Dada yangu anaishi na bwana huu mwaka wa 4 hawajafika nyumbani kutambulishana wala kulipa mahari

Dada yangu anaishi na bwana huu mwaka wa 4 hawajafika nyumbani kutambulishana wala kulipa mahari

Wewe endelea kuchimba mashimo....mambo ya dadaako na shemeji yako waachie wenyewe
 
Ndiyo; wanakosea sana lakini sio jukumu lako kukosoa au kulazimisha masahihisho. Wee subiri tu muda utafika ambapo watajua walikuwa hawajui wanakosea sana.
Una Akili wewe? Hujui mimi ni kaka yake ebo!
 
Mwaka 2018 alienda Dar-es-salaam kutafuta maisha katika harakati za maisha jamaa kajitokeza kua na dada. Cha ajabu huyu sister sijui ana Akili gani hua anakuja yeye tu maskani lakini bwana wake hajawai fika.

Yani hata barua kiufupi hajafata taratibu zozote za kiafrika hii imekaaje? Sijapenda.

Sijapenda kwakweli na hii ni kama kujishushia hadhi yeye na familia yetu. Kitendo hiki kinanipa hasira hata kuwasiliana na sister ni mara chache sana kwa mwaka.

Wanawake sijui akili zao zikoje. Ukitaka matusi jaribu kumuambia izo habari. Ni kweli wanaishi pamoja kama mke na mume ila stail yao Sijapenda naomba ushauri.

Hua sina amani hata kufikia kwao kuna watu ndugu wakienda wanafkia ila mimi hapana siwezi.
Cha kukshauri mkazanie jamaa atoe mahari.Sikuizi wanaume waku oa wameisha
 
Kikubwa wanaishi vizuri na anahudumiwa dada yako huduma yote ikiwemo kwichikwichi basi mshukuru mungu maana siku hizi wanaolewa wanaachwa na watoto bila hata kuambulia kitu.
 
Si mlisema mwanamke asiyekua bikira asilipiwe chochote 🥲
 
Unajuaje kama wazee wapo?
Wazee hawawezi kukosekana hata siku moja. Kama baba (biological father) hayupo lazima atakuwepo aliyeidhinishwa kuisimamia familia yenu. Kama aliyeidhinishwa anazembea jukumu lake hilo, basi wapo baba mdogo/mkubwa, wajomba au First born katika familia yenu. Hakuna kitakachoharibika au kushindikana. Wewe waache hao wajifarague kwa sasa kwa kuwa uzima upo. Likitokea la kutokea (japo hatuliombei) hakuna rangi wataacha kuona.
 
Una Akili wewe? Hujui mimi ni kaka yake ebo!
Ndiyo. Inawezekana akili nilizonazo japo kidogo, zinaniwezesha nikushauri kwa nia njema tu kwamba Dada yako kwanza ni Haramu kwako na usimfuatilie sana esp.katika masuala ya kimapenzi. Unaweza hata kupotezwa kimasikhara kisa eti unampambania dada yako ambaye hata hajalalamika. Kwani wewe ndo ulimpeleka huko? Makubaliano baina yao unayajua wewe?
 
Ndiyo. Inawezekana akili nilizonazo japo kidogo, zinaniwezesha nikushauri kwa nia njema tu kwamba Dada yako kwanza ni Haramu kwako na usimfuatilie sana esp.katika masuala ya kimapenzi. Unaweza hata kupotezwa kimasikhara kisa eti unampambania dada yako ambaye hata hajalalamika. Kwani wewe ndo ulimpeleka huko? Makubaliano baina yao unayajua wewe?
Makubaliano gani haramu hayo?
 
Watu wengi ni zero brain. Unapaswa kujua dada yako anaishi na nani.

Hata kama hajalipa mahari inapaswa kwenda kujitambulisha ukweni. Hiwezi kuishi na mwanamke miaka minne usifanye jitihada za kujua ndugu zake

Wengi akili sifuri wasikukatishe tamaa. Nenda kamweleze shemeji aje ajitambulishe nyumbani

Nina baba yangu mdogo anaishi mwaka 21 hajawah hata kumuona mama mkwe. Baba mkwe wake anamchukia hatari. Sifuri
 
We binafsi una mke? Huamki tu ukaenda ukweni kujitambulisha lazima mipango mikubwa ifanyike. Unakuta mahitaji yanamhitaji jamaa awe na 10M ili kukamilisha Process.

Fikiria kwa kuwa wamekaa miaka yote hiyo huenda wana watoto tayari. Unafahamu taratibu zake za kujitambulisha?
1. Kama wazazi wa pande mbili wanaishi mikoa au wilaya tofafuti kuna ghalama za kuwasafirisha wazazi na baadhi ya ndugu, mahali pa kulala angalau usiku mmoja pamoja na ghalama za chakula wakati wa kwenda kutoa mahali
2. Kwa kuwa ameishi na dada yako bila ridhaa ya wazazi wako basi jua jamaa anafikiria kupigwa faini ya kati ya 1M-2M.
Baada ya hapo apangiwe au kutoa mahali ambayo kiwango kinategemea destruri na tamaduni upande wa mwanamke. Kabla za wafugaji zinatoza mahali kubwa.

3. Baada ya hapo anatakiwa kujibu swali la ndoa inafungwa lini kwa kuwa amejisalimisha. Na hapa haitakiwi kuvuka mwaka.

Hapo ukute mke na mume wamepiga hesabu wameona hiyo pesa waizungushe kwanza🤣🤣
 
Back
Top Bottom