Cyprian Majura Musiba ni nani na anatumwa na nani?

Usihofu, Musiba anatafuta ajira ya ukuu Wa Wilaya ili nafasi ikitokea Rais asimsahau kwenye uteuzi wake.

Akishaupata atatulia tu, Kwa sasa mwache aendelee kuusaka ukuu Wa Wilaya kwa kujipendekeza na kuwazushia watu uongo na kuwachafulia watu sofa zao.

Usije shangaa SIKU akiamua kumtaja hata Mungu kuwa naye ni hatari kwa maisha ya Rais!!

Kwa mfano anaposema CDM imepeleka vijana 500 nje kujifunza namna ya kuisambaratisha serikali yeye alikuwa wapi hadi akawaona na bado hakutoa taarifa ili hao vijana wakamatwe kabla hawajafika popote?

Hao vijana walikodiwa ndege moja au waliondoka kwa magari?

Kwahiyo anataka kusema tangu uanze kuratibiwa mpango huo Wa kuwapeleka hao vijana, wakatafutiwa paspoti ,Viza, wakasafirishwa , bila Serikali wala usalama Wa Taifa kujua !! Kwa lojiki hii anamaanisha Serikali ni dhaifu kiasi hiki?Yaani mambo hayo yote yamefanyika bila Serikali kujua ila ni yeye pekee ndo mwenye Akili nyingi kuliko serikali aliyegundua mpango huo!!!!?

USHAURI, Ni vizuri atafute Namba nzuri ya kujikomba kwa Rais kuliko kuleta hoja za ukichaa kama hizi, Mfano hoja ya CDM amejikuta akiidharirisha Serikali badala ya kuisifia!! Maana ni sawa na kusema Usalama Wa Taifa umelala na haufanyi Kazi Yake vizuri kwanini kushindwa kwao kuwang'amua hao vijana 500 waliosafirishwa na CDM hadi yeye akawagundua badala ya usalama Wa Taifa anataka kusema yeye ndo bora zaidi kuliko usalama Wa Taifa?

apuuzwe tu kama tunavyowapuuzaga wapuuzi wengine.
 
hata Mimi nikiwa upande Wa CCM.naweza nikamtukana mbowe hadharani.na polisi wakabaki wakichekelea.
 
Hiyo aliyofanya tayar ni kazi aliyotumwa!!
 
https://jamii.app/JFUserGuide you musiba and https://jamii.app/JFUserGuide all your listeners
 
Siku hizi akina Musiba watajitokeza wengi sana kwa ajili ya kujitafutia umaarufu.
 
Mtu anaitwa msiba unadhani atakua na uwezo wa kufikiri sahihi? Huyu ni wa kupuuzwa tu.
 
Dalili mojawapo ya madhara ya albadiri ni kuropoka.
 
Hahahaaa! we unategemea tukinyamaza tutaonekanaje ili tuteuliwe!
 
Telling face!!!!!!Nimejaribu kulitazama kwenye video nimegundua jamaa ni dume jike lisilo na aibu linaburuzwa, mtu mwenye akili sawa asingeweza kufanya kitendo kile, ile ni tusi na dharau kwa vyombo vya ulinzi mana kila poyoyo la CCM lianawapa maelekezo ya nin wafanye sio kwa mujibu wa miongozo ya majukumu yao.Kila mwanaccm anajiona ana mamlaka ya kusema lolote bila hofu!!!!!You know why?tunaongozwa na village men.
 
Kijiji gani wamepata hivyo vipeperushi kwa njia ya ndege?Na serikali/wana usalama wako wapi wasilizibiti hilo?hiyo ndege iliruka kutoka wapi?Je naweza kuwa "wrong" nikisema kuwa huo mpango unaratibiwa na serikali(kwa hali ya kawaida hili jambo kama lingekua na ukweli ndani yake basi ndege hiyo ingekua "captured" mapema sana).

Za kuambiwa changanya na zako.
 
