Dada Poa anayeitwa Latifa adaiwa kuuwawa na "Mteja". Akutwa uchi akiwa amenyongwa

Dada Poa anayeitwa Latifa adaiwa kuuwawa na "Mteja". Akutwa uchi akiwa amenyongwa

Mwanamke aliyefahamika kwa jina moja la Latifa, anayefanya biashara ya ngono, amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha baada ya kukutwa ndani ya chumba namba nne katika Lodge ya Dolphin, eneo la Kaloleni jijini Arusha, usiku wa kuamkia Oktoba 18, 2026.

Kwa mujibu wa mashuhuda, Latifa alikuwa amepangisha chumba hicho kwa Shilingi 30,000 tangu mchana, kabla ya kuingia na mwanaume aliyedaiwa kuwa mteja wake. Baadaye, marafiki zake walipoona hajatoka kwa muda mrefu, waliamua kwenda kuangalia kilichokuwa kikiendelea.

Walipoingia chumbani, walimkuta Latifa akiwa uchi, mikono imefungwa, mdomo umezibwa na mtandio ukiwa umefungwa shingoni mwake, hali iliyozua hisia kuwa huenda alinyongwa.

Marafiki zake walimkimbiza katika Hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya kupata msaada wa matibabu, lakini walipofika walibaini kuwa tayari amefariki dunia.

Mwanaume aliyeingia naye chumbani anadaiwa kuondoka na fedha pamoja na simu ya marehemu. Hata hivyo, utambulisho wake na chanzo rasmi cha kifo cha Latifa havijathibitishwa, huku uchunguzi wa mamlaka husika ukihitajika kubaini ukweli wa tukio hilo.


Huyo mhalifu kafanya bonge la mistake kuondoka na hiyo simu, labda kama alipotoka tu hapo alienda kuitupa simu, lakini haisaidii kama waliwasiliana kwenye simu kabla ya kwenda hapo lodge. ni sekunde tu atadakwa. Huyo tusimweke kwenye kundi la wanaume, ni mvaa suruali
 
BTW, serikali iangalie sana jamii zetu zimeharibika vibaya.
Tamaa ya fedha na wivu wa mapenzi vinamaliza roho za watu
 
Tatizo la bongo ni lodge iweje hakuna kamera, hakuna check out nairobi wana utaratibu mzuri japo ni kero ila unasaidia anayeingia na demu hatoki peke yake, akitoka kabla hajavuka reception wanapiga simu kujua alibaki yukoje au mlinzi wa juu anafanya check-in then wanawasiliana ndio unaruhusiwa kutoka, huu ni uzembe bongo umezidi
 
Huyo mhalifu kafanya bonge la mistake kuondoka na hiyo simu, labda kama alipotoka tu hapo alienda kuitupa simu, lakini haisaidii kama waliwasiliana kwenye simu kabla ya kwenda hapo lodge. ni sekunde tu atadakwa. Huyo tusimweke kwenye kundi la wanaume, ni mvaa suruali
Wale malaya wa pale Kaloleni hakuna cha kuwasiliana kwenye simu, wanakua na room zao pale, mnaelewana bei mnaenda kumalizana.
 
sasa tuanzishe kampeni ya PRAY FOR ARUSHA.jiji lile siyo lile tena,ni matukio juu ya matukio.
PRAY FOR ARUSHA
Hao madada kuna baadhi wana mambo ya ajabu muda mwingine sio wa kuwatetea kuna wakati wanakua wezi vibaka wakabaji yaan unaingia nae room anaenda kukukaba anakuibia bila kupenda na ukifanya namna gani anasema anakujazia watu sasa inaweza kua walifika stage akaamzingua jamaa ndio hapo ikawa amekutana na mbaya wake hii nishakutana nayo mara kibao huko kwenye machimbo kuna ambao ni wastaarabu na kuna wengine wanapenda kupata pesa kwa kukukaba apate pesa kimseleleko huduma hakupi na hela anataka kubwa na anakwambia ikiwa namna gani anakujazia watu, sasa mlikua chumbani wawili hakuna anaejua kilikua nini akijaza watu akasema umemgonga na haujamgonga na anataka kiasi fulani wewe unafikiri utasemaje, kingine hio inaweza ikawa ni kisasi alidhurumu mtu akatuma mtu aende akamfundishe adabu isivyo bahati kafa
 
Huyo aliyofanya hivyo tutakutafuta na tutakunyonga wenyewe hutaenda MAHAKAMI umeingia sekta nyeti.
 
Ni wale Malaya wa Tinder na badoo? Kulala anakuambia 350K short time 200K.😀
 
Mwanamke aliyefahamika kwa jina moja la Latifa, anayefanya biashara ya ngono, amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha baada ya kukutwa ndani ya chumba namba nne katika Lodge ya Dolphin, eneo la Kaloleni jijini Arusha, usiku wa kuamkia Oktoba 18, 2026.

Kwa mujibu wa mashuhuda, Latifa alikuwa amepangisha chumba hicho kwa Shilingi 30,000 tangu mchana, kabla ya kuingia na mwanaume aliyedaiwa kuwa mteja wake. Baadaye, marafiki zake walipoona hajatoka kwa muda mrefu, waliamua kwenda kuangalia kilichokuwa kikiendelea.

Walipoingia chumbani, walimkuta Latifa akiwa uchi, mikono imefungwa, mdomo umezibwa na mtandio ukiwa umefungwa shingoni mwake, hali iliyozua hisia kuwa huenda alinyongwa.

Marafiki zake walimkimbiza katika Hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya kupata msaada wa matibabu, lakini walipofika walibaini kuwa tayari amefariki dunia.

Mwanaume aliyeingia naye chumbani anadaiwa kuondoka na fedha pamoja na simu ya marehemu. Hata hivyo, utambulisho wake na chanzo rasmi cha kifo cha Latifa havijathibitishwa, huku uchunguzi wa mamlaka husika ukihitajika kubaini ukweli wa tukio hilo.

Inasikitisha sana. Ila itakuwa huyu mteja lazima wanajuana, moja inawezekana walikuwa na mahusiano kabla labda Latifa akaamua kuendelea na maisha yake muuaji hakuridhika. Simu ya Latifa lazima inasiri zote, tunaamini atakamatwa muda wowote
 
Back
Top Bottom