini ngapi?
Unarudia swali ambalo nilishakujibu katika mada nyingine na nikakupa kitabu yaani marejeo ukasome,sasa huwa nashangaa unaporudia jambo ambalo lilishajibiwa kitambo.

Hilo jambo la kwanza,lakini jambo la pili,ni kuwa hakuna anaeweza kuukosoa Uislamu sababu ni dini ya haki,na ni dini iliyo jengeka katika elimu na uhalisia. Sasa kama una shaka na uislamu jenga hoja au ukosoe.
 
Wewe ndio umechanganyikwa kabisa.Hujui mbele wala nyuma ni wapi.
MODS Paw, Moderator, Fang na wengine, hii mada irekebisheni kichwa cha habari. badala ya dini muweke madhehebu. Tangu kuumbwa kwa ulimwengu magonjwa yamekuwepo na hata matatizo mengine kama njaa na vimbunga na matetemeko. Dini zimekuwepo nyakati zote hizi sambamba na haya matatizo. Sasa anaibuka mtu mmoja mwenye mihemko kusema dini zimeshindwa kukabiliana na corona ambayo ni janga la majuzi. Ikiwezekana pia mada hii ifutwe kwani pia inakoelekea siko
 
Of

Ofcourse God is omnipotent and benevolent.... Why do you say that if he is omnipotent then he can't be benevolent, and if he is benevolent he cannot be omnipotent ? Give me an example to justify / clarify your claim
Mfano ni huu

Mungu yupo

Mungu huyu ni omnipotent, omnibenevolent na pia ni omniscient

Omnipotent: ana nguvu ya kuzuia maovu yasiweze kutokea

omnibenevolent: ana upendo wote na mwenye utayari wa kuzuia mabaya

Omniscient: Mwenye ujuzi wote wa kuelewa ni njia gani uovu unaweza ukapenya, na mwenye kujua ni njia gani ambayo inaweza kuzuia huo uovu

Mungu mwenye kujua njia zote ambazo dhambi na maovu yanaweza yakaja kutokea, Mungu mwenye uwezo wa kuzuia hayo yote yasiwepo, mwenye kila sababu ya kufanya hivyo angezuia maovu yasiwepo.

Kama kungekua na Mungu mwenye ujuzi wote, upendo wote na muweza wa yote basi uovu usingekuwepo

Uovu upo. Hiyo inamaanisha hauwezi kuwa na vyote viwili kwa mpigo (contraiction) yani kuwepo na uovu halafu at the same time kuwe na Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na muweza wa yote

Uovu unathibitisha Mungu huyo hayupo
 
Kumbe hata haujui,, sio kazi yangu kukufundisha.. Hilo ni jukumu lako kusoma na kutafuta kujua kwanini hzo dini zengine ni za uongo..

Nina uhakika wa nilichotafsiri kwasababu nimesoma dini,, nimesoma tafsiri ya Qur'an naelewa,,pia sio kazi yangu kukufundisha, ni jukumu lako kusoma!!

Narudia kukuelewesha,, Allah alivyosema amemuumba Adam kwa mfano wake, hajamaanisha kwamba yeye ( Allah) anafanana na Adam,, hapana, sio hivyo, ina maana tofauti ambaye mtu kama ww huwezi kuelewa,, nenda kasome kwanza ndo uje kupinga..

Mfano wako sio relevant
Kwahiyo wewe umesema dini zingine ni za uongo kwa mujibu wa maelezo ya watu uliyosikia nasio kwamba ulisoma mwenyewe ukahakikisha na ukauona huo uongo?

Ukiendelea kusema unauhakika bila kuweka vivid proof kupinga hoja yangu utakua hujafanya lolote kwasababu utakua upo kwenye "madai" nasio "uthibitisho" madai ambayo hata mimi pia naweza kusema bila kuwa na uthibitisho

Unazidi kukosea kusisitiza kua unanielewesha wakati hujaniambia ni kivipi unauhakika na majibu yako kua ni sahihi wakati ujumbe ulioandikwa hapo ni cypher.
 
Kwani wewe unatafsiri vp kujua kwamba hiki kimefanana na kile ?

