Cyprian Majura Musiba ni nani na anatumwa na nani?

Cyprian Majura Musiba ni nani na anatumwa na nani?

Usihofu, Musiba anatafuta ajira ya ukuu Wa Wilaya ili nafasi ikitokea Rais asimsahau kwenye uteuzi wake.

Akishaupata atatulia tu, Kwa sasa mwache aendelee kuusaka ukuu Wa Wilaya kwa kujipendekeza na kuwazushia watu uongo na kuwachafulia watu sofa zao.

Usije shangaa SIKU akiamua kumtaja hata Mungu kuwa naye ni hatari kwa maisha ya Rais!!

Kwa mfano anaposema CDM imepeleka vijana 500 nje kujifunza namna ya kuisambaratisha serikali yeye alikuwa wapi hadi akawaona na bado hakutoa taarifa ili hao vijana wakamatwe kabla hawajafika popote?

Hao vijana walikodiwa ndege moja au waliondoka kwa magari?

Kwahiyo anataka kusema tangu uanze kuratibiwa mpango huo Wa kuwapeleka hao vijana, wakatafutiwa paspoti ,Viza, wakasafirishwa , bila Serikali wala usalama Wa Taifa kujua !! Kwa lojiki hii anamaanisha Serikali ni dhaifu kiasi hiki?Yaani mambo hayo yote yamefanyika bila Serikali kujua ila ni yeye pekee ndo mwenye Akili nyingi kuliko serikali aliyegundua mpango huo!!!!?

USHAURI, Ni vizuri atafute Namba nzuri ya kujikomba kwa Rais kuliko kuleta hoja za ukichaa kama hizi, Mfano hoja ya CDM amejikuta akiidharirisha Serikali badala ya kuisifia!! Maana ni sawa na kusema Usalama Wa Taifa umelala na haufanyi Kazi Yake vizuri kwanini kushindwa kwao kuwang'amua hao vijana 500 waliosafirishwa na CDM hadi yeye akawagundua badala ya usalama Wa Taifa anataka kusema yeye ndo bora zaidi kuliko usalama Wa Taifa?

apuuzwe tu kama tunavyowapuuzaga wapuuzi wengine.
 
hata Mimi nikiwa upande Wa CCM.naweza nikamtukana mbowe hadharani.na polisi wakabaki wakichekelea.
 
Ameitisha press conference na kutaka vikosi vya usalama viwashughulikie bila huruma Mange Lissu,Mbowe,Maria Sarungi,Zitto na wengine WANNE kwa madai ya kuhatarisha usalama wa nchi na kutumiwa na CIA na FBI
Hana kazi anatafuta huruma ya Magu na Bashite
Hiyo aliyofanya tayar ni kazi aliyotumwa!!
 
https://jamii.app/JFUserGuide you musiba and https://jamii.app/JFUserGuide all your listeners
 
Siku hizi akina Musiba watajitokeza wengi sana kwa ajili ya kujitafutia umaarufu.
 
Mtu anaitwa msiba unadhani atakua na uwezo wa kufikiri sahihi? Huyu ni wa kupuuzwa tu.
 
You are not serious! Hivi kila mtu anaweza kuitisha press bila kibali na akaongea lolote bila kuwa na proof na bado dola ikamwacha tu aende zake kwa mkewe?
Yeye yupo hapo mitaa ya ilala na posta anamangamanga kusaka ugali tena wa kuomba kwa kina bashite, amewaona wapi aliowataja wakitumika na vyombo alivyovitaja na kwa lipi hasa hadi vyombo hivyo vitake habari za hapa?
Kwani marekani ina mpango wa kuja kututawala? Hebu vyombo husika vimhoji aseme vizuri ili kama yeye ni nabii titto mwingine tujue!
Au hili zwazwa linahamisha goli baada ya Trump kuiwakia tz na china? Mtajichambua kama kitumbua!
Telling face!!!!!!Nimejaribu kulitazama kwenye video nimegundua jamaa ni dume jike lisilo na aibu linaburuzwa, mtu mwenye akili sawa asingeweza kufanya kitendo kile, ile ni tusi na dharau kwa vyombo vya ulinzi mana kila poyoyo la CCM lianawapa maelekezo ya nin wafanye sio kwa mujibu wa miongozo ya majukumu yao.Kila mwanaccm anajiona ana mamlaka ya kusema lolote bila hofu!!!!!You know why?tunaongozwa na village men.
 
Kwa hiyo sio kweli kuwa Mange anaratibu machafuko (mapinduzi) hapa nchini?

Msigwa yupo mstari wa mbele kuunga mkono haya machafuko (nimeona postings zake).

Zitto, katika posting zake ameushauri upinzani kuwa kitu kikubwa kifanyike kabla ya 2020. Nadhani alijua ukifika uchaguzi wa 2020 vyama vya upinzani vitafutika.

