Dada yangu ananipa hasira, alikimbia ndoa baada ya mwaka sasa yupo kwa wazazi

Hakukuwa na haja ya kuandika hizo tarakimu za pesa sijaona kama mada yako ilihitaji kuweka hizo tarakimu
Si kuonyesha jinsi huyu bi Mama alivyochakaza mafao ya wazazi halafu akakimbia ndoa mchana kweupe.
 
You are right... Ilishawahi tokea huko Mombasa.. from day one bw. Harusi alianza uchafu huo wa tigo.,. (Aisaee Story ndefu) tu
 
Kwanza wewe mwenyewe umeoa? Mambo ya ndoa ni mengi na ni zaidi ya yanayoonekana kwa watu waliopo nje ya ndoa husika.
Pili unamkingiaje kifua shemeji yako kwamba ni mtu mwema wakati huishi nae? Huenda dada yako anapitia
mateso ya kisaikolojia ndiyo maana anasema ananyanyaswa.
Huenda kweli dada yako ameamua hana mpango tena wa kurudi kwenye hiyo ndoa na kama huo ndiyo uamuzi wake waachie wazazi watumie busara zao kujadiliana nae.
 
Sio kila mwanamke / mwanaume anaweza kumudu kuivumilia ndoa.

Uvumilivu kwenye ndoa kwa % zaidi ya 90 hutegemea malezi na makuzi ya mtu tangu utoto.

Hakuna mwanaume anayeweza kumvumulia mwanamke mjeuri, kiburi, dharau, mchafu, mvivu, na mwenye mdomo kama chuchunge katika ndoa.

Wanawake wengi hushindwa kuivumilia ndoa hasa kwa changamoto ya mume kutowajibika kwaajili ya kuihudumia familia yake aliyoianzisha na mkewe.

Chukulia mfano wale majaji wa shindano la bongo star search wanaweza kweli kuwa kwenye ndoa? kwa aina ya lugha wanayoitumia mbele ya vyombo vya habari!! Vipi wakiwa huru bila ya kuwa mbele ya kamera?
 
60 mil kwa ajil ya kupata mjukuu,kwel wazazi wetu wanaupendo sana,mungu awajalie maisha marefu
 
Ulichokosea ni kuweka hiyo mil 60

Ngoja jobless waje [emoji3][emoji3][emoji3]

Ila ndoa ina mambo mengi, na pengine sababu za wao kushindana kamwe hutozijua, na pengine hazikuhusu.

Huyo dada mtafutieni tu namna ya kujitegemea ili maisha yaendelee.
 
Mpaka sasa sijaona tatizo lake ila naona tatizo kwa wazee wako
Wamekaa na mke wa mtu na hawajitikisi kuuliza anarudi lini kwake zaidi wanamtafutia na dada wa kazi
 

Pole sana ila huyo ni damu yako na watoto wako watamuita shangazi. Usishangae wana rithi hizo tabia. Wewe jinyamazie ombea watoto wako wasiwe hivyo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…