Kwa nchi nyingi za Africa, huyu covid-19 tulikuwa tunaweza kumthibiti kwa "containment measures" tu. Kama kufunga mipaka ni gharama sana, tungeweza kuweka watu wote wanaoingia (irrespective of their source areas) katika "14 days mandatory quarantine". Maana shida inayoonekana kwetu ni kupitia watu wanaoingia nchini. Ila sijui hasa Serikali yetu inawaza nini kwa kweli, inatengeneza bomu.
Watu humu ndani wanapiga tu kelele "tuchukue hatua wenyewe". Kwenye kesi kama hii huwezi iacha Serikali pembeni, ndiyo maana ya uwepo wa Serikali, ifanye "intervention" kwenye mambo kama haya. Binadamu wanatofautiana mitazamo.
Hakuna jambo linaloweza kuwafanya wote waliitikie kwa namna moja, kama watapewa uhuru wa kuamua (ndiyo maana tunaweka taratibu/sheria na mamlaka za kusimamia).
Kwa hili, Serikali ya Tanzania inatusaliti kuchukua hatua kwenye jambo muhimu. Hayo mapato wanayoyafikiria hayatatusaidia hata kidogo pale hili janga likifumuka na kuwa "serious". Hatuwezi kufikia pato la Italy, South Korea, Iran, nk, na tunaona jinsi covid-19 inavyowachachafya.