Ni kitu gani kikubwa anachotaka kifanyike?

Safari ya Zitto hivi karibuni huko Ubeligiji na Oman, pamoja na watu aliokutana nao zaidi ya Lissu, inanifanya nijiulize maswali mengi.

Jamani msifanye mzaha. Upinzani wanajua kuwa kwa kasi hii ya Magufuli hawataambulia kitu kupitia sanduku la kura ifikapo 2019/2020.

Mkakati uliopo kwao ni kuivuruga hii nchi kusudi mataifa ya nje yaingilie kati. Kila dalili inaonyesha hivyo.

JAMBO JINGINE
Ni dhahiri kuwa wanaopata habari zao kupitia social media (JF, INSTA, TWITTER, FB, nk) ni wachache sana - wenye smart phones na computers. Kwa hiyo ili kuwapatia habari watu wa vitochi, hasa vijijini, Mange anaratibu usambazaji vikaratasi (vipeperushi) nchi nzima kwa ndege ili watu wasome kuhusu vurugu za April 26, 2018.

Ni nani anaemfadhili Mange kufanya hivi?

Watu wakinyamaza msifikiri ni wapumbavu.
Kijiji gani wamepata hivyo vipeperushi kwa njia ya ndege?Na serikali/wana usalama wako wapi wasilizibiti hilo?hiyo ndege iliruka kutoka wapi?Je naweza kuwa "wrong" nikisema kuwa huo mpango unaratibiwa na serikali(kwa hali ya kawaida hili jambo kama lingekua na ukweli ndani yake basi ndege hiyo ingekua "captured" mapema sana).

Za kuambiwa changanya na zako.
 
Anaweza akawa na wazo zuri nyuma ya pazia ila akawa na poor presentation kutokana na wrong perception ya baadhi ya aliowataja. Pia, kwa kuanika hivi,ndo kaharibu kama ile issue ya madawa ya kulevya. Hii ni issue nyeti na sio ya kuropoka ovyoovyo tuu.
Mkuu si tu anaweza hana wazo lolote ni mwendelezo wa kutafuta fursa wameishagundua weakness za kiongozi;anapenda cheap popularity na anawachukia wanaomkosoa.Hivi unafikiri ile ni akili ya kawaida?Kwenye psychology tuna kitu kinaitwa "telling face" uso wake unaonesha anatafuta fursa,kila mtafuta fursa anajiona jasiri anapotaja majina ya wakosoaji wakubwa ktk utawala huu.Ulimbukeni na ushamba kwa watawala wetu unaliangamiza taifa (Zitto,2017).Aftalaw mtu mwenyew anaitwa msiba:::
 
Kwa hiyo sio kweli kuwa Mange anaratibu machafuko (mapinduzi) hapa nchini?

Msigwa yupo mstari wa mbele kuunga mkono haya machafuko (nimeona postings zake).

Zitto, katika posting zake ameushauri upinzani kuwa kitu kikubwa kifanyike kabla ya 2020. Nadhani alijua ukifika uchaguzi wa 2020 vyama vya upinzani vitafutika.

Ni kitu gani kikubwa anachotaka kifanyike?

Safari ya Zitto hivi karibuni huko Ubeligiji na Oman, pamoja na watu aliokutana nao zaidi ya Lissu, inanifanya nijiulize maswali mengi.

Jamani msifanye mzaha. Upinzani wanajua kuwa kwa kasi hii ya Magufuli hawataambulia kitu kupitia sanduku la kura ifikapo 2019/2020.

Mkakati uliopo kwao ni kuivuruga hii nchi kusudi mataifa ya nje yaingilie kati. Kila dalili inaonyesha hivyo.

JAMBO JINGINE
Ni dhahiri kuwa wanaopata habari zao kupitia social media (JF, INSTA, TWITTER, FB, nk) ni wachache sana - wenye smart phones na computers. Kwa hiyo ili kuwapatia habari watu wa vitochi, hasa vijijini, Mange anaratibu usambazaji vikaratasi (vipeperushi) nchi nzima kwa ndege ili watu wasome kuhusu vurugu za April 26, 2018.

Ni nani anaemfadhili Mange kufanya hivi?

Watu wakinyamaza msifikiri ni wapumbavu.
Ujinga mtupu kuamini ujinga wako huu. Siamini kama kuna watanzania mbumbumbu wa aina yenu na huyo musiba.

Shaurini mamlaka zimkamate huyo musiba kabla hajasababisha mgogoro wa kidiplomasia baina ya Tanzania na mataifa aliyoyatuhumu. Kumtuhumu kiongozi wa nchi kubwa kama Ujerumani kwamba anaratibu kuandaa mafunzo ya kufanya uhalifu katika taifa jengine, hiyo ni hatari ikiwa ujerumani itataka uthibitisho wa tuhuma hizo. Unapoituhumu taasisi kama FBI (japo sielewi why FBI hapa, labda hakujua kwamba kuna CIA) ni lazima ujipange kuthibitisha hilo.

