Corona Virus: Rais Magufuli ahutubia Taifa - Machi 22, 2020 - Wagonjwa Tanzania wafikia 12

Corona Virus: Rais Magufuli ahutubia Taifa - Machi 22, 2020 - Wagonjwa Tanzania wafikia 12

Ningemuelewa rais angehimiza swala la usafi, kunawa mikono, kusafisha vitasa nya milango, meza na viti hasa baada ya matumizi. Kuepuka kusalimiana. Sasa tunahimizwa tupige kazi kama vile hakuna janga.
Sasa utakula hilo janga manka!
 
Baadhi ya hatua tunazochukua leo tulipaswa kuzichukua kabla ingesaidia sana kama hiyo ya watu kuwekwa kwenye karantini kwa siku 14 kwa gharama zao.

Anaeshauri baadhi ya mikusanyo kama Ibada haiepukiki, sijui kama yuko sahihi kwani wenzetu wamefikia hatua ya kuingia kwenye lockdown baada ya hali kuwa mbaya..

Tuogpe dini zetu, sio waumini wa dini hizo na viongozi wao hata kama ni wengi kiasi gani.
Hivi wewe sehemu kama hospital unaweza kuwanyima watu kwenda? Vitu vingine sivyo vya kuiga. Mazingira ya nchi yetu ni tofauti na Ulaya. Maisha asilimia kubwa yanaendeshwa kwa mikusanyiko. Ukizuia kila kitu kwa muda hata wa wiki moja watu watakula nini?
 
Mkuu umeongea kwa hisia sana. Haya ni mawazo yangu pia. Hapa nilipo nimejikuta najilaumu sana kwa kitendo changu cha jana jioni kwenda mahali kulikokuwa na mkusanyiko wa watu. Najuta sana.

Siamini kama tunachukua tahadhari kwa kiwango kinachotakiwa. Najiuliza kama nchi za wenzetu wamefikia hatua ya kushindwa kujua wafanye nini itakuwaje kwa sisi hohehahe?

Na hili wazo la nchi za joto....kuanzia Mei tutakuwa tunaelekea kwenye msimu wa baridi kwenye maeneo mengi ya nchi yetu na kama hivi ndio tunazidi kushuhudia kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa itakuwaje?

Ole wetu! G Sam,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kila nikipita humu najikuta nataka kutokwa na machozi, Mungu epushia mbali hili baa asee!
 
Anasema tuombe mungu tusitishane.Kwa kuwa corona haijamuuwa mtu hata mmoja nchini

Sent using Jamii Forums mobile app
mi mwenyewe kwa hili nipo pamoja na rais, wagonjwa wote ni raia wa kigeni kuna haja gani ya kupanic sasa
ugonjwa upo toka last year hakuna mtanzania hata mmoja aliyepata tofauti na hawa waliokuja juzi, sasa kuna haja gani ya panic?
ivi lakini inakuaje ugonjwa upo toka mwaka jana leo hii ndo unaingia?
ina maana mda wote huo raia wa kigeni walikua hawaingii nchini?
 
Namuona Putin pia wala hana habari na corona
Tupo wengi
Adjustments.jpg



Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Salary Slip,
"Salary Slip, wewe JPM kila anachosema wewe unatafuta makosa tu- kweli huwa hana zuri hata moja. Any way ni rahisi kuwa mkosowaji kuliko kuwa mtendaji
 
Kwa kiasi kikubwa Pascal Mayalla huwa ana habari za uhakika na zenye uchambuzi kulinganisha na wengi wetu, hata kama humpendi mkubali kakuzidi. Over

Hakuna mahali nimelinganisha kati ya yeye na mimi, nilichozungumza ni ile hali ya ninyi kumwona kama yeye ni authority.

Kwamba anachokisema mnaona kama hakitakiwi kukosewa.

Sijawahi kumpenda wala kumchukia, namchukulia kama member wengine tu humu, na ninachokisoma kwake lazima nikithibitishe mahali kama inawezekana.
 
Back
Top Bottom