Hata kuisoma tu hotuba iliyoandikwa kwa mashine kwa "font size 24" Mzee Magufuli anashindwa kusoma kwa ufasaha!!
Tatizo ni nini??
Pamoja na kukosa "fluency", nimefurahishwa na jambo moja, kukwoti mstari wa Neno la Mungu kutoka Biblia Takatifu....
Hata hivyo naomba kumshauri ndg Magufuli kuwa, aanze yeye na Makonda wake " kuacha njia mbaya (maovu) yao" ili tunapomwomba Mungu kuponya nchi yetu, aone ukweli huo toka ndani ya moyo was kiongozi mkuu wa nchi.....
Na hii ikiwa ni pamoja na kukifuta mara moja kikosi kazi chao cha kuteka, kuumiza na kuua watu wanaowadhania kuwa wanatishia maslahi yao ya kisiasa....
Kusema tu kwa mdomo huku matendo yao yakisema kitu tofauti, ni unafiki na haina maana yoyote zaidi tu kwamba tunazidi kumdhihaki Mungu muumba wetu...!!