Serikali ili ijihami ni budi imkamate huyu na kumtaka athibitishe na akishindwa achukuliwe hatua kali za kisheria na pia ajitokeze hadharani aombe radhi kwa ujinga huu. National security ni jambo nyetina lina taasisi maalum inayosimamia, kama yeye ana ushahidi wa tuhuma hizo alipaswa awasilishe kwenye taasisi hizo si kuita press kiholela hivi. Natarajia huyu mtu kukamatwa very soon.

Ushauri: political propaganda ni profession inayohitaji watu wenye weledi na research ability ya hali ya juu. Msiwape watu wajinga kama huyu wataharibu nchi yetu.
 
Kijiji gani wamepata hivyo vipeperushi kwa njia ya ndege?Na serikali/wana usalama wako wapi wasilizibiti hilo?hiyo ndege iliruka kutoka wapi?Je naweza kuwa "wrong" nikisema kuwa huo mpango unaratibiwa na serikali(kwa hali ya kawaida hili jambo kama lingekua na ukweli ndani yake basi ndege hiyo ingekua "captured" mapema sana).

Za kuambiwa changanya na zako.
Nenda kwenye ukurasa wa Mange huko Instagram halafu usome mabandiko yake kuhusu haya "MAPINDUZI" ya tarehe 26 April, 2018.

Hii sio siri. Anaelezea yote kuhusu hivi vipeperushi.

Usiwe unabisha kijinga. Fact-check me first, kabla ya kuleta ubishi.
 
Unapata wapi nguvu ya kuutangazia umma wa Watanzania kwamba hawa ndugu zetu ni hatari??? Mamlaka unayatoa wapi Musiba.....??? Maana ya mtu hatari katika usalama wa taifa ni wewe wa kutoa hiyo hukumu na maamuzi ya kuwaita wenzetu Hatari???

Naombeni msaada ni nani huyu?? Anapata wapi mamlaka na nani amemtuma????

Anatumia utumbo kufikiri na pamoja na yote
Nyota yake inaGIZA kiasi kwamba watawala anaowatumikia hawamkumbuki
hata kumpa Nafasi yakufagia japo Kwenye Wizara
 
Hebu tutende haki tuwe na balancing story hata kwenye hili la Cyprian Musiba aliyetaja orodha ya watu kumi hatari kwa usalama wa Tanzania.

Kwenye orodha yake kawataja kwa majina na karibia wote ni viongozi wa UPINZANI na wachache ni wanaharakati na watoa maoni huyu.

Naomba tulitendee haki jukwaa nasi tuwe na orodha yetu ila tusitaje majina. Tutaje mtu mwenye viashiria vya hatari... Nitaanza wengine mtamalizia

1. Yeyote anayepuuza maoni ya wengine.. Kwa uchache wao ama wingi wao..
2. Yeyote asiyekubali tofauti za kimtazamo katika jamii moja...
3. Yeyote asiyezingatia utawala wa sheria
4. Yeyote asiyezingatia haki za binadamu....
5..... Ongezea
 
Ujinga mtupu kuamini ujinga wako huu. Siamini kama kuna watanzania wajinga kama wewe. Mkamateni huyu musiba kabla hajasababisha mgogoro wa kidiplomasia baina ya Tanzania na mataifa aliyoyatuhumu. Kumtuhumu kiongozi wa nchi kubwa kama Ujerumani kwamba anaratibu kuandaa mafunzo ya kufanya uhalifu katika taifa jengine, hiyo ni hatari ikiwa ujerumani utataka uthibitisho wa tuhyma hizo. Unapoituhumu taasisi kama FBI ni lazima ujipange kuthibitisha hilo.

Serikali ili ijihami ni budi imkamate huyu na kumtaka athibitishe na akishindwa achukuliwe hatua kali za kisheria na pia ajitokeze hadharani aombe radhi kwa ujinga huu. National security ni jambo nyetina lina taasisi maalum inayosimamia, kama yeye ana ushahidi wa tuhuma hizo alipaswa awasilishe kwenye taasisi hizo si kuita press kiholela hivi. Natarajia huyu mtu kukamatwa very soon.
Musiba amesema hisia zake ambazo zina ukweli ndani yake.

Kinachonishangaza ni kuwa:
[emoji830]Serikali ikitumia vyombo vya dola, kama polisi, kuwakamata wahalifu wa upinzani, mnawaita DIKTETA UCHWARA.

[emoji830]Sasa mnaitaka serikali hiyo hiyo ("MADIKTETA") itumie polisi kumkamata Musiba kwa sababu anawaumbua UPINZANI.

Hivi huwa mnajisikiliza mnapozungumza huu ujinga?
 
Back
Top Bottom