Dada yangu amerudi nyumbani amesema wito wa usister wa Kanisa Katoliki umemshinda na anataka kuolewa

kwanini amerudi kutoka utawani na wakati yeye mwenyewe ndiyo alisema anataka kuwa Sister
Kwa kuwa alisema mwenyewe kuwa sister na sasa amesema mwenyewe kuwa utawa umemshinda anataka kuolewa hana kosa katika hilo ni uamzi wake.
 
Hana kosa lolote,. Kama mawazo yake yalivyomuongoza kwenda kusoma ndio yaliyomfanya akaacha kusoma. Furahi ndg huenda amepatikana shemeji
 
Kwa kuwa alisema mwenyewe kuwa sister na sasa amesema mwenyewe kuwa utawa umemshinda anataka kuolewa hana kosa katika hilo ni uamzi wake.
Kuna yege moja amelionja limemchanganya hatari ebwana hii miyege inachanganya Wanawake we acha tu
 
Umeeleza vizuri sana.
 
Mama yako ni sister!?
Kwani kakwambia ameandika hivi akiwa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima?
Si kasema yupo nyumbani kwa baba na mama,sasa mama yake aliyemzaa yeye na dadaake,anakuaje sister?
Ila maswali mengine yanayotoka kwa watu wengine bhana.
 
Muda huo mimi ndoa imenishinda, nataka niwe Padre. Hawa Wanawake wa Kiswahili, hasa kutoka Mwananyamala, ni shiiida sana.
 
SAsa mwanamke kuolewa inakuaje aibu kwa familia.!
 
Ni kweli kabisa masister wananyonywa sana na hayo mashirika yao.
Wanafanya kila jitihada za kuwasomesha sana na kupata ajira kwenye serikali, ila mshahara wote anaupeleka kwa shirika!!

Hata ishu ya bima ya afya wazazi hawamo akiwa nayo!!
Ni sifa tu za kijinga tunatoa sisi tulio nje ila wao walioko ndani wengi wanashida sana.
Mwisho wanakuwa watumwa wa ngono kwa mapadre ili wapate cha kutuma nyumbani.
 
daa kama kweli tukifa kuna mbingu na moto wake upo kuna watu watakuwa kuni kabisa aisee. ila iyo ya kuacha usista sio kesi kabisa maana lile ni chaguo mtu anafanya mwenyewe bila kulazimishwa ndomaana kila mwaka lazma wanatakiwa kusema km bado ana nia ya kuwa sista au la. maanaake akibadili mawazo ni ruksa kuacha usista. sio kesi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…