Nikivaa jezi yangu ya Manchester United nitaulizwa passport ya UK!
 
Imagine washabiki wa Mamelodi wanakuja kuishangilia timu yao, halafu wanajikuta wanaulizwa passport uwanjani kwa sababu ya jezi walizovaa.

Wakirudi kwao lazima tuwekwe kwenye vituko vya dunia.
Halafu anasema ni 'Uzalendo''. Tuna viongozi wa ajabu sana, uzalendo haubambikizwi ni 'itikadi ya mtu kwa taifa lake'
Kuwa mshabiki wa Yanga au Simba si uhaini wa nchi. Timu hizi zimekuwa na upinzani kwa miaka dahari

Upinzani wa Simba na Yanga ndio umezijenga katika ukanda wa A.Mashariki. Zama hizo Simba na Yanga wakicheza A.Mashiriki inazizima, ni kwasababu ya upinzani lakini haina maana ni kukosa Uzalendo.

Sioni tatizo kabisa ! nadhani tatizo wanalikuza tu. Nitavaa jezi yangu ya Man U.
 
Huwa tunamuonea sana Idi Amin kwa kumfanya kuwa alikuwa dikteta wa ajabu saana, wakati tuna viongozi wengi ukiwaweka katika mizani ya cross multiplication ya muda, elimu, nafasi, wanavyojimwambafy unajiuliza "huyu angekuwa na mazingira kama ya Idi Amin kweli asingekuwa Idi Amin wetu huyu?"
 
Eti ndio bingwa wa sheria wa simba ila kichwani empty
 
Kwa kweli Serikali ya CCM haijawahi kuwa na viongozi wa maana zaidi ya Magufuli na Sokoine na kwa mbali Lowassa, huyu mtu inabidi akamatwe atiwe ndani kuongea ujinga wa namna hii.
 
Kuna baadhi ya vitu mpaka unashangaa, utafikiri hii ni vita nchi yako inapigana na nchi jirani ambayo uzalendo ni lazima kwa maslahi ya Taifa
 
Kila nchi ina utaratibu wake. Na utaratibu wa Tanzania ndiyo huo, so ni lazima kuufuata.

Ova
Huu sio utaratibu ni kuingilia maamuzi ya mtu binafsi, na sio kosa kisheria una haki ya kushabikia timu yoyote

Sasa ule ustahamilivu wa 4 R za kiongozi wa nchi ina maana watendaji wake hawauishi??
 
Mbona kama wana hofu sana kipindi hiki? Kipindi chote depotivo de utopolo walivyokua wanavaa mpk raisi wao walikua hawaoni??
Wanazunguka mbuyu Tu wangemtaja Injinia Hersi na Manara waache tungemwelewa.😁
 
Sio kushabikia Tu Hadi kuwapokea. Mpira WA Tanzania umeharibika Sana. Uzuri WAASISI WA uharibifu huo wako kwenye timu yako pendwa.😂😂
 
Safi sana, Makolo Madunduka ushamba na hasadi umewazidi.
 
Hivi hawa mawaziri huwa wanajiandaa na mahojiano kwa maana nini la kusema? Nikisikia vitu kama hivi naanza kuwa na dharau na elimu ya Tanzania, huyu aliwahi kuwa waziri wa katiba na sheria nchi hii. Hivi Simba na Yanga wakiwa wamejiandaa vizuri kushinda kuvaa kwangu jezi ya Mamelodi au Alhly inaweza kuwa kisingizio cha kufungwa? Michezo ni furaha, utani ndio raha ya mpira wenyewe tusianze kugeuza viwanja vya mipira kuwa airport kuoneshana passport. Mambo ya kijinga kabisa.
 
Hata huku kuna washabiki kibao wa Liverpool, Man sijui Arsenal na wengine je tuoneshe passport za UK au? waziri boya sana, ndio shida ya kuwa na wizara zisizokuwa na kazi unaishia kutoa matamko kama uko nyumbani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…