NA KUJIBU KWA MANENO YAFUATAYO
Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala): {{Je hawaangalii ufalme katika mbingu na ardhi na alivyoumba Mwenyezi Mungu katika vitu, na huenda ikiwa umekaribia muda wao wa kuondoka duniani kumalizika. Basi ni maneno gani baada ya Qur’an watayamini}} [Al-Araaf : 185].
Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala): {{Je hamwangalii Ngamia vipi ameumbwa, na mbingu vipi zimeinuliwa, na milima vipi imekitwa na ardhi vipi imetandikwa}} [Al-Qaashiyah: 17- 20]. Hizi ni alama ambazo Mola anataka tuzingatie kuumbwa kwake.
قال تعالى) : أَمْ خُلِقُوا مِنْ غَيْرِ شَيْءٍ أَمْ هُمُ الْخَالِقُونَ 35أَمْ خَلَقُوا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بَل لَا يُوقِنُونَ) [الطور35: 36]
Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Amesema kwenye Kitabu Chake: {{Au mumeumbwa kwa kisichokuwa kitu au nyinyi ndio waumbaji. Au nyinyi ndio mlioumba mbingu na ardhi bali wao hawana yakini}}. Kulingana na Aya hizi zinaonesha kwamba ulimwengu haukujiumba wenyewe na haukuwa kiumbe ambacho hakikumbwa wenyewe na kitu bali lazima tena kuna aliyeumba ulimwengu huu na akasimama kwa jambo lake (huo ulimwengu) naye si mwingine isipokuwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) hakuna Muumba asiyekuwa Yeye wala Mola asiyekuwa Yeye.
Matendo ya Mitume 17:24-28 “Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono; wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote. Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao; ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu. Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. . .”
Biblia inatutambulisha Mungu aliye muumbaji, mvumilivu na mwenye huruma anayefanya jitihada za kujihatarisha mwenyewe ili kuturejesha katika mahusiano yaliharibiwa na kuwepo kwa dhambi. Katika kutengeneza daraja kati yake na sisi aliwatuma manabii kutuletea habari ya tumaini la wokovu litakalokamilishwa baada ya muda mrefu kupitia kwa Yesu Kristo ambaye katika mpango huo anatambulika kama mwana. Manabii hawa baadaye waliagizwa kuandika waliyotumwa na kupelekea kuwapo kwa kitabu kimoja kikubwa chenye mkusanyiko wa vitabu 66 kutoka kwa waandishi wasiopungua 40 walioandika katika kipindi cha miaka 1500. Mengi ambayo hayakufahamika huko nyuma kuhusu Mungu yanafunuliwa katika kitabu hiki.