Cyprian Musiba atakiwa kumlipa Membe Tsh. Bilioni 9 ndani ya siku 14

Cyprian Musiba atakiwa kumlipa Membe Tsh. Bilioni 9 ndani ya siku 14

Musiba asipotuaga kwa pressure ataishia kuwa chizi, siku hizi nikiitazama ile sura yake namuona hayuko na amani, moyo wake mzito.

Angefanya atleast public apology angeweza kusamehewa na wale aliowakosea, ili apate amani, kwani nao ni binadamu pia, kuliko kukaa kwake kimya huku akiteketea ndani kwa ndani.
Jitu jinga kama lile wala sio la kuonea huruma.
"...waacheni wafu wazikane..."
 
Katiba yetu Ina mwanya. Inaposema kila mtu ni sawa , jiulize mbona Rais hashtakiwi au mbona Rais halipi Kodi?.

Pia kwenye sheria ya tort Kuna kitu kinaitwa punitive damages , yani fidia Kama adhabu.
Rais kwa mjibu ya katiba yetu hashitakiwi kwa kesi za jinai (criminal cases), kwa kesi za madai ni ruhusa kumshitaki amalizapo kipindi cha uraisi. Umuhimu wa hivi vifungu ni kuletaa utulivu wa nchi na kuwatunuku amani na utulivu watu waliowahi kushika kazi hii ngumu, ya kipekee na yenye mamlaka ya juu kuliko zote kwenye taifa hili. Wangeweza kung'ang'ania kuwa maraisi kama wangetaka kwa mbinu mbali mbali hususani kubadili vifungu vya baadhi ya vifungu vya katiba.

Sasa huyo Mwembe wako unamliganishaje na rais. Hana tofauti na mimi au wewe.
 
uwezo wa musiba kulipa ni elfu 20000 kila mwezi , na atatekeleza hilo kikamilifu tuone kama atawekwa kizuizini

Issue sio elfu ishirini, issue ni kiasi chote anachodaiwa.
 
Rais kwa mjibu ya katiba yetu hashitakiwi kwa kesi za jinai (criminal cases), kwa kesi za madai ni ruhusa kumshitaki amalizapo kipindi cha uraisi. Umuhimu wa hivi vifungu ni kuletaa utulivu wa nchi na kuwatunuku amani na utulivu watu waliowahi kushika kazi hii ngumu, ya kipekee na yenye mamlaka ya juu kuliko zote kwenye taifa hili. Wangeweza kung'ang'ania kuwa maraisi kama wangetaka kwa mbinu mbali mbali hususani kubadili vifungu vya baadhi ya vifungu vya katiba.

Sasa huyo Mwembe wako unamliganishaje na rais. Hana tofauti na mimi au wewe.

Point yangu ni kwamba Hakuna usawa wa sheria, ni nadharia tu. Ndio maana umesema mwenyewe huwezi kumlinganisha membe na Rais , kwa maana hiyo kisheria Membe na Rais sio sawa.

Ndio maana Musiba kapigwa bilioni Tisa maana kamchafua Waziri wa mambo ya nje mstaafu, mbunge mstaafu , mfanyabiashara nk.
 
Basi mahakama inapasa pia kuangalia namna bora ya mdai na wadaiwa kulipana, na wala siyo kwa malipo yakamilike ndani ya siku 14 kama vile ambavyo oda ilivyotolewa.

Alipewa muda wa kulipa tangu October 2021, akashindwa hivyo Membe akaiomba mahakama imsaidie kupitia kikaza hukumu. Ndio maana Sasa mahakama imempa siku kumi na nne alipe hiyo pesa.
 
So adhabu alishapata? 🤣🤣🤣🤣 Kwa style hii kweli ccm itatawala milele na watu hawatakuwa na woga.

CCM kutawala milele sio issue, issue Ni kwamba huyo Makonda wako alikataliwa na CCM hiyohiyo Tena hadharani tena pamoja na kiburi chote Cha madaraka.
 
Mimi nilishangaa anamshambulia Membe nikajua jamaa ni boya. Kuna watu kuwashambulia hivi hivi ni hatari.
Huyu bwana ni hatari sana, watu kama hawa wako radhi nchi iangamie kwa kisingizio cha kumlinda rais.Akipelekwa jela ni sahihi kabsaa.
 
Hapana aombe radhi hadharani na kujutia makosa yake. Akubali kutembelea magoti kwenda kwa Membe. Maana sidhani Kama Membe ana shida na hizo pesa bali kumfunza adabu asirudie huo ujinga Tena.
Huo ujanja janja hapana akanyee debe, alikuwa akisema ameyasema haya akiwa na akili timamu.
 
Back
Top Bottom