Dalili za mvua ni mawingu: Mradi wa SGR hautakamilika wote ndani ya utawala wa Magufuli

Ni kweli, kuna kampuni ya kichina ilitaka kusaini na Jakaya kwa dau kubwa lenye mizengwe,lakini haikuwa sababu ya kuwanyima wachina kazi maana kampuni zipo nyingi.
Kampuni za China zilitaka kujenga hii sgr yetu kwa bei ya mara mbili kuliko ya Yapi Merkez, tena isiyokuwa na umeme kama waliyojenga huko Kenya.

Hivyo tukampa Yapi Merkez ambaye anaijenga kwa ubora wa juu sana. Kampuni za China baada ya kuona hivyo sasa vimepunguza bei kidogo kuliko Yapi Merkez na zimeahidi kujenga kwa ubora huo huo au zaidi kidogo wa Yapi Merkez. Kampuni moja tayari imeshaanza kazi ya ujenzi wa sgr kutokea Mwanza hadi Isaka. Kampuni nyingine ya China karibu itaanza kazi kutokea Tabora hadi Isaka. Tunatafuta kampuni nyingine ianzie Tabora hadi Makutupora. Hizi kampuni tatu zitakamilisha vipande vyao ndani ya miaka 2 au 3. Hivyo kufika mwaka 2024 reli yote ya sgr kutoka Dar hadi Mwanza itakuwa imekamilika kwa 100%. Itakayochelewa ni ile ya kutoka Tabora hadi Kigoma na ile ya kutoka Isaka hadi kwa Kagame. Hizi zitasubiri kidogo lakini normal gauge rail inajengwa kutoka Mpanda hadi DRC na wahandisi wetu wa TRC, na itakamilika ndani ya mwaka 1 au 2.

Kenya walioanza kabla yetu bado wanahangaika wakati wala si ya umeme. Sisi tuko vizuri sana. Hakuna mawingu kwenye hili wala dalili zo zote za mvua. Kazi zinaendelea kwa uhakika na spidi ni nzuri. Ujenzi huu ni wa design & construct method hivyo muda ujenzi utakaotumika kwa kila eneo unapatikana baada ya kulifikia eneo na kulifanyia detail design inayokidhi eneo hilo. Hata gharama ya ujenzi inakuwa hivyo hivyo provided total cost isizidi cealing ilyoko kwenye mkataba (framework). Chenji ya pesa lazima itabaki. Shirika letu la reli linasimamia vizuri sana kazi hii na liko imara chini ya Kadogosa!
 
Na ndio sababu ya kuomba Rais Magufuli aongezewe muda wa kutawala Tanzania kukamilisha ndoto zake kwa watanzania !

Au mnasemaje ?
 
Watu walikuwa wanatafuta namna ya kupiga hela mkuu.
Hata mkilalamika sasa utaambiwa miradi mikubwa inatekelezwa huku wanashibisha matumbo yao.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Tatizo siyo kampuni ya ujenzi Tatizo ni Serikali kuwa wasumbufu kulipa wanachelewesha malipo hawalipi kwa wakati
 
Kuna usumbufu mkubwa kwenye malipo Serikali huchelewesha malipo hivyo Tatizo siyo kampuni bali ni Serikali yenyewe
 
Kampuni ingekuwa na Tatizo tungeshasikia mtukufu mwenyekiti wa CCM akipita kelele juu yao, lakini kwa kuwa Tatizo ni wao kuwa wasumbufu kulipa kwa wakati ndiyo maana wapo kimya sana.
 
Mradi wa SGR ni mkubwa sana. Hauwezi kukamilika wote ndani ya kipindi cha awamu hii. Kasi ndogo ya Yapi haina uhusiano na kuchelewa kwa lots zilizobaki. Pesa yake ya mwishi ilikuwa kwenye bajeti ya 2018/19.

Pia serikali ni kama ishajifunza kutoka lot 1 ndiyo sababu pengine lot 5 kapewa Mchina. Huenda lots nyingine wakapewa wengine pia. Mradi mzima wa reli ya kati ni takriban kilomita 2500 hivyo haiwezi kukamilika awamu hii.

Bali kwa kipande cha Dar - Mwanza itakuwa ajabu iwapo hakitakamilika by 2025.
 
Na ndio sababu ya kuomba Rais Magufuli aongezewe muda wa kutawala Tanzania kukamilisha ndoto zake kwa watanzania !

Au mnasemaje ?
Wanajua kuomba aongezewe miaka ya kukaa ikulu kama museveni wa Uganda, lakini hawajui kuomba Serikali iwalipe makandarasi kwa wakati kazi ziende kwa kasi
 
Kampuni ingekuwa na Tatizo tungeshasikia mtukufu mwenyekiti wa CCM akipita kelele juu yao, lakini kwa kuwa Tatizo ni wao kuwa wasumbufu kulipa kwa wakati ndiyo maana wapo kimya sana.
We bichwa bumunda ndio watudanganye kuwa mradi upo tayari wakati bado?
 
Hiyo reli ya Mpanda Hadi DRC itapitia wapi mkuu ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…