Dar es salaam limegeuka jiji la makelele, Serikali imelala?

Usafiri ukiboreshwa miundombinu ikiwa safi hata unaweza ukaishi Ikwiriri na kazi ukafanyia Dar !
 
Umesahau na wanaohubiri dini, hii yote ni kutokana na kuwa na rc mshamba.
 
Usiisahau misikiti na makanisa.
Waguse kote Ila sio hapo mkuu, msikiti ni achana ya dakika mbili, mara tano Kwa siku.
Which means is not a problem.

Kanisa ni sehem takatifu, Taifa letu linahitaji maombi, ili kutoka katika hatua tuliopo.

Bila hayo maombi hata Amani hii isingekuwepo
 
Ushaambiwa jiji la biashara then unalalamika kelele.
Hamia Mtwara/Lindi ambako kumetulia.
Dar ina wakazi 6M, wewe lonely ndo hupendi kelele.
Dar ni Jiji la biashara kuliko majiji kama Dubai na Tokyo?
Mbona huko hakuna hivyo vispika na makelele?

Kuna mdau huko juu amesema hali hiyo ya makelele na kupenda makelele ni dalili ya ujima na umasikini,nakubaliana nae kwa asilimia mia moja.
 
Mkuu hujakaa karibu na ile misikiti ya "swalaa, swalaa, kitanda chako ndiyo kaburi, shuka ndiyo sanda yako, swalaa swalaaa" wanakupigia makelele saa nzima sala ya alfajiri, bila kujali una imani gani?

Maombi hayatambuliki kwa wote katika secular state. Maombi yenu ombeni kanisani kwenu msiwapigie kelele wengine wasioamini kama nyie.
 
Hata Congo, Yemen, Palestina na Sudan wanaomba sana.
Halafu hamuwezi kuomba bila kelele??
 
Na bado! Saa100 Hana ustaarabu na umakini kwenye uongozi!
Tunaandika Jf Kila kukicha,ni malalamiko ila serikali haisomi na haifuatilii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…