Taarifa ya Ummy ina kasoro na haijitoshelezi, au kuna upindishaji wa maksudi.
Mgonjwa aliingia nchini, akapimwa joto uwanja wa ndege KIA akaonekana yupo vizuri, akaruhusiwa kuondoka, tena bila ya maelekezo yoyote ya kumfuatilia.
Mgonjwa, hakupokelewa na ndugu au jamaa yeyote hapo uwanjani, kwa hiyo kaamua mwenyewe kwenda hotelini? Alisafiri vipi toka hapo uwanja wa ndege hadi hotelini?
Utashi wake mwenyewe, akaamua akae hapo hotelini, huenda kwa kujishuku kuwa anao ugonjwa.
Kwa nini alijishuku. Taarifa hii aliwaeleza watu wa hapo uwanja wa ndege?
Akiwa kajiweka karantini, palikuwepo na tahadhari ya kutoeneza ugonjwa kwa wahudumu hapo hotelini?
Hawa waliomhudumia katika maeneo yote haya, dereva na hotelini wamekwishatambulika na kupimwa kama hawakuambukizwa?
Alipotoka hotelini kwenda hospitali, hapakuwepo na uwezekano wa kueneza ugonjwa?
Wizara imefanya juhudi zipi kuwatafuta watu aliokaribiana nao toka kwenye ndege hadi alipokwenda hospitali. Hawa hawawezi kuwa nao sasa wanaeneza ugonjwa huko mitaani?