Dar es Salaam ili uende kazini na kurudi lazima uandae elfu 10 ya usafiri pamoja na chakula. Maskini hana chake hapa nchini

Dar es Salaam ili uende kazini na kurudi lazima uandae elfu 10 ya usafiri pamoja na chakula. Maskini hana chake hapa nchini

Kipato hicho hicho unatakiwa uwe na savings (akiba) maana majanga hayakwepeki, usisahau kufumbia macho misambwanda huko mtaani ukishindwa hutoboi miaka nenda rudi
 
Hahahaha mkuu, hivi dar huwa kuna baiskeli eee. Ngoja nianze kuzingatia.
zipo ndugu yangu...ukienda mwanzo wa kariakoo pale ILALA zipo baiskeli za mtumba Chopa nzuri kweli ukiwa na 150,000/= au 200,000/= unapata baiskeli nzuri mountain bike ambayo utapita popote bila kukuchosha sana.

siku za mwanzo utachoka sana ila ukizoea mkuu utakuwa umejitoa kwenye hicho kitanzi cha usafiri wa kugombania...

je unaishi wapi...? na kazini kwako ni wapi...?​
 
018100094042.JPG
 
Ukae Riverside au Sinza si pesa yote itaishia kwenye madanguro atleast Kimara
Hizo ni tabia binafsi mkuu 😁😁😁
Hata ukikaa kimara na unapenda starehe, kila siku utapitia
 
Dah nmetoka kupiga jana tu hesabu ya mwezi maana nlidownload app ya budget playstore ambayo nilikua naandika kila income na expenses nlizokuwa natumia mbona macho yaligeuka mekundu na nguvu kuniisha

Maana daily 20k mafuta gari
Daily 20k home na hapo baadh ya vitu vipo
Bills umeme,maji nk 50k
Chakula job 10k hpo ndo kujibana
Vocha
Na mengineyo.
NB;
Sinywi pombe wala si mtu wa starehe
Umefka mwsho wa mwezi Expenses zimegonga 3m+ nikawa kama nimemwagiwa maji

[emoji23][emoji23][emoji23]kuna vitu sio sawa kuvipigia hesabu unaweza jikuta siku nzima umevimba uso hucheki na mtu.
 
Huyu ni mwajiriwa wa serikali atawezaje kuamua sehemu ya kwenda kufanya kazi?
Kama ni mwajiriwa wa serikali angalia makazi ya karibu na kazini, unafanya kazi tmk kwanini ukakae Kimara? au tegeta? Panga hapo Mbagala, buza n.k.

Usiishi sehemu kwa kufata mkumbo, hasa marafiki na ndugu, angalia unafuu wako wa kufika kazini tu.

Mfano mm wakati naanza maisha nilitaka kukaa karibu na kazi yangu lakini kwa sababu ni Mbagala ndugu walinisema sana, unakaeje Mbagala kama..... Mm sikuskiliza leo wenyewe wamekubali na kuacha kunishangaa kama mwanzo na ili waone mm ni mtu wa msimamo nimenunua kiwanja sehemu wasioikubali kabisa yan mbali nao, ila mm naangalia kipato changu sio chao.

MATOKEO YA MAISHA YAKO YA BAADAYE NI WW MWENYEWE SIO NDUGU WALA MARAFIKI ZAKO.
 
Pengine atakuwa amejenga mbali ndiyo maana analalamika kuhusu nauli kwasababu sio yeye Tu wapo wengi ambao wamejenga nje ya mji na wanafanya kazi city centre
 
Pengine atakuwa amejenga mbali ndiyo maana analalamika kuhusu nauli kwasababu sio yeye Tu wapo wengi ambao wamejenga nje ya mji na wanafanya kazi city centre
Asee ni kweli mkuu lakini kama anashindwa kuresize iyo 10k ya nauli ili aweze kuilipa basi hali yake itakuwa ngumu, kwa mfumo wa Kiafrika pambana kuendana na mabadiliko, punguza matumizi yasiyo ya lazima ili ujazie iyo ya naul. Mambo mengine huwezi kubadili hata ufanye nini.
 
Ningeshauri kama ingependeza kungekua na usafiri wa kushare ambao watu wanaotoka Kimara mpaka Posta, Gongo la mboto mpaka Posta na Bunju mpaka Posta na kama gari ya watu watano then mnachangia hata elfu 5 na inakua ni nzuri zaidi
 
Katafute chumba karibu na ofisi pangisha ili uwe unaenda home wikiend tu
Ukishindwa huko unapokaa Kama umejenga pangisha ilo jengo lako ww kapange mjini karibu na ofisini kwako
 
Hapa watu wanamkashifu mtoa thread lakini kiuhalisia maisha ya watumishi wa umma wanaokaa dar ni magumu tena zaidi ya sana kwanza huwezi kupata kiwanja kimara cha 8m huo ni uongo na ukipata ni mlima hata pikipiki haifiki nilikuwaga na ndoto za kuajiriwa serikalini nikiamini huko kwenyewe mungu sio athuman nikafanikiwa kupata ila asaivi najuta sana tena zaidi ya sana asilimia 100 nilikuwaga private sector fulani nilikuwa nalipwa mara 8 ya mshahara niliokuja kuupata serikalini huo wa serikali bado hujala nauli sjui maji wakati kule kulikuwa na mabus na chakula kilikuwepo kiukweli huwa najuta ila naamini ntaacha kazi siku sio nyingi siwezi kuteseka na fani yangu
 
Muhimu ni kujipanga tu ila kiukweli kitu ambacho sintopenda mwanangu au wanangu waje kupitia ni kuajiriwa serikalini bora private sector sijui hawa wanoopigaga viwango vya mishahara huwa wanazingatia nini ipo siku ntatoka kwenye kisima hiki watumishi wengi mishahara ovyo no posho usafiri nauli zimepanda
 
Back
Top Bottom