Anaweza akawa na wazo zuri nyuma ya pazia ila akawa na poor presentation kutokana na wrong perception ya baadhi ya aliowataja. Pia, kwa kuanika hivi,ndo kaharibu kama ile issue ya madawa ya kulevya. Hii ni issue nyeti na sio ya kuropoka ovyoovyo tuu.
Mkuu si tu anaweza hana wazo lolote ni mwendelezo wa kutafuta fursa wameishagundua weakness za kiongozi;anapenda cheap popularity na anawachukia wanaomkosoa.Hivi unafikiri ile ni akili ya kawaida?Kwenye psychology tuna kitu kinaitwa "telling face" uso wake unaonesha anatafuta fursa,kila mtafuta fursa anajiona jasiri anapotaja majina ya wakosoaji wakubwa ktk utawala huu.Ulimbukeni na ushamba kwa watawala wetu unaliangamiza taifa (Zitto,2017).Aftalaw mtu mwenyew anaitwa msiba:::
 
Ujinga mtupu kuamini ujinga wako huu. Siamini kama kuna watanzania mbumbumbu wa aina yenu na huyo musiba.

Shaurini mamlaka zimkamate huyo musiba kabla hajasababisha mgogoro wa kidiplomasia baina ya Tanzania na mataifa aliyoyatuhumu. Kumtuhumu kiongozi wa nchi kubwa kama Ujerumani kwamba anaratibu kuandaa mafunzo ya kufanya uhalifu katika taifa jengine, hiyo ni hatari ikiwa ujerumani itataka uthibitisho wa tuhuma hizo. Unapoituhumu taasisi kama FBI (japo sielewi why FBI hapa, labda hakujua kwamba kuna CIA) ni lazima ujipange kuthibitisha hilo.

Serikali ili ijihami ni budi imkamate huyu na kumtaka athibitishe na akishindwa achukuliwe hatua kali za kisheria na pia ajitokeze hadharani aombe radhi kwa ujinga huu. National security ni jambo nyetina lina taasisi maalum inayosimamia, kama yeye ana ushahidi wa tuhuma hizo alipaswa awasilishe kwenye taasisi hizo si kuita press kiholela hivi. Natarajia huyu mtu kukamatwa very soon.

Ushauri: political propaganda ni profession inayohitaji watu wenye weledi na research ability ya hali ya juu. Msiwape watu wajinga kama huyu wataharibu nchi yetu.
 
Nenda kwenye ukurasa wa Mange huko Instagram halafu usome mabandiko yake kuhusu haya "MAPINDUZI" ya tarehe 26 April, 2018.

Hii sio siri. Anaelezea yote kuhusu hivi vipeperushi.

Usiwe unabisha kijinga. Fact-check me first, kabla ya kuleta ubishi.
 
Anatumia utumbo kufikiri na pamoja na yote
Nyota yake inaGIZA kiasi kwamba watawala anaowatumikia hawamkumbuki
hata kumpa Nafasi yakufagia japo Kwenye Wizara
 
Hebu tutende haki tuwe na balancing story hata kwenye hili la Cyprian Musiba aliyetaja orodha ya watu kumi hatari kwa usalama wa Tanzania.

Kwenye orodha yake kawataja kwa majina na karibia wote ni viongozi wa UPINZANI na wachache ni wanaharakati na watoa maoni huyu.

Naomba tulitendee haki jukwaa nasi tuwe na orodha yetu ila tusitaje majina. Tutaje mtu mwenye viashiria vya hatari... Nitaanza wengine mtamalizia

1. Yeyote anayepuuza maoni ya wengine.. Kwa uchache wao ama wingi wao..
2. Yeyote asiyekubali tofauti za kimtazamo katika jamii moja...
3. Yeyote asiyezingatia utawala wa sheria
4. Yeyote asiyezingatia haki za binadamu....
5..... Ongezea
 
Musiba amesema hisia zake ambazo zina ukweli ndani yake.

Kinachonishangaza ni kuwa:
[emoji830]Serikali ikitumia vyombo vya dola, kama polisi, kuwakamata wahalifu wa upinzani, mnawaita DIKTETA UCHWARA.

[emoji830]Sasa mnaitaka serikali hiyo hiyo ("MADIKTETA") itumie polisi kumkamata Musiba kwa sababu anawaumbua UPINZANI.

Hivi huwa mnajisikiliza mnapozungumza huu ujinga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…