Binadamu ameumbwa kwa mfano wake ( unique),, hilo ndo linaloongelewa,, usikwepe mada kwa kutoa mifano isiyohusiana
Lete fact kupinga hilo sio porojo tu
kwa hiyo wewe ulikua unanipinga tu kuwa hakuna wakufanana na Allah ilihali hujui criteria zinazozingatiwa katika kujua vitu vinavyofanana?

Mimi tafsiri nayoijua ndio hiyo uliyoipinga.

Narudia kuuliza tena swali hili

Unatafsiri vipi na kutofautisha kujua hiki kimefanana na kile?

Naweza kukuambia binadamu kafanana na nyani ukanipinga kwa kusema nyani ana manyoa mengi, hivyo nyani hafanani na binadamu

Kwa fact hiyo hata binadamu hakuna wa kumfananisha na binadamu mwenzake kwasababu hata utofauti wa fingerprints na DNA unatosha kuhitimisha kua binadamu hawafanani
 
Unarudia swali ambalo nilishakujibu katika mada nyingine na nikakupa kitabu yaani marejeo ukasome,sasa huwa nashangaa unaporudia jambo ambalo lilishajibiwa kitambo.

Hilo jambo la kwanza,lakini jambo la pili,ni kuwa hakuna anaeweza kuukosoa Uislamu sababu ni dini ya haki,na ni dini iliyo jengeka katika elimu na uhalisia. Sasa kama una shaka na uislamu jenga hoja au ukosoe.
Ukiona swali limejirudia ujue mjadala nao umejirudia

Ukiona mjadala umejirudia maana yake majibu yako hayakukata kiu la swali

Duniani kuna zaidi ya dini 10,000, Mpaka umeona uislamu ni dini ya kweli kuliko zingine niambie umesoma dini ngapi?
 
Uovu upo kwasababu Mwenyezi Mungu ametupa free will,, uwezo wa kuchagua kufanya mazuri au mabaya..

Hivyo kama mtu umeamua kufanya ubaya ni kwasababu umeamua wewe ( your free will),, lakini haimaanishi kwamba Mungu hawezi kuepusha hilo..

Na kuna sababu kuhusu kutokea hilo... Tatizo lenu hamsomi kuelewa,, mnabisha tu
freewill nayo ni hadithi inahitaji mjadala wake kuelezea kimapana zaidi

Kwani haiwezekani kuwa na freewill yenye kuhusisha mazuri pasipo uovu?

kama haiwezekani basi Mungu si muweza wa yote
 
Pia hakuna anayeweza kuikosoa Qur'an,,
Hii inaonesha dhahiri Uislamu ndio dini ya haki.

Kuna maandiko katika Qur'an zaidi ya miaka 1400 iliyopita inaeleza sayansi,, wanasayansi ndo wamekuja kugundua juzi tu.. Hii inaonesha dhahiri kuwa Qur'an ni maandiko ya Allah kupitia mjumbe wake Muhammad ( SAW)
Kwani swala la kukosolewa lipo katika makubaliano kua ili ionekane mtu kaikosoa Qura'n ni mpaka waislamu wakubali kua imekosolewa?

Kama ni ishu ya kukiri, basi sio tu uislam bali hakuna dini yeyote iliyoweza kukosolewa na kukiri kua imepotoka na kuikubali dini nyingine

Ila kama kuikosoa ni kunakuja kwa kuhoji kweli wa hicho kitabu basi hata mimi nimekuwa nikifanya hivyo na hata hapa naweza nikarudia tena

Kabla ya kuangalia Qura'n inaweza kukosolewa au lah nataka uniambie unajuaje Qura'n imeongea ukweli?
 
Wapi nimesema kwamba nimesikia kwa watu kwamba hzo dini zengine ni za uongo ?

Unataka nikupe vivid proof gani sasa ? Nimekwambia tafsiri ya hiyo ayah imeelezwa katika vitabu vya tafsiri,, na maana yake haikuwa kama ulivolenga wewe..

Jenga hoja !!
that was my assumption kwasababu ulininyima ushirikiano kwa kunipa directly answer

Kama hukujua kwa njia hiyo ndo utueleze sasa

Kumbuka ulisema kama hujasoma dini, basi hustahili kusema dini ni ya uongo.

Duniani kuna zaidi ya dini 10,000, Mpaka umeona uislamu ni dini ya kweli kuliko zingine niambie umesoma dini ngapi?
 
Back
Top Bottom